Home » » RC NJOMBE AWATAKA WANASIASA KUHAMASISHA WANANCHI KUJIUNGA NA MFUKO WA AFYA YA JAMII MIJINI (TIKA)

RC NJOMBE AWATAKA WANASIASA KUHAMASISHA WANANCHI KUJIUNGA NA MFUKO WA AFYA YA JAMII MIJINI (TIKA)

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Wednesday, October 2, 2013 | 4:35 AM


 Kaimu meneja  wa mfuko  wa Taifa  wa  bima ya afya  (NHIF) mkoa  wa  Iringa Emmanuel  W. Mwikwabe (kulia ) akitoa  ufafanuzi  wa jambo mbele ya mkuu  wa mkoa wa Njombe kepten Mstaafu Asser Msangi kushoto leo nje ya  ukumbi wa RC Makambako
 Mkuu  wa  wilaya ya Njombe  Sarah Dumba  (kushoto) akiteta jambo na mmoja kati ya watenda kazi wa NHIF Iringa nje ya  ukumbi wa RC Makambako
 Utambulisho wa  wageni mbali mbali  waliofika katika  warsha  hiyo ukifanyika
 Washiriki  wa  warsha  hiyo ya mfuko wa Afya  ya jamii mjini (TIKA) mjia Makambako  leo
 Meneja  wa mfuko  wa Taifa  wa  bima ya afya  (NHIF) mkoa  wa  Iringa Emmanuel  W. Mwikwabe akieleza  faida  ya TIKA mbele  ya washiriki
 Sekretarieti ya  NHIF 
 
 Meza kuu   ikifuatilia  warsha ya  mfuko  wa Afya ya jamii mijini (TIKA) leo
 Mwakilishi  kutoka TAMISEMI Edwin Mgendera mkurugenzi msaidizi  idara  ya huduma na  sheria akijitambulisha  rasmi

 Mkuu  wa mkoa  wa Njombe Bw  Msangi katikati akiwa katika picha ya pamoja na makundi mbali mbali ya  washiriki
 Meneja  wa  CHF  kutoka NHIF Bw  Constantine Anthon Maleda akitoa  mada  juu ya  TIKA


serikali  ya  mkoa  wa Njombe  iimewataka   wanasiasa  katika mkoa  huo  kuendelea  kuhamasisha  wananchi kujiunga na mfuko wa    afya  ya  jamii (CHF) unaowalenga  wananchi  wa vijijini na ule wa tiba kwa kadi (TIKA) kwa  mijini.

Mkuu  wa mkoa  wa  Njombe  kepteni mstaafu Asseri Msangi  alitoa ratiba  hiyo mara  baada  ya kufungua warsha   warsha ya  uanzishaji  wa mfuko wa  afya ya  jamii mijii (TIKA)   katika mji wa  Makambako  mkoani  Njombe  kwenye   ukumbi wa RC mjini Makambako  mkoa  wa Njombe leo

Alisema  kuwa  serikali  kjupitia  wizara  ya afya  na  ustawi  wa  jamii imeandaa mfumo huo wa tiba kwa  jamii ili  kuisaidia  jamii  kuweza  kupata matibabu pale  inapopatwa na matatizo ya  kifya na  kuwa katuka nchi  zote  duniani  hakuna nchi hata  moja ambayo inatoa bure  huduma za afya  kwa wananchi  wake ukiacha nchi  ya Libya ambayo ilikuwa ikitoa bure matibabu  ila kwa  sasa huduma  hiyo katika nchi hiyo pia haipo.
Hata  hivyo  mkuu huyo wa  mkoa  aliwataka madiwani katika kuweka  usawa  mzuri katika  uchangiaji  wa  huduma  za afya kupitia  huduma  hiyo  tiba kwa kadi  ili  kuwawezesha  wananchi  wengi  kujiunga na mpango  huo.
Kaimu meneja  wa mfuko  wa Taifa  wa  bima ya afya  (NHIF) mkoa  wa  Iringa Emmanuel  W. Mwikwabe   akielezea  juu ya makusanyo ya  NHIF katika  mkoa wa  Njombe  alisema kuwa  kwa  mwaka 2012/2013 kiasi  cha Tsh milioni 428 zimekusanywa  katika wilaya ya  Makete ,Njombe mji na Halmashauri ya  wilaya ya Njombe pamoja na Ludewa.

Alisema  kuwa fedha  hizo  ni makusanyo ya mfuko wa NHIF na  CHF  ambapo katika  wilaya ya  Makete  jumla ya  Tsh  milioni 70.2  za NHIF zilikusanywa na Tsh milioni 28 za CHF  zilikusanywa na kufanya  jumla kuu kwa  wilaya  hiyo kufikia  Tsh milioni 98.2.

Wakati  wilaya ya  Ludewa  makusanyo  ya NHIF  ilikuwa ni Tsh miliioni 78 na CHF ilikuwa ni Tsh milioni 47  na  kufikisha  jumla ya Tsh milioni 125 na  wilaya ya  Njombe mji  makusanyo ya CHF ilikuwa ni milioni 1 na NHIF ilikuwa ni kiasi cha Tsh. milioni 94.8 na Halmashauri  ya Njombe  fedha  za CHF ni  Tsh.milioni 2 na NHIF ilikuwa Tsh.milioni 106.9

Hivyo  alisema kumekuwepo na mwitikio mkubwa  wa wananchi  kujiunga na mifuko  ya  CHF na NHIF hivyo  ni imani yake  iwapo uhamasishaji utafanyika  vema kwa  mfuko  huo wa TIKA pia  wananchi  wengi  watajiunga   na kunufaika  zaidi.
Alizitaka  Halmashauri  kuwa na mikamkati ya  kuboresha  huduma ya  upatikanaji  wa dawa ,vifaa tiba  ,uhusiano mzuri kati ya  watoa  huduma na  wagonjwa   ili  asilimia 30 ya  Halmashauri ziwe na  mikakati  na mbinu  endelevu ya  uhamasishaji  inayoshirikisha  jamii  kwa ujumla.
Meneja  huyo alisema kuwa   fedha  za makusanyo  yatokanayo na CHF na NHIF asilimia 2 ya  3 kununua  dawa  na usimamizi  wa  upatikanaji  na matumizi ya  dawa  (CHMT's)
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA