Home » » BODI YA HUDUMA YA AFYA YA HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA YAVUNJWA RASMI

BODI YA HUDUMA YA AFYA YA HALMASHAURI YA MANISPAA YA IRINGA YAVUNJWA RASMI

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, October 1, 2013 | 12:43 AM


katibu wa  sekretarieti  ya afya Dr May Alexandera akieleza mafanikio  yaliyofikiwa
Mstahiki wa meya  wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa Amani Mwamwindi katikati akiwa na naibu wake Gervas Ndaki na mkurugenzi  wa Halmashauri ya Manispaa yaIringa Terresia Mahongo wakati  bodi  hiyo ilipokuwa ikivunjwa
katibu wa  sekretarieti  ya afya Dr May Alexander kulia  akipongezwa  na  diwani wa kata ya Mtwivila Bw  Vitus Mushi
Wajumbe  wa bodi   ya  huduma ya  afya  ya  Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa  na kamati  za usimamizi wa  vituo  katika Halmashauri  wakiwa katika  picha ya pamoja na viongozi  mbali mbali  wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa kutoka  kushoto wa kwanza ni naibu  meya  Bw Gervas Ndaki, mstahiki meya  wa Manispaa ya  Iringa Bw Aman Mwamwindi, diwani wa kata ya Ruaha  Bw Alfonce Mlagala na mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa Bi Terresia Mahongo 

BODI  ya  huduma ya  afya  ya  Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa  na kamati  za usimamizi wa  vituo  katika Halmashauri  hiyo  mkoani Iringa  imeeleza  changamoto  mbali mbali na mafanikio  yaliyofikiwa  katika  utekelezaji  wa  shughuli  zake .

Katika  taarifa  yake  iliyotolewa  jana mbele ya  wajumbe  wa bodi  hiyo  katika  ukumbi wa Halmashauri ya Manispaaa ya  Iringa na katibu wa  sekretarieti  ya afya Dr may Alexander ambae  ni mganga  mkuu  wa  afya Manispaa ya  Iringa baada ya bodi hiyo kumaliza muda  wake  ,ilisema  kuwa bodi  hiyo ilianza  kazi  mwezi  julai 2010 chini ya  mwenyekiti  wake Dr Omari Lushino  ambae  ni mjumbe  anayewakilisha huduma  za  afya  binafsi  kwa  faida .

Alisema  kuwa  katika  kipindi  cha miaka mitatu  bodi   hiyo ilifanikiwa  kutekeleza mambo mbali mbali  ikiwa  ni pamoja na kusimamia ufunguzi  wa  zahanati ya Kitwiru na Njiapanda mwaka  2010, pia kusimamia ujenzi  wa nyumba ya mtumishi katika  Zahanati  ya Njiapanda ,ujenzi  wa  wodi  ya wanawake  na wanaume katika Zahanati  ya Itamba mwaka 2010

Ujenzi  huo  una lengo la kuipandisha  hadhi  Zahanati  hiyo  kuwa  kituo cha afya  kupita mpango  wa  maendeleo ya afya ya msingi (MMAM) ambapo  hadi  sasa  jengo  hilo katika  hatua  ya  ukamilishaji .

katibu  huyo  alitaja  mafanikio  mengine  kuwa ni  kusimamia ukamilishaji  wa  nyumba  ya  mtumishi  katika Zahanati ya Nduli ,ujenzi  wa uzio  katika  kituo cha  afya Ipogolo,kampeni ya huduma ya tohara  kwa wanaume  katika kituo cha  Ngome kuanzia  mwaka  2011,kampeni  za umezaji  wa  dawa  za  kuthibiti magonjwa yasiyopewa kipaumbele (NTDS) katika ngazi  ya jamii  tangu mwaka  2010 pamoja na kufanikisha  kufungua  Hospital ya  wilaya   iliyopo Frelimo na ujenzi  wa Hospital  hiyo

Kuhusu  uanzishaji  wa mfuko  wa afya ya  jamii -mjini  alisema  kuwa bodi yake imefanikiwa kwa  kiasi kikubwa kuanzisha  mfuko huo unaotumia mkakati  wa tiba kwa kadi (TIKA) ambao  ulianza  mwezi machi  2013.

Aidha  alitaja  changamoto  mbali mbali kuwa ni pamoja na  bodi hiyo  kutokuwepo kwa mafunzo  ya  kuwajengea  uwezo wajumbe wa vyombo hivyo na ukosefu  na ucheleweshaji wa fedha   kwa ajili ya ukamilishaji wa  miradi ya maendeleo.

Bodi   za huduma ya afya  za Halmashauri na kamati  za afya za vituo vya  huduma ,chimbuko  la dhana  ya  kuwa na bodi lilitokana na azimio  la alma Ata la mwaka 1978 amblo lilianzisha mpango  wa huduma ya afya ya msingi ( Primary Health care).
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA