Home » » RAIS KIKWETE AWAONYA WAWEKEZAJI WA LIGANGA LUDEWA AWATAKA KABLA YA KUWAHAMISHA WANANCHI KUWAJENGEA NYUMBA BORA ,MBUNGE FILIKUNJOMBE AWAKOMALIA ZAIDI

RAIS KIKWETE AWAONYA WAWEKEZAJI WA LIGANGA LUDEWA AWATAKA KABLA YA KUWAHAMISHA WANANCHI KUWAJENGEA NYUMBA BORA ,MBUNGE FILIKUNJOMBE AWAKOMALIA ZAIDI

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Wednesday, October 23, 2013 | 1:58 AM


Rais Kikwete akiwa  katika  pozi kwenye mgodi wa chuma eneo la Mndindi Ludewa mkoani Njombe jana  ,nyuma na mgodi  wa chuma
Rais Kikwete kushoto akipata maelezo  kutoka kwa wawekezaji  wa kichina katika mradai wa Liganga Ludewa kulia wa kwanza ni mbunge wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe  akifuatilia kwa karibu mazungumzo hayo
Rais Jakaya Kikwete  wa tano  kulia akiwa  katika picha ya pamoja na watenda kazi  wa kampuni ya kichina ambao  wanasimamia mradi wa kufua  chuma eneo la Liganga kijiji cha Mndindi  Ludewa mkoani Njombe  wa kwanza kulia ni mbunge wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe na wa tatu kulia ni naibu waziri wa Nishati na madini GEorge Simbachawene  anayefuata ni mzee Mzindakaya
Mkuu  wa Trafiki Ikulu Kedmundi Mnubi akiongoza msafara  wa Rais Jakaya Kikwete
Rais Jakaya  Kikwete  katikati akiwa na mbunge wa jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe na mzee Mzindakaya ambae ni mtendaji wa NDC  jana katika eneo la Liganga kijiji cha Mdindi Ludewa mkoani Njombe ,nyuma ni mdogo wa chuma
Rais Kikwete akisisitiza jambo kuhusu kuwahamisha wananchi  wanazunguka mradi huo
Rais  Kikwete  akitoka kutembelea maradi wa Liganga kijiji cha Mndindi Ludewa
Huu ni mgodi wa chuma
Wananchi  wa Mndindi  Ludewa  wakimshangilia  Rais Kikwete
Rais Kikwete  akiwahotubia wananchi wa kijiji cha Mndindi Ludewa
Mkuu  wa Trafiki Ikulu Bw Kedmund Mnubi akiwa jirani na mgodi wa chuma Liganga Ludewa
Kikosi cha  wanahabari  waliopo katika msafara wa JK  wakiwa katika  picha ya pamoja na mzee wa matukio daima wa tatu kushoto  na mzee  wa TBC Mbeya Hosea Cheyo wa tatu  kulia
Mwanahabari wa radio Ice Fm Brighter Nyoni akiwafuatilia mambo katika  msafara wa JK kituo hiki cha Radio kipo Makambako Njombe na ni miongoni wa vituo vinavyofanya vyema  nyanda za juu  kusini chini ya mkurugenzi wake mwanahabari Mic
Naibu  waziri wa Maji Dr Binilith Mahenge akipozi kwa picha eneo la mgodi wa  chuma Ludewa
Rais Kikwete na mtoto wa mwekezaji wa kichina katika mradi wa Liganga Ludewa
Wananchi  wakiwa  wamezuia msafara  wa JK eneo la Shauri Moyo Ludewa  huku watoto  wakipanda juu ya miti  kumwona Rais wao
Rais Kikwete akipiga picha na wauguzi wa na walimu


RAIS  Jakaya  Kikwete  awaonya   wawekezaji  wa kichina  katika  maradi  wa Liganga wilaya Ludewa  kuwa hatapenda  kuona  wawekezaji hao  wakiwaondoa  wananchi  wa kijiji  cha wa Mndindi na Amani wanaozunguka  mgodi  huo  wa  chuma bila kujengewa  nyumba  za  kisasa  wala  kutafutiwa makazi yenye hadhi .
Rais  Kikweli alitoa  onyo hilo  jana   kufuatia  maombi ya  mbunge  wa   jimbo la Ludewa  DEo Filikunjombe  aliyetaka  serikali  kuwahakikishia makazi bora  wananchi  watakaopisha   eneo hilo la madini ya  chuma  kwa kuhakikisha  wanajengewa  nyumba  za kisasa na  sio  kuwajengea  tena  nyumba za miti na udongo kama  ambazo  wataziacha  sasa.
Kwani mbunge Filikunjombe alisema  kuwa imekuwa ni kawaida ya  wawekezaji  waliowengi  kuwalipa  fidia ambayo imepita na wakati  wananchi huku  wakijua  wazi  kuwa maisha ya  sasa  yapo juu na hayalingani na kiwango cha  fidia  ambazo  zimekuwa  zikilipwa  kwa  wananchi  wanaopisha  miradi mbali mbali.
“Mheshimiwa  Rais Kikwete  nashukuru  sana  umefika  hapa  Linganga   na kuona jinsi mradi unavyo endelea  kufanya kazi  hivyo  hawa  wananchi wa Mndindi na Amani  wanapaswa  kuhama makazi yao na  kuandaliwa  makazi mapya  …ila  wapo ambao  nyumba  zao zimejengwa zaman kwa miti na udongo  na  hawana huduma  ya maji  hivyo ombi langu kama mbunge namba wawekezaji hao iwapo watataka  kuwahamisha wananchi wangu  kwanza  kuhakikisha  wanawaandalia makazi  bora  kwa  kuwajengea  nyumba  za kisasa  na sio  kuwajengea  ama  kuwalipa fidia kutokana na nyumba  walizowakuta nazo”
Pia  mbunge  huyo aliwataka  wananchi watakaolipwa  fidia  kwa  ajili ya  kupisha shughuli za machimbo hayo ya linganga kuhakikisha   wanatumia  vema  fedha  hizo badala ya  kufanya kama  wenzao  wa lipisha machimbo ya makaa ya mawe  ambao badhi yao  badala ya  kujenga  nyumba  wakatumia  fedha  hizo  kwa ajili ya kuongeza wake na baada ya fedha  kumalizika  wakaanzisha mgogoro na mwekezaji kuwa fedha  walizolipwa na  kidogohawajafanyia  chochote .
Katika  hatua  nyingine Mbunge Filikunjombe  alipongeza  jitihada  mbali mbali  zinazofanywa na Rais KIkwete katika  kuwahudumia  watanzania na kuwaonya  wapinzani ambao  wameendelea kupinga  jitihada za serikali ya  CCM wakati  wao wenyewe ni  miongoni  mwa  watanzania  wanaoendelea  kunufaika na  matunda  ya kazi ya  serikali iliyopo madarakani.
Kuhusu  ujenzi  wa  chuo cha  Veta  katika  eneo  la Shauri  moyo Ludewa  mbunge huyo alimpongeza Rais Kikwete na  kuwa  ujenzi  wa  chuo  hicho ni ukombozi mkubwa  kwa  wana  Ludewa katika kukuza  ajira kwa vijana na kuongeza kasi ya maendeleo ya  wilaya  hiyo.
Aidha Mbunge  Filikunjombe  awaliwashukia waqwekezaji hao  wa Kichina  kwa kuwataka  kuiga mfano wa  mwekezaji mdogo mzalendo MMI ambae  amekuwa akisaidia  jamii ya  wana Ludewa kwa shughuli mbali mbali  za kimaendeleo  na kuwa wana Ludewa hawataona faida ya  kuwa na mwekezaji mkubwa  kutoka China ambae hasaidii chochote kama kuchangia miradi ya maendeleo ya  wana Ludewa.
" Mheshimiwa Rais napenda  kumpongeza  sana mbele yako mwekezaji mdogo  wa kampuni ya MMI kwa  jinsi ambayo  endeleo kuwa karibu na wananchi kwa  kuchangia miradi ya maendeleo ya wana Ludewa kama elimu , afya  na mingine  sasa nawaomba hawa  wachina nao  kuinga mfano  huo"
 
Kwa upande  wake  Rais  Kikwete  mbali ya  kuungana na mbunge  Filikunjombe  katika  kuwatetea   wananchi wanaopisha miradi hiyo bado  alisema  kuwa ili  wananchi hao  waweze kuhamishwa maeneo yao  lazima kujengewa  nyumba za kisasa na  wale  wanaoishi katika  nyumba ya  vyumba   viwili kwa  sasa  kujengewa  nyumba  ya  vyumba  vinne na  wale  wanaoishi katika nyumba ya vyumba  sita basi  kuongezwa  vyumba sita  vingine na   sio kuwajengea  nyumba kama  ile ya mwanzo.
Pia  alisema  kuwa kabla ya  kuwahamisha  lazima mwekezaji  huyo wa kichina  kuhakikisha eneo ambalo  wanapelekwa  wananchi hao ambao ni wakulima  kuandaliwa maeneo yanayoenda sambamba nay a  sasa kwa maana  maeneo  yenye mashamba ikiwa ni pamoja na kusaidiwa  kulimiwa mashamba yao kwa awamu ya kwanza ,kujengewa  shule  zenye  nyumba  za  walimu na kuwekewa  miundo mbinu yote  na si vinginevyo.

Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA