Home » » RIPOTI MAALUM YA VYUO VYA HOTEL NA UTALII VISIVYO NA SIFA KUPEWA USAJILI IRINGA,

RIPOTI MAALUM YA VYUO VYA HOTEL NA UTALII VISIVYO NA SIFA KUPEWA USAJILI IRINGA,

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Sunday, September 22, 2013 | 1:33 AM


WAKATI mkoa  wa Iringa na  mikoa  ya nyanda za juu ikiwa  katika harakati  ya kuitangaza mikoa  hiyo  kiutalii uchunguzi  wa mtandao  huu umeonyesha  vyuo  vingi vya  mafunzo ya  hotel na utalii  vilivyopo mkoa  wa Iringa vinaendesha mafunzo  hayo kwa  kudra  za mwenyezi Mungu .

Kwani  mbali  ya  vyuo  hivyo  kutokuwa na sifa ya  kuitwa  vyuo vya  Hotel na utalii bado vinaonekana  kupewa usajili  wa muda  na  uongozi  wa VETA kanda  ya nyanda  za juu .

Mtandao  huu wa www.matukiodaima.com umepata  kutembelea  vyuo  vyote  vinavyoendesha mafunzo ya  Hotel na utalii mkoani Iringa na vilivyo  vingi  ambazo  vinajitangaza  kuwa na  usajili havina sifa ya kuitwa  vyuo  kutokana  na mazingira  yanayozunguka  vyuo  hivyo  huku vyuo  vilivyo vingi vinaonyesha  kufanya  ubabaishaji mkubwa .

Kwani vyuo  hivyo  ukiacha  vyuo  viwili vitatu ambazo  vipo  mjini Iringa ambapo vinaendesha kwa  kuzingatia  sifa  zinazohitajika na VETA ila  bado vinavyobaki  ni aibu  tupu kuviita  ni  vyuo  vya mafunzo  ya Hotel na utalii kwani ukitembelea  vyuo  hivyo  ni aibu  kwa mkoa  na Taifa  kwa ujumla kuigiza  elimu .

Hivi  karibuni VETA  kanda  ilitangaza  kutovitambua  baadhi  ya  vyuo   kutokana na kudai  havina sifa ya kutoa mafunzo  hayo ila cha kushangaza  vyuo vinaitwa  havina sifa  kwa mwonekana na ukichunguza  ndivyo  vinavyoongoza kwa  kukithi sifa  za kuitwa  chuo ila vilivyopewa  usajili  ni  ubabaishaji  mkubwa ndio unaotawala katika  vyuo  hivyo.

Hofu yetu  ni kujidanganya  kuwa  watoto  wetu  wanapewa  elimu ya  vyuo vya  Hotel bora  kumbe  wanadanganywa kwa  uzembe  wa  baadhi ya  wasimamizi  wachache wa VETA ambao wanashindwa  kutenda  haki katika  kusajili  vyuo  kwa  ubora na badala  yake  kusajili kwa kujuana .

Usikose jumapili  ijayo  kutakuwa na mwendelezo  wa habari  hii kwa  kuvitaja  vyuo  vilivyonyimwa usajili japo  vinasifa na  vile  vilivyopewa  usajili  bila kuwa na sifa sitahiki.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA