Home » » KISWAGA AJITOLEA BATI ZA KUEZEKA NYUMBA NZIMA YA MWALIMU SHULE YA MSINGI MLANDA JIMBO LA KALENGA

KISWAGA AJITOLEA BATI ZA KUEZEKA NYUMBA NZIMA YA MWALIMU SHULE YA MSINGI MLANDA JIMBO LA KALENGA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Thursday, November 14, 2013 | 8:36 AM


 Wananchi  wa Mlanga  kata ya Magulilwa  jimbo la Kalenga  wakisaidia  kushusha  bati  zilizotolewa  msaada wa mkazi  wa  jimbo  hilo Bw  Jackson Kiswaga kwa ajili ya kuezeka nyumba  nzima  ya mwalimu  katika  shule ya msingi Mlanda
 Mkazi  wa  jimbo la Kalenga mpanda maendeleo ya  elimu Bw  Jackson Kiswaga  kushoto akikabidhi  msaada wa bati 40  zenye thamani ya zaidi ya Tsh 800,000 uongozi wa  shule ya msingi Mlanda na kijiji  hicho  leo ili kutatua  kero ya nyumba za  walimu  shuleni hapo
 Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mlanda jimbo la Kalenga Shaban Kikoti  akipokea msaada wa bati  kutoka kwa mkazi wa jimbo la kalenga anayeishi jijini Dar es Salaam Bw Jackson Kiswaga  leo

Bw  Kiswaga  akikabidhi  msaada wa mpira kwa viongozi wa serikali ya kijiji  cha Mlanda leo kwa ajili ya kuwawezesha  vijana  kujishughulisha na michezo baada ya kazi nzito 


MKAZI  wa  jimbo la Kalenga  anayeishi  jijini Dar es Salaam Bw Jackson Kiswaga  amekabidhi msaada wa bati 40 zenye thamani ya  zaidi ya Tsh 800,000 kwa viongozi wa kijiji  cha Mlanda  kwa ajili ya  kuezeka  nyumba ya mwalimu kama  njia ya kutatua  kero ya uhaba wa nyumba kwa walimu  shuleni hapo.

Akikabidhi msaada  huo  leo mbele ya  viongozi wa serikali ya kijiji  na  shule  hiyo ,Kiswaga  alisema  kuwa amelazimika  kutimiza ahadi  hiyo  baada ya  kuombwa na wananchi  wa kijiji  hicho kwa njia ya barua .

Alisema  kuwa ameguswa na tatizo la uhaba  wa  nyumba za  walimu  shuleni hapo hivyo kutoa  kwake  bati  hizo 40  zitawezesha  kukamilisha  kuezeka  nyumba  mmoja ya  mwalimu  iliyojengwa kwa  nguvu za  wananchi  wa kijiji  hicho.

 Mwalimu mkuu  wa shule  hiyo Shaban Kikoti  alisema  kuwa   msaada  huo  utatatua  kero ya nyumba ya mwalimu  ambayo  ilikamilika  toka mwaka  jana  ili bati  ilikuwa tatizo .

Hata  hivyo  alisema  shule  hiyo bado inakabiliwa na changamoto ya madawati 100  ili  kupunguza tatizo la  wanafunzi  kukaa chini .

Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA