Home » » VYUO VISIVYO NA SIFA VILIVYOPEWA USAJILI IRINGA , VETA MNAFANYA HIVYO KWA MASLAHI YA NANI? HII SEHEMU YA PILI

VYUO VISIVYO NA SIFA VILIVYOPEWA USAJILI IRINGA , VETA MNAFANYA HIVYO KWA MASLAHI YA NANI? HII SEHEMU YA PILI

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Sunday, September 29, 2013 | 1:44 AM


KAMA  ilivyo ada  elimu  bora  hutolewa katika mazingira  bora  yenye kiwango  kizuri  kisicho na  kasoro ila  iwapo  eneo la utoaji  huduma  likawa katika  hali  ya ubabaishaji  ni  wazi   huduma  itakayotolewa  pia ni ya kibabaishaji.

Awali  ya  yote  nitumie  nafasi  hii adimu kuwapongeza  wazalendo  wote  walioamua  kuwekeza katika  elimu  hasa  ya  vyuo vya  Hotel na utalii  mkoani  Iringa amani mnapaswa  kupongezwa  kwa kuendeleza  jitihada za  serikali katika ukuzaji wa utalii katika  mikoa  ya nyanda za  juu  kusini nasema  hongereni  sana.

Mbali ya pongezi  hizo kwa  wale  walioamua  kuanzisha  vyuo ila  bado  nitaendelea  kuweka  ukweli  hapa  juu ya vyuo  tunavyovitaka kwa ajili ya utoaji  wa  elimu  bora  hasa  tukizingatia kuwa  walendwa  wa  vyuo  hivyo ni  watoto  wetu ambao  wamevutiwa  kuingia katika tasnia  ya Hotel  na utalii hivyo  mategemeo yao ni  kuja  kupata elimu  bora  itakayomuwezesha  kupata  ajira  tena  si ajira  inayotokana na mkuu  wa  chuo ama mwalimu  kuhonga kwa mmiliki wa  Hotel ama afisa  husika  ili mwanafunzi  wako apate nafasi ya kazi hapa tutakuwa  tunajidanganya na  kuwatumia watoto  wetu kama  kitega  uchumi na huo ni ufisadi mbaya unaopaswa  kukemewa.

Ni matumaini  vyuo  hivi viendeshwe kwa  misingi na taratibu za VETA kama  wasimamizi  wakuu  wa  vyuo  hivyo  na mamlaka  zote  zinazohusika na si vinginevyo.

Kama  hivyo  ndivyo hebu  tujiulize  sasa  katika  mkoa  wa Iringa  pekee  una  vyuo  zaidi ya 6 vinavyojitangaza  eti  kuwa  ni vyuo  vya Hotel na  utalii ambavyo vimeendelea  kutafuna fedha  za watoto  wa  waokota  matunda ( masikini) lakini  vyuo  vilivyo vingi kwa mujibu  wa uchunguzi  wa mtandao  huu  wa www.matukiodaima.com na www.francisgodwin.blogspot.com ni  vyuo  feki ambavyo vimeshindwa  kabisa  kukaribia  sifa  za kuitwa  chuo na  kupewa barua  ya  kuruhusiwa kuendeshwa ama  usajili ila kila   chuo  ukiuliza eti  unaambiwa kina usajili wa  VETA hii ni aibu kubwa .

Cha  kushangaza vyuo  ambavyo  sifa  zake zinaendana na zile zinazohitajika  na VETA kama  wasimamizi  wakuu  wa  vyuo  hivyo ndivyo VETA kanda ya  nyanda za juu  chini ya  mkurugenzi  wake mama angu Monica  Mbele ndivyo vinavyotangazwa  katika  vyombo  vya  habari  kuwa havina  sifa .

Sina shaka na  uamuzi  wa mkurugenzi  wa kanda wa VETA Bi Monica  Mbele wa  kuvitangaza  vyuo  hivi kama ni  feki  kutokana na  kutotimiza sifa kama yeye anavyosema  ila  ni  wasiwasi na utendaji kazi wake ama  wasaidizi  wake ambao binafsi sina hakika kama maamuzi yao wamekuwa  wakiyafanyia  kazi kwa maana ya  kutembelea  chuo  kimoja  hadi cha mwisho na kuangalia ni  kipi chenye sifa  ya  kuitwa  chuo na kipi  kinapaswa kuitwa  kijiwe  cha wahuni   wachache kuwaibia  watanzania  kwa kupokea  ada  za kutoa  elimu  wakati si  sehemu ya kutolea  elimu hiyo  ya  chuo cha Hotel na utalii.

Ushauri  katika  hili Bi Monica Mbele unapaswa kujisahahisha  kama ni wewe  mwenyewe  umetenda haya  ya  kuvifunga  baadhi ya  vyuo  vyenye sifa na kuziacha  vyuo hivi ila kama ni  wasaidizi  wako  walikuletea  ripoti  hii ya  vyuo nikueleze  wazi kuwa  hao  wasaidizi hawakutakii mema na  waogope kama  ukoma  kwani wanataka  kukuchafulia sifa  yako  kubwa ambayo binafsi bila kushurutishwa huwa  naamini kama ni mmoja kati ya wanawake  wa  chuma katika  kazi .

Ila  pia kwa  upande  wako kabla ya kuvifunga  vyuo  hivyo ni vema ungejiridhisha  kuliko ilivyo  sasa kila  mmoja kwa  wamiliki hawa wa  vyuo anakuchukia wewe  kuwa umefanya  upendeleo katika   hili .

Japo  si mtendaji  wa  VETA  ila kidogo nina  uelewa  juu ya sifa  za  kuitwa chuo cha Hotel na Utalii sifa ambazo mmiliki anapaswa kuzifuata  na  hizi ndizo sifa  nilizopata  kuzitumia katika  uchunguzi  wangu katika  vyuo  hivyo na  leo  kuona ni  wazi kuna  makosa katika  kuvitambua   vyuo  hivi kuwa ni bora  na kushindwa  kuvitambua  hivi  bora  kuwa si bora.

1. darasa  kubwa
2.viti  na meza  za  kutosha 
3.Pratical rooms
4.jiko
5.Restaurant
6.bar
7.Standard ya  walimu (CV)
8. Vitabu vya  kufundishia
N.K
Hizi ndizo sifa  nilizopata  kuzitumia  katikakufanya  utafiti  wangu sifa  ambazo kwa  haraka haraka hata  leo  tukiondoka mimi na jopo la wanauchunguzi  wengine  nje ya VETA Iringa kuvizungikia  vyuo  hivi ambavyo  bila  woga  naviita ni  vyuo  feki ambavyo wao  wamevipasisha  kuwa ni vyuo  vyenye  sifa  ukweli hakuna  kinachokaribika mfano upande wa CV za walimu, ukubwa wa darasa , Pratical room  na  sifa  nyingine nyingi ni vituko ni kama vyuo  vinavyoigiza katika elimu.

Kwa  leo nitavitaja  vyuo  viwili vya awali ambavyo nitaomba  uchunguzi  wa timu  ya VETA  Taifa  kama  utafika  kuanzia kwa  uchunguzi kama  kweli  vilipaswa  kutangazwa  kuwa ni vyuo  visivyo na sifa vyuo  hivyo ni Ruaha na  Delima hebu leo VETA tuweke  chini tofauti  zetu na wamiliki wa vyuo  hivyo na tutende haki katika kugawa  sifa  za macho ama  zile za VETA kama  kweli vyuo  hivi ni feki ama   wale  waliotumwa  kuvitazama  vyuo  hivyo walirejesha majibu feki ?hapana  siwafundishi kazi ila katika ukweli tusemezane  kweli  tupu na asiwepo  wa  kutoa  vitisho  wala  kuchukia kwa  kuelezwa  ukweli ila narudia  tena  sina  shaka na uelewa wa  watendaji kazi wa VETA lakini katika  hili mnasafiri katika mtumbwi wa mhongo mnaruhusu mmoja  wenu  kuendelea  kuutafuna mtumbwi huo kabla ya kuvuka bahari .

Sasa nasema  sitaki  kuona VETA mkifanya  kazi  kwa kujuana  na kuacha  kutenda  ukweli na sitaki  kuona wala  kusikia mtu akilalamika  kwa mtazamo  wangu huu .

Usikose  jumapili  ijayo  katika   mwendelezo wa  sehemu ya  tatu  ya uchunguzi  huu  wa vyuo  visivyo na sifa  kupewa usajili na vilivyo na  sifa  kunyimwa usajili Iringa na tutavitaja vyuo visivyo na  sifa  ambavyo  vimepewa usajili.
....................................................................................................................................
TANGAZO ! TANGAZO! SHAMBA HEKA 20 IRINGA LINAUZWA  TSH MILIONI 12
Shamba  hili heka 20  lililozungushiwa  miti ya  nguzo za  umeme na ndani ya  miaka miwili  unaweza  vuna mbao linauzwa  pia  shamba  hili linafaa kwa  kilimo cha mazao mbali mbali  kwani  lina  rutuba  ya kutosha iwapo ni mfugaji weweza litumia kwa ufugaji ama kujenga shule  ,kiwanda  n.k 
Shamba  hili  lipo eneo  la Ifunda Kibaoni  jirani na shule  ya sekondari  ya  la Lyandembela  kwa  mawasiliano tupigie simu 0754 026 299/0712 750 199 au 0789281030
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA