Home » » MAZOEZI YA JESHI LA POLISI MJINI IRINGA YAWACHANGANYA WANCHI

MAZOEZI YA JESHI LA POLISI MJINI IRINGA YAWACHANGANYA WANCHI

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Thursday, November 7, 2013 | 10:53 PM

Taarifa  zilizotufikia  kutoka mjini Iringa hivi  punde zinadai  kuwa  mazoezi  la  kupambana na majambazi yanayofanywa na jeshi la  polisi mjini Iringa eneo la Hazina  ndogo  yamewachanganya  wananchi  na  kujikuta  wakitaharuki  kwa  hofu ya  kuvamiwa na majambazi.

Polisi  hao  ambao  wanaigiza  kuvalia  nguo kama majambazi huku  wengine  wakiigiza  kupambana na majambazi  hao na mmoja kati ya muigizaji  wa ujambazi  kuigiza  kuuwawa huku  tukio  limeonyesha  kuwakimbiza  wananchi .

Mpasha  habari  wetu  wa www.matukiodaima.com  kutoka mjini  Iringa anadai  kuwa  wakati polisi  wakitaka  kuondoka  eneo la tukio baada ya  kufanikiwa  kuzima jaribio  la uigizaji wa  kupambana na majambazi hao  gari  lao lilizima na kupelekea  wananchi  kulizingira  gari  hilo  wakitaka  kuona maiti ya aliyeuwawa katika maigizi hayo.

kamanda  wa  polisi  wa  mkoa  wa Iringa Ramadhan Mungi  ameuthibitishia mtandao  huu  wa www.matukiodaima.com  kwa  njia ya simu  kuwa  hakuna  utekeji  wala jambazi aliyeuwawa katika jaribio hilo .

Mungi  alisema  kuwa kilichofanyika  na mazoezi  ya  kupambana na ugaidi  na matukio ya  ujambazi zoezi  ambalo  linafanyika nchi  nzima.

Wakati  huo  huo huku  Ubaruku  Mbarali  Mbeya  nako mambo  si shwari  baada ya  kutokea  vurugu  kubwa  zilizopelekea  nyumba kadhaa kuchomwa  moto  na nyingine  kuvunja  wa na  wananchi  wakipinga hatua ya mwekezaji kumpiga  risasi  mmoja kati ya  wananchi  wakati  wakipinga hatua ya mwekezaji kufunga mfereji wa umwagiliaji
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA