Home » » MAKADA CHADEMA JIMBO LA IRINGA MJINI WAJIUNGA CCM ,WAMPIGA MAKOMBORA MAZITO MBUNGE MCHUNGAJI MSIGWA

MAKADA CHADEMA JIMBO LA IRINGA MJINI WAJIUNGA CCM ,WAMPIGA MAKOMBORA MAZITO MBUNGE MCHUNGAJI MSIGWA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, November 26, 2013 | 6:20 PM 
 Mwenyekiti  wa CCM mkoa wa Iringa  Jesca Msambatavangu  akiwapokea  makada wa Chadema jimbo la Iringa mjini  walioamua  kuachana na Chadema na kujiunga na CCM
 Maandamano  ya  boda boda na magari  katika  kuhitimisha  mbio za Bendera  ya  CCM mkoa  wa Iringa
 Wananchi  wa maeneo ya  Miyomboni  eneo la mashine  tatu  wakishuhudia msafara wa Bendera  ya  CCM  ukipita  eneo hilo
 Makada wa Chadema  wakisalimisha kadi zao kwa mwenyekiti wa CCM mkoa  wa Iringa Bi Jesca Msambatavangu
 Umati  mkubwa wa  wananchi waliojipanga  barabarani  wakati  wa msafara  wa bendera  ukipita
 Msafara  wa bendera  katika  manispaa ya  Iringa
 Wananchi  wakiwa katika mkutano  wa  kilele  cha mbio za bendera  mkoa  wa Iringa

 Vijana  walioshiriki  kukimbiza  bendera ya CCM mkoa  wa Iringa
Kada  wa  Chadema katikati Violeth Mwakisyala akiwa ameungana na wana CCM kuweka alama ya dole baada ya  kujivua Chadema na  kujiunga CCM
Kada wa CCM Bw  Julio Elieza kushoto akisoma maandishi ya CHANA GWANDA NA GAMBA NA  VAA UZALENDO mara  baada ya kujiunga na CCM akitokea Chadema
 kada  wa Chadema  Bw Mmasi akionyesha kadi  yake ya  Chadema kabla ya kujiunga na  CCM katika  kilele  cha mbio  za bendera
 Mwenyekiti  wa  CCM mkoa wa Iringa  akimkaribisha  CCM Bi Violeth  baada ya  kujiengua  Chadema


 Makada  na  wapiganaji  wa Chadema  waliojiunga na CCM
 Kiapo cha  utii  kwa  waliojiunga na CCM kutoka  vyama  mbali mbali
 Kiongozi  mkuu wa mbio  za bendera  Alli  Simba akijiandaa kumkabidhi  bendera diwani  wa kata  ya Makorongoni Bw Thadeus Tenga  ili akabidhi kwa  mwenyekiti  wa CCM mkoa
 Tenga  akijiandaa kupokea  bendera  toka kwa Simba
 Mwenyekiti wa CCM mkoa  wa Iringa  Jesca Msambatavangu kulia akipokea  bendera  toka kwa diwani wa kata ya makorongoni na kiongozi wa  mbio hizo
MBUNGE wa jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa amerushiwa makombora na baadhi ya wanachama wa chama hicho ambao juzi walitimkia Chama cha Mapinduzi (CCM).
 
Makombora hayo yalirushwa katika uwanja wa Mwembetogwa mjini hapa, wakati CCM Mkoa wa Iringa ikihitimisha mbio zake za bendera ya CCM.
 
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu  alisema lengo la mbio za bendera ya CCM ni kuhamasisha amani na utulivu nchini.
 
Malengo mengine ni kukagua utekelezaji wa Ilani ya chama hicho unaofanywa na serikali, kuhamsisha vijana kujiajiri na kuwashukuru watanzania kwa kuendelea kuinga mkono CCM.
 
Katibu Uenezi na Itikadi Mkoa wa Iringa, Dk Yahaya Msigwa alisema jumla ya wanachama 120 kutoka vyama mbalimbali vya upinzani kikiwemo Chadema wamerejea CCM kupitia mbio hizo.
 
Baadhi ya wanachama wa Chadema waliokabidhiwa kadi zao kwenye hitimisho la mbio hizo zilizoanza miezi miwili iliyopota ni pamoja na Ibrahim Mmasi na Vaileti Mwakisyala.
Akirusha makombora kwa Mchungaji Msigwa, Mmasi alisema ni kiongozi asiyeambilika huku akimtuhumu kwamba ni mroho wa madaraka .
 
Mmasi alisema wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2010, Mchungaji Msigwa aliwatuhumu baadhi ya viongozi akiwemo aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini Monica Mbega (CCM) kwa kuwa na vyeo vingi vya kisiasa hali iliyosababisha ashindwe kutekeleza wajibu wake kwa wananchi.
 
“Wananchi walimsikia Mchungaji Msigwa na kumpa ubunge, lakini baada ya kupata nafasi hiyo anazidi kujilimbikizia vyeo hali inayofinya demokrasia ndani ya chama,” alisema.
 
Akivitaja baadhi ya vyeo vya mbunge huyo, Mmasi alisema mbali ya kuwa mbunge, Mchungaji huyo ni diwani, mwenyekiti wa chama hicho wilaya, mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na waziri kivuli.
 
Alisema hali ya kisiasa ndani ya chama hicho wilayani hapa na mkoani kwa ujumla sio nzuri kwa kuwa hakuna demokrasia ya kukosoa na kukosolewa.
 
“Kuna udikteta wa mawazo, watu wakisema ukweli wanachukiwa, mambo hayako shwari hata kidogo,” alisema.
 
Alisema kuna viongozi ambao hawapikiki chungu kimoja na mchungaji Msigwa, hawasalimiani, hawaaminiani kwa kile kinachoelezwa kwamba hapendi kukosolewa.
 
Huku akishangiliwa na baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo, Mmasi alisema kabla ya Uchaguzi Mkuu ujao, Chadema mjini Iringa itakuwa imesambaratika.
 
“Uchaguzi ndani ya chama hicho umekaribia, waliopo na tuliokuwepo tunajua kinachoendela, hali sio nzuri kwasababu wanachama walio wengi wanataka mabadiliko, hali hiyo haitawaacha salama,” alisema.
 
 huku   wanachama   zaidi  ya 200 wapya  wakijiunga na  chama  hicho  huku  baada ya  makada  wa chama  cha  Demokrsani na maendeleo (CHADEMA)  wakijiengua katika chama  hicho na kujiunga na CCM.
Makada  hao  wa Chadema  wameeleza  kufurahishwa na utendaji kazi wa serikali ya CCM na kuchukizwa  kile  walichodai ni ubabaishaji wa Chadema katika ngani ya jimbo , mkoa  na Taifa kwa madai  kuwa  vitendo vya kifisadi  ndani ya Chadema  ni moja ya  sababu ya  wao  kujiengua.
Makada  hao wakitumia  muda  mwingi kushambulia  mbunge  wa jimbo la Iringa mjini na  diwani  wa Mvinjeni  na viongozi  wa Chadema  taifa  walisema  kuwa  wamechoshwa na porojo za  viongozi  hao. 
Pia  vijana  hao  walisema  kuwa  wamekuwa wakipokea  vitisho  mbali mbali kutoka kwa  viongozi na makada wa Chadema  pale wanapotaka  kuhamia CCM
   
Msambatgavangu  alisema  kuwa  CCM  mkoa  wa  Iringa  haitawavumilia   viongozi  wa serikali  ambao watashindwa  kutekeleza majukumu yao .
Huku  ikiwatoa  hofu vijana  waliopo upinzani ambao  wanataka  kurudi CCM kuwa  wana uhuru wa kwenda  chama chochote cha  siasa.
 
Kwa kupitia mbio hizo za bendera Msambatavangu alisema jumla ya wanachama wapya 4,000 wamepatikana katika wilaya zote za mkoa wa Iringa, na wanachama zaidi ya 1,000 wamejiunga na jumuiya mbalimbali za CCM
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA