Home » » VETA IRINGA NAOMBA SABABU ZA MSINGI ZA KUVINYIMA USAJILI VYUO HIVI NA KUVIPA USAJILI VILE.....

VETA IRINGA NAOMBA SABABU ZA MSINGI ZA KUVINYIMA USAJILI VYUO HIVI NA KUVIPA USAJILI VILE.....

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Sunday, October 20, 2013 | 2:45 AM

AWALI  ya  yote  ninapenda  kuwaomba  radhi  wasomaji  wa  safu  hii kwa  kutuweka mwendelezo wa makala  haya  katika  safu  hii kwa juma mbili  sasa  kutokana na sababu zilizo nje  na uwezo  wangu ila pia  vitisho kutoka kwa  baadhi ya  wahusika wanaoguswa  moja kwa  moja na sakata  hili japo natamka  wazi sitaogopa vitisho daima  nitasema kweli tupu.

Kwa  yeyote anayeana anaonewa  katika hili nitamwomba atangulie mahakamani mimi  nipo  nyuma yake kuja kueleza ukweli nasema siku  zote  ukweli hauna  urafiki na uongo na ukweli  utakuweka  huru   daima.

Baada  ya  kusema  hayo  sasa  naomba  leo kuelezwa sababu  ya VETA Iringa kuvinyima  usajili japo  wa barua  vyuo vya  Hotel na utalii kama Delima na Ruaha  na   kuvita vyuo ambavyo hata  kwa macho  havionyeshi  kuvifikia vyuo  hivi  Iringa ?

Moja  kati ya  sifa  ya  kuitwa  chuo  cha Hotel na utalii ni pamoja na  kuwa na darasa  kubwa ,walimu  wenye sifa  ,vifaa vya  kufundishia na kujifunzia  nk  sasa naomba  kutoka nafasi  kwa  mkurugenzi wa kanda ya nyanda  za  juu Bi Veronica Mbele na  timu  yake  kupita  leo katika  vyuo  vyote na kuangalia kama  vyuo   vya  Hotel na utalii  Iringa  vinasifa japo  hizo  chache  ama sifa  zake  zimepitiliza  zaidi ya hizo?

Delima na Ruaha  nimevichukulia kama  ni vyuo  vya mfano  kwa leo ambavyo binafsi  baada ya  kupita  na kutazama sifa hizo chache kati ya nyingi  ambazo  binafasi  nilipata  kuchunguza usiku na mchana  nikaona ni  heri hivi  kuliko vile vilivyopewa usajili na leo  kujitangaza  kuwa  vimesajiliwa .

Naomba  kwa  leo  niishie  hapa japo nitaendelea  tena  wiki ijayo kwa  kuvitaja  vyuo  viwili  vingine  ambavyo hivi havina  sifa  kabisa  ila wenyewe  wanadai vimesajiliwa pia  wiki ijayo  tutaweka  na picha ya  vyuo  hivyo kwa  wale  wanaopenda  kutoa vitisho karibuni kwa  vitisho  ila sitaongopa vitisho.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA