Home » » BREAKING NEWSS....MFANYABIASHARA NA DIWANI WA KATA YA NJOMBE MJINI LUPYANA FUTE[Jacky's]AMEFARIKI DUNIA GHAFLA

BREAKING NEWSS....MFANYABIASHARA NA DIWANI WA KATA YA NJOMBE MJINI LUPYANA FUTE[Jacky's]AMEFARIKI DUNIA GHAFLA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Sunday, October 20, 2013 | 2:08 AM

.    
 Marehemu Lupyana Fute[Jacky's] Kushoto akisalimia na Waziri Mkuu Mizengo Pinda Wakati wa Harusi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Mzee Philip Mangula Iliyofanyika Mjini Njombe (picha na Maktaba)
Lupyana Fute enzi  za uhai wake akizungumza Kwenye Moja ya Vikao vya Baraza la Madiwani Enzi za Uhai Wake.

Na Mwandishi Wetu.

Diwani wa Kata ya Njombe Mji Lupyana Fute Ambaye Pia Alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa NEC Wilaya ya Njombe Amefariki dunia Ghafla Jioni ya jana mjini Njombe .

Taarifa za Awali toka Kwa Mashuhuda wa Tukio Hilo Akiwemo Solanus Mhagama Amesema Kuwa Kwa Mara ya Mwisho Marehemu Lupyana Fute Alimpigia Simu na Kumwambia Amtafutia Gari la Kikosi cha Zima Moto na Uokoaji Baada ya Moto Kuzuka Kwenye Chumba cha Jengo la Ofisi yake Iliyopo Karibu na Tumaini Dispensari.


Bwana Mhagama Amesema Kuwa Mara Baada ya Kufika Kwa Gari Hilo na Kufanikiwa Kuzima Moto Kwa Kushirikiana na Wananchi Uliokuwa Ukiwaka Kwenye Chumba Cha Kuhifadhia Vitu[STOO] ndipo Marehemu Alipoingia Ofisini Kwake Alikopotezea Fahamu.

Aidha Amesema Kuwa Walipoingia Ndani ya Chumba Ofisini Kwake Walimkuta Marehemu Fute Akiwa Amepoteza Fahamu Huku Akiwa Ameketi Kwenye Kiti Chake Ndipo walipomchukua na Kumwahisha Katika Hospitali ya Kibena.Mara Baada ya Kufika Katika Hospitali Ya Mji Njombe Kibena Ndiko Waliko ambiwa Ameshafariki.

Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Bwana Edwin Mwanzinga Amesema ni Kweli Diwani Huyo Amefariki Dunia Hivyo Taarifa Zaidi Zitaendelea Kutolewa.


Taarifa Zaidi Juu ya Msiba Huo Utaendelea Kujulishwa Kupitia Mtandao Huu Endelea Kufuatilia.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA