Home » »

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, September 3, 2013 | 12:41 AM

MAANDAMANO YA MAADHIMISHO YA TAMASHA LA 11 LA TGNP JIJINI DAR ES SALAAM ASUBUHI HII YAFANA -LIVE

Washiriki  wa  tamasha  la  11  la mtandao  wa  jinsia  Tanzania (TGNP) wakishiriki maandamano  ya amani ya  maadhimisho ya miaka 20 ya  mapambano ya   ukombozi  wa  wanawake kimapinduzi
 Wanmaandamanaji  hao  wakiwa na mabango  yenye  jumbe  mbali mbali

Wanahabari  wa  vyombo  mbali mbali  nchini ambao  wamepata  kushiriki katika  tamasha  hilo Tamasha la  11  la mtandao  wa  jinsia  Tanzania  (TGNP) limeanza  kwa  maandamano  katika  ofisi  za  TGNP eneo la Mabibo  jijini Dar es Salaam.

Maandamano hayo  yameanzia lango  kuu la ofisi  za  TGNP na  kuhitimishwa  katika  viwanja  vya tamasha  eneo  hilo la TGNP.

Akizungumza  katika  uzinduzi  wa  tamasha  hilo mkurugenzi  wa  TGNP Usu Mallya  alisema  wakati  TGNP  inaazimisha  tamasha  hilo  bado inajivunia  mapambano makubwa  yaliyodumu kwa  miaka 16 katika  kupigania jengo hilo ambalo lilikuwa na kesi mahakamani hadi  wanaposhinda  kesi  hiyo.

Hivyo  alisema ushindi  wa  kesi  hiyo  dhidi  ya  jengo  hilo  utawafanya  sasa  kuendelea  kuboresha  zaidi  jengop  hilo na kulifanya  kuwa  la kisasa  zaidi na  kuendeleza mafunzo mbali mbali
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA