Home » » MAHAFALI YA 13 YA DARASA LA SABA KATIKA SHULE YA KIMATAIFA YA SOUTHERN HIGHLANDS MAFINGA

MAHAFALI YA 13 YA DARASA LA SABA KATIKA SHULE YA KIMATAIFA YA SOUTHERN HIGHLANDS MAFINGA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Saturday, September 14, 2013 | 2:35 AM


,
Mgeni  rasmi katika mahafali  ya 13  ya  shule ya  kimataifa  ya  Southern Highlands Mafinga Bw Mahenge akitoa vyeti kwa  wahitimu,kushoto ni mkurugenzi   mtendaji wa  shule hiyo Bi Mary Mungai

HOTUBA YA MKURUGENZI MTENDAJI WA SHULE MBELE YA MGENI RASMI MR. DANIEL MPOGOLE MENEJA WA BENK YA WANANCHI MUFINDI (MUCOBA) TAREHE 14/09/2013.


-           Ndugu mgeni rasmi
-           Wajumbe wa Bodi ya shule,
-           Viongozi wa chama na serikali,
-           Viongozi wa dini na madhehebu,
-           Wageni waalikwa na wazazi,
-           Wafanyakazi na walimu wote,
-           Wanafunzi wote,
Ndugu mgeni rasmi,
Ninamshukuru Mungu kwa kutukutanisha sote leo hapa katika shule yetu ya Southern Highlands. Mungu amesimamia na kuongoza safari zetu toka popote na kutufikisha salama, natoa pole kwa uchovu na kwa wale waliopata matatizo madogomadogo wakati wa safari. 
Karibuni wote Southern Highlands School, kwa wazazi hapa ni sehemu ya nyumbani kwenu kwa sababu sehemu ya familia zenu wanaishi hapa.
Ndugu mgeni rasmi,
Tumefarijika sana na tunathamini kufika kwako hapa shuleni leo. Tunaamini nawe umetuthamini, maana umekubali mwaliko wetu. Tunashukuru. Hapa shuleni leo utaona baadhi ya shughuli tunazofanya kwa ujumla wetu, yaani wanafunzi, walimu na wafanyakazi, bila kuwasahau wazazi walioleta watoto.
Ndugu mgeni rasmi,
Shule hii ilianza mwaka 1994 kama Day Care na Pre-school. Mwaka 1997 ikakuwa na kuanza shule ya msingi –Primary School. Mwaka 2001 shule ilitoa wanafunzi wa kwanza wa darasa la Saba. Wanafunzi walikuwa 17, wote walifaulu vizuri na wote walichaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza (Form I).
-           Katika matokeo ya mitihani ya darasa la 7 ya mwaka 2001 Southern Highlands School ilishika nafasi ya kwanza kitaifa katika mitihani ya Somo la Kiingereza.
-           Tulimshukuru Mungu na tunaendelea kumshukuru Yeye. Kwa kuwezesha watoto wetu wa Southern Highlands School, kufaulu vizuri, kwa kishindo.
-           Matokeo mazuri ya wanafunzi wote kufaulu mitihani ya kitaifa ya darasa la saba na wote kuchaguliwa na kuendelea na masomo ya Sekondari umeendelea. Kila mwaka wanafunzi wote wa darasa la saba wanafaulu na wote wanachaguliwa kwenda kidato cha kwanza.
Ninaamini wanafunzi wote wa darasa la saba 47 waliomaliza mwaka huu 2013, watafaulu na kuchaguliwa kuendelea na sekondari. Sababu walikuwa wanapenda masomo na nidhamu yao ni nzuri.
-           Pia walimu wetu wanawajibika vizuri kwa malengo. Walimu wa shule hii wanajitolea sana. Kwa kuonyesha shukurani zetu, Advisory Board ya shule na Board of Director’s imeamua kuwapongeza walimu kwa sh. Kidogo. 
Mgeni rasmi utawakabidhi baadaye.
-           Wamekataa kabisa kushindwa. Ninawasifu, Ninawapongeza. Mungu Awabariki walimu wote na wanafunzi, na wafanyakazi wengineo.
Kutokana na UBORA wa ELIMU na TAALUMA nzuri ipatikanayo Southern Highlands School utamkuta mwanafunzi kutoka Southern Highlands School katika kila shule bora ya Sekondari Tanzania.
-   Ninawapongeza walimu na wanafunzi wote kwa kuwa wengi wao wana hofu ya Mungu.      Wengi wana Nidhamu nzuri. Wanajifunza kwa bidii.
-   Ninawapongeza Wazazi na Walezi kwa kushirikiana na shule na watoto wao katika   kuwaelimisha katika shule bora ya Southern Highlands.
Ndugu mgeni rasmi.
Si wanafunzi wa darasa la saba tu wanaofanya vizuri katika mitihani, ni pamoja na darasa la nne. Kila mwaka wanafunzi wote wa darasa la 4 wanafaulu mitihani yao ya kitaifa.
-           Wanafunzi wa madarasa yote wanafanya vizuri katika masomo yao. Kila mtoto anajitahidi kufanya vizuri ndio maana upo ushindani mkubwa kati ya watoto. Hili linaonekana katika kufungana katika alama na grade katika matokeo ya mitihani yao.
Ndugu mgeni rasmi,
Pamoja na taaluma nzuri na bora katika shule ya Southern highlands, matunzo na malezi ya watoto ni mazuri. Pia watoto wanalelewa katika hali ya kumpenda Mungu ambaye yuko katika madhehebu na dini zote.
-           Nidhamu ya wanafunzi kwa ujumla ni nzuri. Mara chache hutokea uvunjifu wa sheria za shule na mtoto mhusika hupewa adhabu husika.
-           Wazazi wote mmesoma sheria za shule na adhabu zake. Ninaamini mnatusaidia kukumbusha warudipo nyumbani.
-           Hapa naomba ushauri tuboreshe sheria na adhabu kwenye mkutano wa wazazi.
Ndugu mgeni rasmi
Shule yetu ya Southern Highlands School inafundisha masomo yote kw alugha ya kiingereza. Ni ya bweni na kutwa.
 -           Tunapokea watoto wanaohamia kutoka shule zinazofundisha kwa kiingereza na Kiswahili. Tunapokea kwa madarasa ya 1-3 na 5. Pia tunapokea kwa darasa la 4 na 6 kwa wanaotoka shule za kiingereza tu.
-           tunapokea pia watoto wa chekechea na awali kwa watoto wenye umri wa miaka 31/2 hadi 5.
Ndugu mgeni rasmi.
Ninawashukuru sana wazazi/walezi wanaotambua ubora wa elimu itolewayo hapa na kuamua kuleta watoto wao. Wamechagua jambo bora. Ninawashukuru wote ambao hushirikiana na shule kwa kukubali wito, wao kuuliza n.k.
-           Nawashukuru walezi wote na wafanyakazi wote wa shule hii maana kila mmoja katika nafasi yake amejitahidi kufanya kazi vizuri.
-           Kipekee ninawashukuru sana viongozi wa dini na madhehebu yote hasa wale ambao wako karibu na shule kila wakati. Wanakuja shuleni, wanaomba, wanafanya ibada. 
Wanafundisha neno la Mungu kwa kila mtoto kutokana na dhehebu lake. Ninawashukuru sana. Mbarikiwe na Mungu.
Ndugu mgeni rasmi.
Ninashukuru sana kwa ushirikiano uliopo kati ya shule yetu na viongozi wa serikali hasa Idara
ya Elimu, na Ukaguzi wa shule, Idara ya maji, Idara ya Ujenzi na idara ya Ardhi.  Tumekuwa
tukiwasiliana na kushauriwa kila tunapohitaji.
Ninashukuru mashirika yote tunayoshirikiana kuwalea watoto na wote wana Southern
Highlands  e.g TANESCO, MUCOBA,NMB n.k.
Ninashukuru tena ndugu Mgeni rasmi kwa kuwa pamoja nasi na kufanya kazi ya kugawa zawadi na kutunuku vyeti kwa wahitimu wa darasa la Saba.

Asanteni.
Mungu awabariki.
Imeandaliwa na        ………………
                                    Mary  A. Mungai
                                    Mkurugenzi Mtendaji wa Shule.

HOTUBA YA MWENYEKITI WA BODI YA SHULE KWA MGENI RASMI MR. DANIEL MPOGOLE MENEJA WA BENKI YA WANANCHI MUFINDI – (MUCOBA) - KWENYE MAHAFARI YA DARASA LA SABA TAREHE 14/09/2013. -


Mwenyekiti  wa  bodi ya  shule ya  Southern Highlands Mafinga Bw Omary Mahinya akitoa  hotuba ya bodi  mbele ya  wahitimu wa darasa la  saba mwaka 2013
Ndugu mgeni rasmi - Uongozi wa shule - Wajumbe wa bodi ya shule - Wageni waalikwa - Viongozi wa kiroho na taasisi mbalimbali - Mabibi na mabwana. 
 
 Ndugu mgeni rasmi.
 Kwa niaba ya Bodi ya shule na viongozi wa Shule ya Southern Highlands, napenda kuchukua nafasi hii kukushukuru kwa kukubali mwaliko wetu na kufika hapa kubariki hafla hii ya mahafali ya shule yetu ya Southern Highlands. 
 Napenda kuchukua fursa hii kukukaribisha tena Mgeni rasmi ili uweze kutoa nasaha zako kwa vijana wetu wahitimu wa darasa saba mwaka huu 2013.
 Taarifa kamili za taaluma na maendeleo ya shule yetu imewasilishwa na Mwalimu Mkuu. 
Hata hivyo ni vyema nikaongelea tena, kwani tangu shule hii ilipoanza imeonyesha mafanikio makubwa kitaaluma, na ubora wa majengo na mazingira kwa ujumla. 
Katika miaka 4 iliyopita shule yetu imekuwa ikichukua nafasi za juu Kimkoa na Wilaya.
 Kwa vigezo hivi shule hii ya Southern Highlands ni kioo cha Wilaya, Mkoa na Taifa. 
 
Hatuna sababu ya kutojivunia matunda haya ambayo ni zao la Uongozi bora toka ngazi ya Bodi ya shule, Mkurugenzi Mtendaji, Walimu, Wafanyakazi wote na Wazazi ;ambao ni Wadau wakuu wa shule hii. 
Kwa niaba ya Bodi ya shule napenda kutoa pongezi za dhati kwa wote niliowataja hapo juu.
 Hata hivyo mafanikio haya yasingepatikana kama ninyi wazazi na walezi mngekuwa mmetutupa mkono. 
 Wahitimu toka shule yetu wamekuwa wakifanya vizuri katika Sekondari kidato cha IV na kidato cha VI popote walipo kwenda.
 Hii inadhihirisha kuwa Southern Highlands School imewajengea msingi bora wa Elimu ambao ni TUNU ya kujivunia sana. 
 Kwa mantiki hiyo basi, uwepo wako hapa ndugu Mgeni rasmi ni uthibitisho wa Mchango wako kwa shule hii. Nakushukuru sana kwa hilo. Ndugu mgeni rasmi. Uongozi wa shule umehakikisha kuwa kunakuwepo mpango endelevu wa kuboresha mazingira ya shule. 
Viunga vyote vimewekwa katika hali nadhifu, njia za miguu kusakafiwa au kuwekwa kokoto, mifereji ya maji ya mvua imejengwa vizuri.
 Viwanja vya michezo vimeboreshwa na pia upandaji wa maua na miti ya kivuli pia ipo. 
Lengo la uongozi wa shule yetu ni kuhakikisha kuwa Southern Highlands School inakuwa mfano bora na kioo kwa jamii inayotuzunguka kwa kuweka mazingira bora ya kuishi na ya kuvutia kwa yeyote anayeishi hapa shuleni na wageni watakao tutembelea. Ndugu mgeni rasmi.
 Nitakuwa mchoyo wa fadhila, nisipo washukuru wazazi wote na wajumbe wa Bodi ya shule ambao ndio wadau wa maendeleo ya shule hii.
 Natambua kwamba michango yenu imewezesha kwa kiwango kikubwa kufikiwa kwa mafanikio haya tuliyonayo. 
Napenda kuwapongeza na kuwatia nguvu kudumisha moyo huo, na Mungu awabariki. Ndugu mgeni rasmi.
 Napenda kuthibitisha kuwa shule yetu ya southern Highlands imeweza kutekeleza mipango yake endelevu. 
Juhudi zilizofanywa na uongozi wa shule, wazazi pamoja na wadau mbalimbali zimewezesha kutoa matunda mazuri ambayo ni hazina ya taifa letu. 
Hivyo nakuomba kwa niaba ya uongozi wa shule yetu utunuku vyeti vya kuhitimu darasa la saba na tuzo mbalimbali kwa wale wote waliofanya vizuri katika masomo yao mwaka huu 2013.
 Mwisho napenda kuwashukuru wadau wote kwa ujumla wao ambao kwa namna moja au nyingine wamekuwa ni chachu ya maendeleo ya shule. 
Asanteni sana. Imeandaliwa na 
Mr. Omary. Mahinya. Mwenyekiti wa Bodi ya shule- SHS.


wahitimu  wa darasa  la  saba  mwaka  2013  katika  shule  ya  Southern Highlands Mafinga  wakiingia kwa maandamano  ukumbini leo
Meza  kuu  wakiongozwa na mkurugenzi  wa  shule  hiyo ya  Southern Highlands Mafinga
Baadhi  ya  wazazi  wanaosomesha  watoto  wao katika  shule  hiyo bora  mikoa ya  kusini mwa  Tanzania
Mkurugenzi  mtendaji wa  Southern Highlands Mafinga Bi Mary Mungai (kulia) akiwa na  watumishi  wa shule  hiyo wakati wa utambulisho  wao
Walimu na  watumishi wa shule ya  Southern Highlands Mafinga  wakijitambulisha
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA