Home » » AJALI YAUA WAWILI YAJERUHI ZAIDI 28 IRINGA

AJALI YAUA WAWILI YAJERUHI ZAIDI 28 IRINGA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, November 5, 2013 | 8:55 AM


AJALI mbaya  imetokea  katika  eneo la Nzihi wilaya ya  Iringa  vijijini  mkoani  Iringa  jioni ya leo kwa basi  la kampuni ya Runda  kufeli  breki  wakati  likishuka  mteremko  wa Nzihi na  kuligonga  daladala  lililokuwa  limesimama  mwanzo  wa mteremko  huu.

Kamanda wa  polisi  wa  mkoa  wa  Iringa Ramadhan  Mungi ( Pichani)  amethibitisha   kutokea kwa ajali hiyo na kuwa  ajali   hiyo imetokea majira ya saa 11  jioni wakati basi hilo  likishuka mteremko huo.

Kamanda  Mungi akizungumza na mtandao huu  wa www.francisgodwin.blogspot.com  amesema  kuwa  katika ajali  hiyo  watu   wawili akiwemo mwanamke  mmoja na mwanaume  mmoja  ndio  ambao   wamepoteza maisha   huku  madereva  wa magari  hayo mawili wote  wakiwa  wamevunjika  miguu  yao.

Amesema kuwa majeruhi  zaidi ya 28 wa ajali  hiyo  wamelazwa katika Hospital ya Ipamba  na  baadhi  yao  wamekimbizwa katika  Hospital  ya  rufaa ya  mkoa  wa Iringa na  kuwa hali  zao  zinaendeleza  vizuri.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA