Home » » MWENGE WA UHURU WAZIMWA IRINGA LEO , RAIS KIKWETE AHIMIZA AMANI ,ALIYETAKA KUVAMIA MWENGE ACHEZEA KICHAPO

MWENGE WA UHURU WAZIMWA IRINGA LEO , RAIS KIKWETE AHIMIZA AMANI ,ALIYETAKA KUVAMIA MWENGE ACHEZEA KICHAPO

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Monday, October 14, 2013 | 6:42 AM


 Vijana  wa halaiki   kutoka  shule mbali mbali za Manispaa ya  Iringa  wakionyesha umahili  wao katika kutoa ujumbe wa Mwenge


 Askari  wa FFU  Iringa  wakiwa  wamemkamata  kijana ambae jina lake  bado kufahamika  aliyetaka  kuvamia mwenge  kwa  nia mbaya  wakati wakimbiza  mwenge  wakiwa mbioni kukabidhi mwenga kwa Rais Jakaya  Kikwete uwanja wa Samora Iringa
 Watoto  wa halaiki  wakiwa  wamepumzika
 Rais  Jakaya  Kikwete akiwa amekabidhiwa  rasmi  mwenge wa  Uhuru leo  baada ya  kuhitimisha mbio  zake nchini
 Rais Kikwete  akiwa ameushika mwenge wa Uhuru  leo  uwanja wa  samora  Iringa
 Rais Jakaya  Kikwete  akiwa  katika picha ya pamoja na washindi  wa mbio za mwenge kikanda na jumla  leo
 Rais Jakaya  Kikwete akipokea  mwenge kwa ajili ya  kupiga picha ya  pamoja na washindi wa mbio  hizo kikanda


 Rais  Jakaya  Kikwete akiwa na  viongozi wa  dini  walioshiriki  kumwomba dua baba wa taifa  leo
 Rais Kikwete akisalimiana na askofu wa Roman Katoliki leo

 Wageni mbali mbali wakiwemo mabalozi  wakiwa katika picha ya pamoja na rais Kikwete
 Wabunge pamoja na katibu  mkuu wa CCM  Philip Mangula wa kwanza kushoto  na Spika  wa bunge Anne makinda wa tatu  kulia anayefuata ni mbunge wa jimbo la Iringa mjini Peter Msigwa
 Mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa akimpongeza Rais Jakaya  Kikwete kwa  hotuba yake  nzuri " Mheshimiwa Rais  nimeipenda sana hotuba yako leo"
 Rais Kikwete akiwa na  wabunge wa Chadema Iringa ,mchungaji Peter Msigwa na Chiku Abwao ambao  pia  walishiriki kilele  cha mbio za mwenge
 Rais Kikwete akipongezwa na mbunge Chikua Abwao na mbunge Msigwa kushoto

 Mbunge  Chiku Abwao  akipiga  picha ya Spika makinda  leo uwanja wa samora


 Rais Kikwete katika picha ya pamoja na wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania na spika Makinda  wa tatu  kulia

 Rais Kikwete  katika  picha ya pamoja na wakuu wa  wilaya nchuini

 Mke wa rais Mama  Salima Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na spika Makinda na wakimbiza mwenge Kitaifa  leo
 Wakuu  wa wilaya  Gelard Guninita  na Venance  mwamoto  katika picha ya pamoja na mwananchi  kulia

 Mpiga  picha wa TBC akiwa  juu ya  paa kufuatilia matukio ya   kilele  cha Mwenge  leo
Spika  wa bunge Anne Makinda  akiwa na  waziri wa nchi  ofisi ya  waziri mkuu sera na  uratibu  wa bunge Wiliam Lukuvi
Na matukiodaima.com
RAIS wa Jamhuri ya  muungano  wa Tanzania  Dr Jakaya  Kikwete leo  amezima mwenge  wa Uhuru huku akiwataka  watanzania kuendelea  kudumisha amani ,mshikamano  na utulivu na  kutangaza kiama kwa  wale  ambao watajihusisha na biashara  ya madawa ya  kulevya .

Akiwahotubia  watanzania  katika  kilele  cha  mbio  za mwenge wa Uhuru  kwenye uwanja  wa Samora mjini Iringa ,rais Kikwete  alisema  kuwa  mbio  za  mwenge  wa  uhuru  zimekuwa  zikiendelea  kuwaunganisha  watanzania na  kuendelea kuibua  na kutekeleza  miradi mbali mbali ya  kimaendeleo nchini .

Hata  hivyo  alisema  wapo  baadhi ya  watu ambao  wameendelea  kupinga mwenge  wa  uhuru ambapo kwa upande  wake hawashangai  wanaofanya hivyo kwa ni mtazamo  wao .

" Wakati  leo  umma  wa watanzania  wakiendelea  kuushangilia  mwenge wa uhuru na  hata  kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho haya ila  wapo  baadhi yao ambao hawautakii mema mwenge huu....kama huyu  mmoja ambae leo  amejionyesha hapa ...sasa  sijui  mwenge umemkosea  nini"

Mbali  ya  hilo  pia  Rais  Kikwete  alisema  kuwa  serikali  yake  imejipanga  vema  kuhakikisha  inachukua hatua  sitahiki kwa wale  wote  wanaojihusisha na  biashara  na utumiaji wa  madawa  ya  kulevya .

Kwani  alisema  mbali ya kazi  kubwa  inayofanywa na  serikali  katika mapambano dhidi ya  dawa  za  kulevya ila bado  baadhi ya  watu  wameendelea  kuifanya  kazi hiyo ya  dawa  za  kulevya na  kuwataka  watanzania  kushirikiana na  serikali  katika kuwafichua  wahusika  wa dawa  za kulevya na serikali itawalinda wale  wote wanaotoa  taarifa  za  wahusika wa  dawa za  kulevya.

Aidha Rais  Kikwete  alisema  kuwa pamoja na kuwa  hivi  sasa  Taifa  limekuwa katika utulivu mkubwa  wa amani  ila bado watanzania  wanapaswa  kuendelea  kuenzi amani ambayo baba wa Taifa hayati mwalimu  Julius Nyerere aliiacha na  kupitia  mwenge wa uhuru  watanzania  wamekuwa  wakiendelea  kumuenzi kwa  kuyatenda  yale  ambayo mwenge wa Uhuru  umekuwa  ukiyabeba.

Rais  Kikwete  alisema  kuwa si vema  watanzania  kuendelea  kugawanywa kwa  misingi ya  itikadi, dini, rangi ama  raslimali kwani  iwapo  watanzania  tutakubali  kugawanywa kwa misingi  hiyo tutakuwa tunalipeleka  taifa  pabaya na kila mtanzania anapaswa  kuendelea  kuenzi amani iliyopo na kuchukia mgawanyiko wa aina  yeyote.

Akielezea  kuhusu janga  la  ukimwi alisema  kuwa   bado  tatizo hilo la UKIMWI  limeendelea  kuwa kubwa  katika mkoa  wa Njombe ambao  unaongoza kwa maambukizi ukifuatiwa na  mkoa wa Iringa ambao unashika nafasi ya pili kitaifa kwa UKIMWI  hivyo  kuwataka  wananchi wa mikoa  hiyo kuendelea  kuchukua hatua  ya  kupunguza kasi ya maambukizi ya VVU na  kuendelea  kutumia dawa ya  kupumbaza virusi vya  UKIMWI inayotolewa na  serikali na  wale ambao hawajaathirika kujilinda wasiathirike .

Katika  hatua  nyingine  Rais  Kikwete  amewataka  watanzania  kujiandaa   kusherekea   mapinduzi ya  miaka 50 ya Zanzibar ,kukamilika kwa katiba  mpya ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania  shughuli ambazo zitafanyika mwakani.

Wakati  huo  huo sherehe  hizo  za kilele cha mbio  za mwenge wa Uhuru nusuru ziingie  doa baada ya  kijana  mmoja ambae  jina lake  halikuweza  kupatikana mara  moja  kuwavamia  wakimbiza  mwenge kitaifa  na  kutaka  kukonya mwenge  huo  kabla ya  kukamatwa na  kupokea  kipigo  kikali mbele ya Rais Kikwete  toka kwa askari wa FFU.

Tukio la kijana  huyo kutaka  kupokonya  mwenge  huo  lilitokea  dakika chache  baada ya  waziri wa habari ,vijana ,utamaduni na michezo Dr Fenella Mkangala  kumwomba Rais Kikwete  kushuka jukwaa kuu na kusongea  eneo maalum la kukabidhiwa  mwenge  kutoka kwa  wakimbiza  mwenge  hao.

Wakati wakimbiza mwenge hao  wakisogea   huku  wakiwa karibu kumfikia  Rais Kikwrte kama   hatua 10 hivi  kijana  huyo  alichomoko kutoka  upande  ambao  wanahabari  walikuwa  wamesimama na  kuwafuata kwa mbele  wakimbiza mwenge hao na kutaka  kuupokonya  mwenge huo .

Hata  hivyo kabla ya  kuugusa  mwenge  huo  mmoja kati  ya  vijana  wakimbiza  mwenge   kitaifa   kutoka mkoa  wa Iringa alimdaka  kijana  huo na  kumnyanyua  juu juu kabla ya  askari wa FFU waliokuwepo  eneo hilo sanjari na mwenge  kumkamata na kumpa kichapo na  kumpakia katika gari la polisi na kumpeleka  polisi.

MWISHO
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA