Home » » RAIS JAKAYA KIKWETE KUZINDUA RASMI MKOA WA NJOMBE OCTOBA16 /2013

RAIS JAKAYA KIKWETE KUZINDUA RASMI MKOA WA NJOMBE OCTOBA16 /2013

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Wednesday, October 2, 2013 | 1:45 AM

 Mkuu  wa mkoa  wa  Njombe Kepten  Mstaafu Asser  Msangi akitoa  taarifa  ya  uzinduzi  wa mkoa wa Njombe leo katika ukumbi wa RC
.........................................................................................................................................................................

Serikali  mkoa wa  Njombe  imetangaza  ratiba  kamili ya  uzinduzi  wa  mkoa  mpya  wa Njombe ambapo mkoa  huo  sasa utazinduliwa rasmi na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania  Dr Jakaya  Mrisho  Kikwete  Octoba 16 mwaka  huu.

Mkuu  wa mkoa  wa  Njombe Kepten  Mstaafu Asser  Msangi ametoa  taarifa  hiyo leo katika ukumbi wa RC mjini Makambako  kuwa siku ya tarehe 16 mara  baada ya  Rais  Kikwete  kutoka  mkoa  wa Iringa katika  kilele  cha mbio  za mwenge  wa Uhuru kitakachomalizika kitaifa  mkoani Iringa atafanya  uzunduzi wa mkoa  huo wa Njombe katika uwanja wa  saba saba pamoja na kuweka jiwe la msingi katika ofisi ya  Halmashauri ya mji wa  Njombe.

Hata  hivyo alisema  siku inayofuata  ambayo ni Octoba  17  mheshimiwa  Rais  Kikwete  atakuwa wilaya ya Makete  ambapo  shughuli atakazozifanya ni pamoja na kusalimia  wananchi  wa kijiji cha Kipengere ,kuweka jiwe la msingi sekondari ya  Lupalilo,kuweka  jiwe la msingi Zahanati ya  Ivalalila,kuzindua  chuo  cha VETA na baadae  kuwahotubia  wananchi katika mkutano utakaofanyika uwanja wa Iwawa  mjini Makete .

Mkuu  huyo wa mkoa alisema kuwa Octioba 18 Rais Kikwete  atafanya ziara  katika eneo la Lupembe Njombe  kwa  kuzindua  kiwanda  kipya  cha Chai Cha Iganga Tea Company  ,kuweka jiwe la msingi mradi  wa  umeme  wa Mapembasi uliopo Halmashauri ya  mji .

Wakati Octoba 19 atakuwa  wilaya ya  Ludewa  ambako atazindua maabara  ya kisasa katika  Hospital ya  wilaya ya  Ludewa  na baada ya hapo atafanya  mkutano wa hadhara  katika uwanja wa Ludewa mjini .

Katika  ziara  hiyo  wilayani Ludewa Octoba 20  atatembelea  mradi  wa Liganga(Chuma)  katika  kijiji  cha Mndindi  kabla  ya  kuondoka kuelekea  mjini Njombe kwa mapumziko huku Octoba  21 Rais  Kikwete atafanya majumuisho ya  ziara  yake  mkoa mpya  wa Njombe  katika ukumbi wa Halmashauri ya Njombe kabla ya  kuondoka  mkoani hapo.

Hivyo amewataka  wananchi  kujitokeza kwa  wingi katika uzinduzi  wa mkoa  huo pamoja na maeneo ya miradi ambayo Rais Kikwete atapita  mkoani  humo.

Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA