Home » » RAIS KIKWETE AHITIMISHA ZIARA YA MKOA WA NJOMBE APONGEZA JITIHADA ZA MAENDELEO

RAIS KIKWETE AHITIMISHA ZIARA YA MKOA WA NJOMBE APONGEZA JITIHADA ZA MAENDELEO

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Wednesday, October 23, 2013 | 1:59 AM


Rais Kikwete  akizungumza na viongozi wa mkoa  wa Njombe katika majumuisho ya ziara  yake mkoa wa Njombe
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe  Deo  Sanga  akimpongeza mkuu wa mkoa wa Njombe Aser Msangi  kulia kwa kazi nzuri anayoifanya ya  kuendeleza mkoa wa Njombe
Viongozi  wa  mkoa wa Njombe  wakisubiri kumpokea  Rais Kikwete  katika ukumbi wa Halmashauri
Rais  Kikwete  akisikiliza kwa makini maelezo ya  mwenyekiti wa CCM mkoa  wa Njombe
Mwenyekiti wa CCM mkoa  wa Njombe  Deo Sanga  akimpongeza mkuu wa mkoa  wa Njombe Aser Msangi na mkuu wa wilaya ya Njombe Sarah Dumba mbele ya JK kuwa ni watendaji  wazuri
 ........................................................................................................


Rais  Jakaya  Kikwete amehitimisha  ziara yake  mkoani Njombe  kwa  kupongeza  jitihada  kubwa  za maendeleo  ambazo zimeendelea  kuonekana katika mkoa huo.
Mbali  ya  kupongeza jitihada  hizo pia alisema  kuwa  serikali yake  itaendelea  kuwa  karibu na  wananchi   wa mkoa  wa Njombe na  watanzania  kwa ujumla  na  kuwa  sehemu  kubwa ambayo amepata kupita  katika  wilaya  za  mkoa  wa Njombe  wananchi  wanalalamikia  soko la mahindi na  kuendelea  kudai  fedha  zao kwa wakala  wa mazao  ya chakula.
Rais  Kikwete ametoa  pongezi  hizo leo  katika  ukumbi wa Halmashauri ya  wilaya ya  Njombe wakati  wa majumuisho ya  ziara  yake siku  sita  katika  mkoa  wa Njombe
Alisema kuwa  tayari  mchakato  wa kuwalipa wakulima  madeni  yao ya mahindi  waliouza kwa  wakala  wa chakula na amepata  kuwasiliana na waziri  wa  fedha  Dr  Wiliam Mgimwa  ili  kuona  wakulima  hao wanmalipwa  fedha zao.
Aidha  amesema  kumekuwepo na maombi ya  wakulima  kuwa wana mahindi ambayo yamekosa  soko na kuiomba  serikali  kununua mazao  hayo japo ni  wazi  serikali imekuwa ikinunua mahindi kwa ajili ya akiba na tayari zoezi hilo la kununua mahindi kwa akiba  limekamilika.
Alisema kuwa hadi sasa  tayari tani  zaidi ya  4000  zimenunuliwa nab ado tani 49000 hivyo  wakati wakiendelea na zoezi hilo atawashauri  kwenda  kununua mahindi hayo ambapo hata  hivyo tani  zaidi ya 300,000 za mahindi ya  wakulima wa  mkoa  wa Njombe hazitanunuliwa na serikali hivyo  kuwataka  viongozi wa  mkoa wa  Njombe  kutafuta  soko kwa  watu  binafsi.
Hata  hivyo alisema kuwa awali  serikali iliweka  vizuizi  barabarani kuzuia  mahindi kutoka nje  ila  baada ya uchunguzi   imebainika  kuwa zoezi hilo  linawanufaisha  wale  weanaokaa katika  vizuizi   huku mahindi  yakiendelea   kupita .
Pia  rais Kikwete  aliwahakikishia  wakulima  kuwa  serikali kwa  mwakani imejipanga  kuanza  kununua  mahindi  mapema  zaidi na kuwa  haitaweka  akiba ya  mchele  katika maghala  ya  Taifa  isipo  kuwa kwa mkoa wa Dodoma  watanunua  mtama  kama akiba
Hata  hivyo rais  Kikwete  amepongeza  jitihada za kuendeleza zao la pareto katika mkoa  huo na kupiga marufuku wale  wote  wanaonunua pareto  moja kwa moja kutoka kwa  wakulima  huku  wakikwepa  kodi .
Alitaka  viongozi wa Halmashauri  ya Makete na mkoa  kuwabana  watu hao wanaokwenda kulipa kodi na kutaka ofisi zinazotoa vibali  kuweka masharti ya  watu hao  wanaopewa  vibali  vya kununua  zao la pareto  kuripoti  ofisi za Halmashauri ili kulipa kodi.
Kwani  alisema hakuna  serikali inayoendeshwa bila kodi hivyo ni  wajibu  wa  kila mmoja  kulipa  kodi hiyo kupitia zao  hilo la Pareto.
Alisema  ni vema Halmashauri kubuni mbinu  nzuri ya kukusanya mapato yasiyo na usumbufu badala ya  kuendelea  kuwabana  mamalishe  ambao  wanafanya  shughuli  hizo kwa ajili ya kijikimu .
Kuhusu  uendelezaji  wa mazao mengine ya biashara  aliwataka  viongozi  wa mkoa wa Njombe  kubuni mbinu nyingine ya  kubuni mazao ya biashara kama kilimo cha miti ,maua na mazao mengine ya biashara   ili  kukuza uchumi  wa  wakazi  wa Njombe.
“ Msipuuze  kilimo  cha matunda ,nyanya  na mboga  mboga  kwani ni kilimo ambacho kina  faida  kubwa  na kinaweza  kumwezesha  mwananchi  kukuza  uchumi  wake…muwe na mpango  wa  kuendeleza  kilimo cha matunda badala ya  kutegemea  matunda  kutoka Afrika ya kusini na sasa  watanzania  wanakula  sana matunda “alisema  Rais  Kikwete
Alishauri  wilaya ya  mikoa  kuwatumia mabwana shamba  wake katika  kufundisha  wananchi  kulima mazao mapya ya biashara  ikiwa ni pamoja na kutumia  chuo cha Kilimo Uyole  kwa ajili ya  kuwapa mafunzo  hasa  wale mabwana  shamba wanaofundishika  .
Kwani  alisema kuwa  maeneo yote dunia  ambayo  hayana  mazao ya biashara  wananchi  wake  wamekuwa  wakiongoza kwa umasikini.
Alisema  kuwa  moja kati ya mazao ambayo ni  vigumu kupandisha  bei  ni pamoja na mazao ya chakula  ila  mazao ya biashara  mtu anaweza  kuongeza  bei .

" Natumaini  wananchi  wetu  iwapo  watalima mazao  ya biashara  wataweza  kujikwamua  zaidi kiuchumi badala ya  kubaki wakilima  mahindi  pekee ambayo yatamfanya  kuendelea  kuwa masikini.....sisi kama  serikali  tutaendelea kuwaunga  mkono wananchi ambao  wanaendesha  pia mazao ya biashara "

Rais  Kikwete  alisema kuwa mbali ya ziara  hiyo bado atafika  tena katika mkoa  wa Njombe  ili kutembelea  maeneo  yanayolima matunda na mazao mengine ya biashara  kama maua na mengine.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA