Home » » WANAHABARI IRINGA WALIBANA GAZETI LA RAI WATAKA LITAJE MAJINA YA WAANDISHI WALIOHONGWA NA VIONGOZI WA CCM MKOA WA IRINGA

WANAHABARI IRINGA WALIBANA GAZETI LA RAI WATAKA LITAJE MAJINA YA WAANDISHI WALIOHONGWA NA VIONGOZI WA CCM MKOA WA IRINGA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, October 29, 2013 | 6:04 AM


 Mwenyekiti  wa chama  cha  waandishi  wa habari mkoa  wa Iringa Frank Leonard kulia akitoa msimamo  wa  wanahabari dhidi ya  gazeti la Rai na mbunge Msigwa  leo ,kushoto ni katibu mtendaji wa IPC Francis Godwin
 Wanahabari Clement Sanga kushoto akiwa na mwakilishi  wa New habari {2006} Ltd  wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania , Rai  na Bingwa mkoa  wa Iringa Mercy Mwalusamba wakati  wa kikao  cha  cha wanahabari  mkoa  wa Iringa  leo  kujadili habari  zilizoandikwa na gazeti la rai jumapili

 Wanahabari  wakifuatilia kwa makini kikao  hicho

WANAHABARI  mkoani Iringa wamekanusha  vikali habari  zilizoandika na gazeti la Rai  toleo namba 1067 la  jumapili wiki iliyopita kuwa wanahabari  mjini Iringa  wamehongwa fedha na  viongozi  wa CCM mkoa  wa Iringa ili  wasiandike habari ya msaidizi  wa mbunge Wiliam Lukuvi Bw Thom Malenga kukamatwa  kwa  tuhuma  za kujihusisha na ujangili.

Wahanabari  hao  katika  kikao  chao kilichofanyika   leo  katika  ofisi  za klabu ya  waandishi  wa habari mkoa  wa Iringa (IPC) mbali ya  kukanusha habari  hizo  kuwa zimeandikwa kwa  lengo la  kuchafua  tasnia ya habari mkoa  wa Iringa ila bado wanalitaka  gazeti  la Rai  na mbunge wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa  kuwataja  waandishi  waliohongwa na  viongozi  wa CCM mkoa  wa Iringa kabla ya  wanahabari  hao  hawajachukua  hatua zaidi  dhidi ya gazeti  la rai pamoja na mbunge Msigwa.

"Kilichoandikwa na  gazeti la  Rai jumapili kuhusu wanahabari Iringa hawajatutendea  haki na  wametuvunjia  heshima  yetu kwa  wadau  wa habari mkoa  wa Iringa na nje ya  mkoa  wa Iringa.....ila tunachotaka Rai kuwataja  waandishi  hao  waliohongwa  ili sisi kwa  sisi kama  wanahabari  kuanza  kuchukuliana  hatua ....wakishindwa  kufanya  hivyo ndani ya  siku 14  kuanzia  leo jumanne  tutawafikisha  baraza la habari Tanzania (MCT)"

Walisema  wanahabari hao  katika tamko  lao  la pamoja  lililotolewa na mwenyekiti wa IPC Frank  Leonard  kuwa taarifa  hiyo  imechafua  vibaya  wanahabari  Iringa na  sio wacache ni  wote  kutokana na jinsi  ambavyo gazeti  hilo lilivyoandika habari hiyo tena mbaya  zaidi mwandishi  wa habari  hiyo hakuweza kuwatendea haki  wanahabari Iringa hata  kwa kuonyesha  kuwahoji katika habari  yake hiyo.

Leonard alisema  kuwa si  kweli kama  wanahabari Iringa walishindwa  kuandika habari hiyo ya  kukamatwa kwa Malenga isipo  kuwa wanahabari  Iringa ni makini na hawakutaka kuandika habari kwa  kukurupuka hivyo walitaka  kabla ya  kuandika kuweza kumpata msemaji wa kikosi  hicho cha kupambana na ujangili  ili kulizungumzia hilo kabla  ya  kuandika jambo  ambalo  wao kama  wanahabari  walikuwa  wakilisikia  mitaani bila  kuwa na uhakika.

Uandishi  wa habari  mzuri ni pamoja na  kuzingatia maadili  ya uandishi na  sio kuandika bila  ya  kuwa na uhakika  wa kile  unachokiandika .

Hata  hivyo alisema  kwa kuwa mbunge Msigwa amenukuliwa katika  gazeti hilo kama  ndio msemaji wa jambo  hilo wao kama  wanahabari watamwandikia  barua mbunge  huyo  ili kusaidia  kuwataja wanahabari  waliohongwa  pesa vinginevyo wao kama  wanahabari  wa mkoa  wa Iringa hawatamvumilia mbunge Msigwa katika  hilo .

Pia  alisema  kuwa suala  hilo kwa  sasa  ameachiwa mwanasheria  wa IPC ili  kulifanyia kazi ikiwa ni pamoja  na  kuwaandikia barua Rai na mbunge Msigwa kuwataka  kuthibitisha ukweli  wa kilichoandikwa  dhidi ya  wanahabari mkoa  wa Iringa.

Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA