Home » » BREAKING NEWSssss WAOMBOLEZAJI WAPATA AJALI MBAYA MCHANA HUU HUKO NYORORO MUFINDI

BREAKING NEWSssss WAOMBOLEZAJI WAPATA AJALI MBAYA MCHANA HUU HUKO NYORORO MUFINDI

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, October 29, 2013 | 6:00 AM


Habari  za  uhakika  ambazo mtandao  huu  wa www.matukiodaima.com  umezipata  kutoka  Nyororo  wilayani Mufindi  zinadai  kuwa  watu  zaidi ya 3   wamejeruhiwa  vibaya   baada ya  gari  walilokuwa  wamepanda  kwenda  msibani  kupinduka  .

Akizungumza na mtandao  huu  ndugu  wa msiba  huo Bw  Saugo Ndemo  amesema  kuwa ajali hiyo imetokea mchana  huu na hadi sasa  jitihada za  kuokoa  majeruhi  zinaendelea japo  hakuna  aliyepoteza maisha  eneo la ajali

Ndemo  alisema  kuwa ajali  hiyo  imetokea  mita  300 hivi kutoka  mjini Nyoyoro na  kuwa waombolezaji  hao  walikuwa  wakienda  kumzika ndugu yake aliyemtaja kwa  jina la
Katalina  Ng'oumbi aliyefariki  dunia  jana.

habari  kamili na picha  zitakujia  baada ya  kikosi cha  matukio daima .com  kwenda eneo la  tukio
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA