Home » » RC IRINGA AZINDU MBOLEA MPYA YA YARA AWAONYA WACHAKACHUAJI KUKIANA

RC IRINGA AZINDU MBOLEA MPYA YA YARA AWAONYA WACHAKACHUAJI KUKIANA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, September 24, 2013 | 1:19 AM

 Mkuu wa  mkoa wa Iringa Dr Christine Ishengoma akizundua mbolea  mpya  ya YARA  leo mjini Iringa

MKUU wa  mkoa  wa  Iringa  Dr Christine  Ishengoma  amezindua  ghala  la  kuhifadhia  mbolea  mpya  aina ya YARA na  kuwataka  wakulima  mkoani hapa  kuitumia  mbolea   hiyo  ambayo itaongeza  kasi  ya  uzalishaji  wa  mazao  yao.

Mkuu  huyo  wa  mkoa  pia  amekemea  tabia ya  baadhi ya mawakala  mkoani  Iringa kuacha mara moja  tabia ya  kuwabambka  wananchi  kwa  kuuza  mbolea  feki .

Amesema hayo  leo wakati  wa uzinduzi  wa  mbolea  hiyo mkoani Iringa katika  mkoa  wa  Iringa  na  kuwa  baadhi ya mawakala  wamekuwa si waaminifu na  kuwadanganya  wakulima kwa kuweka  chumvi katika mifuko  ya mbolea  ama  saruji na  kuwadanganya  kuwa ni mbolea  .

Hivyo  amewataka wakulima kuwa  waangalifu  na  mawakala  pia  kuachana na tabia  ya  kuwarubuni  wakulima kwa  kuwauzia mbolea  feki na badala  yake  kuifanya kazi hiyo kwa uaminifu zaidi.

Mkuu  huyo wa mkoa  alisema  kuwa  kampuni  hiyo ya  mbolea ya YARA  imekusudia  kuleta  mapinduzi maklubwa ya kilimo  mkoani Iringa  hivyo ni rai yake  kwa  maofisa  kilimo mkoa  wa Iringa katika Halmashauri zote  kushirikiana na kampuni hiyo katika  kuongeza kasi ya  uzalishaji.

Alisema katika msimu  wa kilimo 2013/2014  mkoa  wa Iringa  umepatiwa mgao wa  mbole  wa kutosha   hivyo  imani ya mkoa  kuona  kiwango cha  uzalishaji kinaendelea  kukua  zaidi.

Hata  hivyo  alisema mbali ya kiwango  kikubwa  cha  vocha  cha pembejeo  kutolea  basi  si wakulima  wote  ambao  watanufaika na vocha hizo .

Pia  mkuu  huyo wa mkoa  alizitaka kamati za  usimamizi  wa  vocha  kufanya kazi  hiyo kwa uangalifu na  kuwa mchezo wa  kucheza na vocha kwa mwaka  huu hautafumbiwa macho.

Hata  hivyo  alisema mbali ya  mkoa  wa  Iringa  kuongoza  kwa uzalishaji ila bado asilimia 52  ya  wajawazito na watoto chini ya miaka  5 mkoani  Iringa  bado imeendelea  kuwakumba  wananchi na kupelekea  mkoa  wa Iringa  kushika nafasi ya  tatu kitaifa cha utapiamlo  kwa  watoto.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA