Home » »

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Monday, September 23, 2013 | 8:44 AM

KISWAGA ASEMA ATAENDELEA KUSAIDIA KUINUA ELIMU NYUMBANI KWAKE KALENGA,AJITOLEA KUSOMESHA WATOTO 8 ACHANGIA TSH MILIONI 1 YA UMEME KUSOMESHA WATOTO WENGINE WAWILI MAGUMBIKE

Mkazi  wa kijiji  cha Nyamihuu kata ya Nzihi jimbo la Kalenga Bw  Jackson Kiswaga kushoto akikabidhi msaada  wa vifaa vya michezo kwa mwenyekiti wa serikali ya    kijiji  cha Magubike Bi  Lenatha Mwayongile leo kwa ajili ya kuendeleza michezo  kijijini hapo
Mwenyekiti  wa serikali ya  kijiji  cha Magubike Bi Lenatha  akimkabidhi mmoja kati ya  walimu  wa shule ya  sekondari ya kata ya Magubike  vifaa vya michezo vilivyotolewa na mfadhili  wa maendeleo wa ndani ya  kijiji  hicho  Bw Jackson Kiswaga  leo
Mgeni  rasmi katika mahafali ya 10 ya shule  ya Msingi Magubike Bw  Jackson Kiswaga  kushoto akimkabidhi  mhitimu wa  darasa la  saba Anna Komba  cheti  chake  cha kuhitimu elimu ya msingi  leo
Mgeni  rasmi  katika mahafali ya  10 ya  shule ya Msingi Magubike Bw  Jackson Kiswaga  akitoa hotuba yake kwa  wazazi na  wahitimu  wa darasa la  saba  leo


Mgeni  rasmi katika mahafali ya 10 ya  shule ya msingi Magubike jimbo la Kalenga Bw Jackson Kiswaga katikati  akiwa  katika  picha ya pamoja na  wahitimu wa  darasa la saba na viongozi  wa  serikali ya  kijiji na kata ya Nzihi pamoja na  walimu  wa  shule hiyo  leo 

..................................................................................................................................
MKAZI wa  kijiji  cha Nyamihuu kata ya Nzihi jimbo la Kalenga  wilaya ya  Iringa mkoani hapa Bw Jackson Kiswaga  amesema  kuwa amelazimika  kurudisha fadhila kwa  wananchi jimbo la kalenga kwa  kuchangia  elimu kama njia ya  kuunga mkono jitihada za  serikali  iliyopo madarakani chini ya Rais Jakaya  Kikwete kwa  kuendelea kufikisha  elimu ya sekondari kupitia shule za kata.

Kiswaga  ametoa kauli  hiyo leo katika mahafali ya 10 ya shule ya Msingi Magubike ambako ameahidi kuchangia kiasi cha Tsh milioni 1 kwa ajili ya kuingiza umema katika  shule hiyo  pamoja na kujitolea  kusomesha  wanafunzi wasio na uwezo wawili elimu ya sekondari na kufanya idadi ya  wanafunzi atakaosomesha  kufika wanafunzi 8 hadi sasa .

Hata  hivyo alisema  kuwa misaada  hiyo ni mwendelezo wake wa kuendelea  kukabidhi misaada mbali mbali katika  shule  za msingi na jamii ya  jimbo la kalenga  kama sehemu ya  kuhamasisha  jamii ya  wana Kalenga  waliosoma katika  shule za msingi na  sekondari  kukumbuka kurudi  kuchangia maendeleo katika vijiji na jimbo  hilo la Kalenga .

Bw  Kiswaga  alisema  kuwa hadi  sasa , pia  kujitolea  kusomesha  watoto  watatu sekondari  na kuchangia kiasi cha Tsh milioni 1.5 kwa  ajili ya kurejesha  umeme katika shule ya msingi Tanangozi .

Pamoja na misaada  hiyo pia amepata  kujitolea  kusomesha  watoto  watatu  katika  shule ya msingi Nyamihuu na kuchangia fedha  za madawati kiasi cha Tsh 500,000 na sasa  shule  hiyo ya Magubike ambayo mbali ya  kujitolea Tsh milioni 1 ya  umeme  pia atasomesha  watoto wawili sekondari na kuchangia Tsh 50,000 kwa  ajili ya ukarabati  wa bomba la maji shuleni hapo na kutoa jezi seti mbili na mipira  miwili kijijini hapo.

Alisema  kuwa  ahadi hizo na misaada hiyo ameendelea  kuitoa baada ya jamii kutoa mialiko katika  shughuli mbali mbali na yeye kutumia marafiki zake  kujipiga piga kwa kuchangia  kiasi na kuwataka  wanakalenga  wengine  kujitokeza  kuchangia maeneo yao na jimbo la kalenga kwa ujumla .

Kuhusu tatizo la simu  kijijini hapo Kiswaga  alisema  suala  hilo lipo nje ya uwezo  wake ila ataendelea  kuwapigania  ili  kijiji  hicho kinachoongoza  kwa uzalishaji wa  tumbaku ,nyanya na mazao mbali mbali ya biashara  kupata  huduma  hiyo ya  mnala  wa simu haraka  iwezekanavyo.

Mkuu  wa shule  hiyo  ya msingi Magubike Bi  Gaithana Kihuyo  akitoa taarifa ya  shule  hiyo mbali ya  kupongeza  misaada  hiyo bado  alisema  walilazimika kumualika  Kiswaga  kama mkazi wa jimbo  hilo ambae amekuwa akijitolea  kuhamasisha maendeleo  kijijini kwake.

Huku  mwenyekiti  wa  serikali  ya kijiji  hicho  Lenatha Mwayongile  akiwahakikishia  wananchi hao  kuwa misaada  hiyo ni changamoto kubwa  kwa  wananchi hasa katika kutambua mkazi  wa kweli anayewajali wananchi na kuwa wataikumbuka daima  .

Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA