Home » » MATUKIO NA HABARI KUTOKA MKOA WA LINDI LEO

MATUKIO NA HABARI KUTOKA MKOA WA LINDI LEO

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, October 1, 2013 | 12:51 AM


Bodaboda watakiwa kuiyunga mkono
Na  Ali  badi  MASASI ....    

SERIKALI imesema kuwa makundi ya vijana wanaojishughulisha na shughuli za bodaboda nchini wanatakiwa kukithamini na kukiunga mkono kwa vitendo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa vile ndicho Chama pekee kilichopo madarakani na kwamba kinauwezo wa kuwakomboa kiuchumi.
 
Hayo  yalielezwa  jana wilayani hapa na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia January Makamba wakati alipokuwa akizungumza na madereva wa bodaboda wilaya ya Masasi Mkoa wa Mtwara katika ziara yake aliyoifanya wilayani humo.
 
Alisema kuwa vijana hasa wanaofanya kazi ya bodaboda wanapaswa kutambua kuwa CCM ndio Chama kilichopo madarakani kwa sasa hivyo kinayo fursa kubwa ya kutekeleza mambo mbalimbali ya maendeleo kwao ikiwemo kuwatafutia fursa za kujikwamua kiuchumi kwa makundi ya vijana na kuwapunguzia gharama za kodi zinazowakabili na kukwamisha jitihada zao za kujiletea maendeleo.
 
Makamba alisema kuanzia sasa vijana hasa wanaofanya kazi ya bodaboda wanakila sababu ya kukithamini na kukiunga mkono kwa nguvu zote Chama Cha Mapinduzi ili kiweze kuwakomboa kimaendeleo badala ya kushabikia Vyama vya upinzani ambavyo havina dira wala mwelekeo wa kuleta maendeleo.
 
 Alisema vijana hasa makubdi ya bodaboda waepuke kushawishiwa na viongozi wa Vyama vya siasa vya upinzani katika kufanya maandamano na vurugu ambazo zinalenga kurudisha vyuma juhudi mbalimbali za maendeleo zinazofanywa na serikali ya CCM ambapo mwisho wa siku vijana hao hubakia bila kazi yeyote ya kujiingizia kipato na kukabiliwa na ugumu wa maisha.
 
“Vyama vya upinzani havina uwezo wa kutekeleza shughuli za maendeleo kwa wananchi kama kinavyotekeleza Chama Cha Mapinduzi kupitia serikali yake iliyopo madarakani hii inatokana na Vyama hivyi vya upinzani kutokuwa madarakani na kwamba Chama Chama Mapinduzi kwa kutambua umuhimu uwepo wa vijana hawa kitahakikisha kinawakomboa kiuchumi kwa kutatua changamoto zinazowakabili,”alisema Makamba
 
Aidha Naibu Waziri huyo alitumia fursa hiyo kuwapongeza madereva hao wa bodaboda wilayani Masasi kwa kuanzisha Saccos ya umoja wa madereva wa bodaboda na kwamba hatua hiyo itawasaidia kuweza kujikwamua kiuchumi kwa urahisi zaidi ambapo serikali pia itakuwa bega kwa bega katika kusaidia kuiendeleza Saccos hiyo aidha Makamba ameahidi kutoa pikipiki mbili kwenye umoja huo wa bodaboda
 
Akisoma risala kwa niaba ya wanachama wa umoja wa madereva wa bodaboda wilayani Masasi mbele ya Waziri huyo mwenyekiti wa umoja wa huo Idi Mohamedi alisema umoja huo unajumla ya wanachama 45 na kwamba unakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kutowepo kwa mikataba baina yao na waajili wao kutozwa kodi nyingi na serikali pia kunyang’anywa vyombo hivyo na majambazi wakati wakiwa kazini.
Mwisho.

Mbunge viti maalumu atoa msaada wa shuka
Na Ali  badi MASASI ...

JUMLA ya shuka 190 zimetolewa msaada katika Hospitali ya Halmashauri ya mji wa Masasi Mkoani Mtwara ikiwemo na vituo vya afya vitatu vilivyopo katika Halmashauri ya wilaya lengo likiwa ni kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya afya nchini.
 
Msaada huo umetolewa jana na Mbunge wa viti maalumu kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mtwara, Agnes Hokororo ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi
 
Alisema kuwa yeye kwa kushirikiana na mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) mikoa ya Lindi na Mtwara wametoa msaada huo baada ya kuguswa na changamoto zilizopo kwenye sekta ya afya wilayani Masasi na kwamba hatua hiyo itasaidia kupunguza changamoto hizo ikiwemo ukosefu wa shuka katika vituo vya afya na zingine ambapo kwa ujumla zinakwamisha utoaji wa huduma kwa wananchi.
 
Alisema sekta afya ni miongoni mwa sekta ambazo zinakabiliwa na changamoto nyingi katika kutoa huduma zake kwa wananchi hivyo serikali kwa kushrikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo wameendelea kushikamana kwa pamoja katika kupunguza baadhi ya changamoto ili kuhakikisha huduma ya afya inatolewa kikamilifu kwa wananchi.
 
“Msaada huu wa shuka utasaidia wananchi wa maeneo husika wanaopatiwa huduma wakati wakiwa wamelazwa na kwamba mimi kwa nafasi yangu licha ya kutoa msaada huu bado nitaendelea kuwashawishi wadau ili tuweze kutatua changamoto zilizopo kwenye sekta ya afya na sekta zingine ili kuleta maendeleo kwa wananchi wa Mtwara,”alisema Mbunge huyo
 
Akipokea msaada huo wa shuka 70 mganga mkuu wa Hospitali ya Halmashauri ya mji wa Masasi,Dkt Harry Mwambe alimshukuru Mbunge huyo kwa kuweza kuipatia Hospitali yake shuka hizo na kwamba awali kulikuwa na tatizo la ukosefu wa shuka hasa katika wodi ya kinamama,vituo vya afya ambavyo pia vimepata msaada huo ni Nagaga 35,Lupaso 50 na Chiwale 35
 
Nae meneja wa mfuko wa taifa wa bima ya afya mkoa wa Mtwara, Joyce Sumbwe alisema kuwa mfuko huo utaendelea kushirikiana na serikali katika kuhakikisha kuwa huduma za afya na changamoto zake zinakwisha na wananchi wanapatiwa huduma zilizobora mijini na vijijini na pia kuahamisha wananchi kuchangia baadhi ya huduma za afya ikiwemo kujiunga na mfuko wa afya ya jamii CHF
Mwisho.Wananchi walia kunyanyswa


Na Ali  Badi MASASI 

wananchi
wa kijiji cha Mailisita wilayani Masasi mkoa wa Mtwara wamelalamikia vitendo vya unyanyasaji wanavyofanyiwa ikiwemo kunyang’anywa begi zao na baadhi ya makondakta wa daladala zitokazo Masasi mjini kwenda hadi kijiji cha Ndanda wilayani humo na kuutaka uongozi wa serikali ngazi ya wilaya kuingilia kati suala hilo.
 
Wakizungumza jana mbele ya mkuu wa wilaya hiyo, Farida Mgomi mara baada ya kumalizika mkutano wa kuhamasisha kilimo bora cha zao la korosho uliyofanyika kijijini hapo wanakijiji hao walisema kuwa makondakta hao wamekuwa wakiwatoza viwango vya juu vya nauli tofauti na viwango halisi wanavyotakiwa kulipa.
 
Walisema makondokta hao wamekuwa wakiwatoza nauli ya Sh.1000 kwa umbali wa mailisita badala ya viwango vya kawaida vya Sh.500 ambavyo hata mamlaka ya Udhibiti Usafiri Nchi kavu na majini (SUMATRA) wameviweka na kuvitambua na kwamba wao wanapo hoji juu ya nauli hiyo ya Sh. 1000  hunyang’anywa  begi zao pamoja na mali zingine.
 
Wakizungumza kwa niaba ya wanakijiji wenzao juu tatizo hilo,Banaba Suwedi,Shabani Mohamedi na Vicent George wameimba serikali wilayani humo kuingilia kati tatizo hilo ambapo kwa sasa wananchi wamekuwa wakipoteza mali zao ambazo wamekuwa wakipolwa na makondokta hao kwa madai kuwa wananchi hao kupinga kulipa nauli ya Sh.1000 kwenye daladala hizo.
 
Walisema wao nauli ambayo wanaitambua siku zote wanaposafiri kutoka kijijini hapo hadi mjini Masasi ni Sh. 500 na siyo Sh. 1000 kama wanavyotozwaa na makondakta  wa daladala hizo na kwamba siku zote wanaposafiri kwenye mabasi ya kawaida yaendayo Lindi na Mtwara wamekuwa wakitozwa viwango vya  Sh.500 na siyo Sh.1000 hivyo wameiomba serikali kumaliza mvutano huo.
 
“Tunaiomba serikali kuiingilia kati suala hili kwakweli hawa makondakta vitendo wanavyotufanyia kwenye daladala zao ni unyanyasaji sasa kabla na sisi hatujachukua sheria mkokoni tunaomba hawa makondakta wapewe elimu juu hili vinginevyo hali inaweza kuwa mbaya hapa,”alisema kijana mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Issa Stepheven
 
Nae mkazi mwingine Mohamedi Bakari alisema kitendo cha makondakta hao kutoa lugha chafu na kupola begi zao kwa wanakijiji wanaosafiri kwenye daladala zao si cha busara na kwamba wanapaswa kutambua viwango hali vya nauli kuendana na viwango vinavyotambulika kisheria.
 
Aidha wananchi hao wameiomba mamlaka ya Udhibiti usafiri wa vyombo vya abiria Nchi kavu na majini (SUMATRA) kuwataka wamiliki wa vyombo hivyo vya abiria kubandika karatasi inayoonyesha viwango vya nauli kwenye vyombo vyao ili kila abiria kabla ya kupanda chombo hicho aweze kuona hatua hiyo itapunguza migogoro inayojitokeza. 
 
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Masasi ameahidi kulifuatilia suala hilo na kuwataka wananchi hao kuwa watulivu kwa kipindi hicho ili kupata ufumbuzi utakaosaidia kulitatua tatizo hilo na kuresha hali ya amani baina ya makondakta hao na wananchi.

.........................................................................................................................

TANGAZO !TANGAZO ! SHAMBA HEKARI 10 LINAUZWA KILOLO KWA KIASI CHA TSH MILIONI 3.5

Shamba  linauzwa ni  zuri  kwa  kupanda miti ya  aina mbali mbali ya  mbao  ni nguzo  za  umeme pia  chai  inakubali na  mazao ya chakula  .

sifa  la  shamba  hili lina ukubwa wa hekari 10 sehemu ya shamba  tayari  limepandwa miti  ya mbao na  karatasi  miti aini ya paina 

Shamba  lipo  kijiji cha Lusinga wilaya  ya Kilolo mkoani Iringa linauzwa k uanzia Tsh milioni 3.5 maelewano yapo  tupigie  simu 0754 026 299/0712750199
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA