Home » » WATUHUMIWA WA UPIGAJI NONDO WIZI MAFINGA WANUSURIKA KUUWAWA KWA KICHAPO

WATUHUMIWA WA UPIGAJI NONDO WIZI MAFINGA WANUSURIKA KUUWAWA KWA KICHAPO

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Friday, September 27, 2013 | 8:37 AM

 
 
Mmoja  kati ya  watuhumiwa wa wizi Mafinga  wilaya ya Mufindi  akiwa  amechezea kichapo toka kwa  wananchi wenye hasira  kali  leo
Askari  polisi  wakisaidia  kuokoa maisha na  watuhumiwa wa upigaji nondo Mafinga 

 
Watuhumiwa hao  wakiwa  kituo cha  polisi  baada ya  kuokolewa  kutoka mikononi mwa  wananchi wenye hasira kali  leo

Watu watatu wamenusurika kufa baada ya kipigo kikali kutoka kwa wananchi wenye hasira baada ya kugundulika kuwa ni vibaka ambao hupiga nondo na pengine kuwachoma visu raia/wananchi warudipo majumbani mwao nyakati za usiku.

           Watu hao walikamatwa juzi hapa Mafinga na watu wa stand kuu ya mabasi, na msako wa kuwakamata vibaka hao ulikuwa ni wa kundi kubwa kutoka standi na kuwafuata kinyanambo sehemu za vilabu vya pombe za kienyeji ambapo mara ya kwanza walipoenda walimkuta mmoja na kumpeleka kituo kidogo cha polisi kilichopo maeneo hayo ya standi kuu, alipobanwa aoneshe wezake akataja maeneo ambayo huwa wanashinda na alipoelekeza tu hilo eneo jopu nzima la watu wa standi wakarudi tena huko Kinyanambo na kuwabamba vibaka wawili tena.

          Hivyo vibaka hao hadi leo hii bado wameshikiliwa mikononi mwa polisi kwa uchunguzi zaidi. 
                                                                                                               Picha na Rogers Mselu mdau  wa www.matukiodaima.com Mafinga
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA