Home » » KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU AWASHUKIA WAPINZANI WA MWENGE

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU AWASHUKIA WAPINZANI WA MWENGE

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Friday, October 11, 2013 | 11:45 AM
 Mkuu  wa  wilaya ya  Iringa Dr  Leticia  Warioba  akiwa ameshika mwenge wa uhuru  baada ya  kupokea kutoka kwa mkuu wa wilaya ya  Mufindi Evarista Kalalu (kushoto) leo  wakati wa makabidhiano ya mwenge  Uhuru kati ya Mufindi na Iringa eneo la Muwimbi
 Chipukizi  wa  wilaya  Halmashauri ya  Iringa  wakitoa ujumbe wa mwenge mbele ya kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru Kitaifa  leo
 Wabunge  wa  viti maalum mkoa  wa Iringa  kupitia  CCM Ritta kabati  kushoto na Lediana Mafulu  katikati  wakiwa katika  picha ya pamoja na mkurugenzi  wa Halmashauri  ya wilaya ya  Iringa
 washereheshaji  wa  Halmashauri  ya  Iringa KIONGOZI  wa  mbio  za mwenge  Kitaifa Juma Alli Simai  amewataka  viongozi  wa  vyama  vya  siasa   kujenga  utamaduni  wa kuheshimu uzalendo na kuacha  kutumia majukwaa ya  siasa na  vyombo vya habari kupinga mwenge  wa Uhuru.

Akizungumza  na  wananchi wa Kalenga  wilaya ya  Iringa  vijijini  leo kiongozi huyo alisema kuwa   mwenge  wa  Uhuru ambao  uliasisiwa na baba  wa Taifa  hayati  mwalimu  Julius Nyerere ulilenga  kuwaunganisha  watanzania  kuwa  kitu kimoja na kuendelea  kujenga mshikamano ,upendo na umoja  wa kweli kwa watanzania.

Hivyo  alisema  kuwa  ni  vema  serikali  kuendelea  kuwachukulia hatua  viongozi  wa  vyama  vya siasa ambavyo  vinaendelea  kupandikiza  chuki miongoni mwa  watanzania kama mtaji  kwao  wa kisiasa.

“Ifahamike  kuwa  jitihada  kubwa  zilizofanywa na baba  wa Taifa  na  waasisi wengine wa taifa  hili katika  kupigania  uhuru ndio  sababu ya  leo Tanzania  tunaendelea  kufurahia amani na utulivu mkubwa  uliopo ambao  umetokana na jitijhada  kubwa za baba  wa Taifa…..hivyo kila  mtanzania anapaswa  kuendelea  kumuenzi baba  wa Tkaifa kwa  kushiriki mbio  za mwenge wa Uhuru”
Katika  hatua  nyingine  kiongozi  huyo aliwataka  viongozi  wa umma katika  wilaya  zote nchini  kuendeleza  ushirikiano baina yao  na  wananchi  kama njia ya  kudumisha  utawala  bora.

Bw  Simai alisema  kuwa  mbio  za  mwenge wa Uhuru mbali ya  kupita kila  wilaya ila umekuwa ukipita  baadjhi ya maeneo   japo  ujumbe  wa mbio za mwenge  ambao umekuwa  ukibeba  umekuwa ukiwalenga  watanzania  wote  hivyo hata  wale  ambao hawajafikiwa na mbio  hizo za mwenge  pia kufanya  jitihada za  kuwafikishia  huko  waliko.

Akizungumzia  kuhusu  miradi 11 iliyopitiwa kwa  kuwekewa  mawe ya msingi na baadhi  kufunguliwa alisema  kuwa miradi  hiyo katika Halmashauri ya  Iringa ni miradi  iliyojengwa kwa  kiwango  cha hali ya  juu na kupongeza  mkurugenzi  wa Halmashauri  ya Iringa na  wataalam wake kwa usimamizi mzuri  wa miradi ya maendeleo.

Alisema  kuwa  ubora  wa miradi ambayo mwenge wa Uhuru  2013  umepata  kupitia katika  Halmashauri ya  Iringa ni miradi ya kuigwa na Halmashauri nyingine  hapa nchini.

Katika  hatua  nyingine kiongozi  huyo  aliwataka wananchi  kuendelea  kuchukua  tahadhari  dhidi ya UKIMWI pamoja na dawa  za  kulevya kwa  kuepuka  vitendo  vinavyo changia maambukizi mapya ya  UKIMWI  huku kuhusu  dawa  za kulevya na  rushwa akiwataka  wananchi  kuwafichua  wahusika  wa dawa za  kulevya na rushwa  ili  waweze  kuwajibishwa  kisheria.

Kwa  upande  wake  mkuu  wa wilaya ya  Iringa Dr  Leticia Warioba  akitoa  taarifa  ya  miradi hiyo kwa kiongozi  huyo alisema  kuwa  katika Halmashauri ya  Iringa miradi 11 yenye  thamani  ya zaidi ya Tsh bilioni 1.7 imepitiwa na mbio  za mwenge mwaka huu.

Aliitaja  miradi  hiyo kuwa ni  pamoja na ujenzi  wa  kituo  cha polisi Ifunda,,kitalu  cha  miti Ifunda,bwawa la  kuvuna maji  ya  mvua,ukarabati  wa barabara na miradi mingine  ya shule ,maabara na vicoba

Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA