Home » »

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Sunday, September 15, 2013 | 4:33 PMBREAKING NEWS;ANAYETUHUMIWA KUMTEKA NA KUFANYA MAUWAJI YA DEREVA BODA BODA AKAMATWA APEWA KIPIGO NUSURU KUUWAWA POLISI ,WAOKOA MAISHA YAKE


kijana anayetuhumiwa kumteka na  kufanya mauwaji ya  dereva  Boda  boda Edga Lalika akiwa amezimia baada ya  kupewa kichapo na madereva  boda boda  leo eneo la Stendi  kuu ya mkoa  wa Iringa baada ya kukamatwa  eneo la Mwangata
Hapa akiokolewa na polisi
Askari polisi mjini Iringa  wakimuokoa mtuhumiwa wa mauwaji ya  dereva  boda boda mjini Iringa
Hapa  akiingizwa katika gari la polisi kunusuru  kuuwawa kwa kuchomwa moto
Wananchi  wakishuhudia  tukio  hilo leo
Polisi  wakimuokoa mtuhumiwa wa mauwaji  ya  dereva  boda boda  leo mjini Iringa
Gari la  polisi ambalo limembeba mtuhumiwa wa mauwaji ya  dereva  boda boda
Msafara  wa madereva  boda  boda  wakilifukuza gari la  polisi kwa nyuma
Mwili  wa marehemu Edga Lalika anayedaiwa kuuwawa na mtuhumiwa huyo juu aliyekamatwa  leo

JESHI  la  polisi mjini Iringa leo  limefanya  jitihada  kubwa  za  kuokoa maisha  ya  mtuhumiwa  mmoja  wa  mauwaji ya aliyekuwa  dereva  boda  boda  mjini Iringa marehemu Edga Lalika  ,baada ya  vijana  wanaofanya kazi  ya  boda boda  kumzingira  kwa  kichapo na kutaka  kumchoma  moto.

 Tukio  hilo  limetokea majira  ya  saa 5.34 asubuhi  katika  eneo la Mashine tatu karibu na  stendi  kuu  ya mabasi   yaendayo  mikoani.

Madereva  boda  boda  hao  zaidi ya 100  walimzingira  mtuhumiwa  huyo  na  kumpa  kichapo  kikali  kabla ya  kutaka kumumwagia mafuta ya  Petrol kwa ajili ya kumchoma moto.


Wakizunguza na mtandao  huu wa  www.matukiodaima.com   kwa  kutotaja majina yao madereva  boda  boda  hao  walisema  kuwa  kijana  huyo amekamatwa maeneo ya  Mwangata  katika Manispaa ya  Iringa akiwa na  pikipiki inayosadikika  kuwa ni mali ya marehemu Edga Lalika aliyeteka  eneo la Mlandege  mjini Iringa kabla ya  kukutwa ameuwawa eneo la Tosamanganga wilaya ya  Iringa  vijijini .

Walisema  kuwa  mwili  wa  marehemu Lalika  ulikutwa  ukiwa katika hali mbaya  huku  sikio moja  likiwa  limekatwa  lote na la  pili kukatwa  nusu  na kichwani  wakiwa  wamemponda kwa kitu kizito .

Hata  hivyo  walisema  kuwa  baada ya  kukamatwa na kupewa  kichapo alidai  kuwa  pikipiki hiyo alinunua  kutoka kwa askari polisi  mmoja ambae hata  hivyo aligoma katakata  kumtaja  jina .

"Lengo  letu kumleta  eneo hili la Mashine tatu ni kutaka  kumuua kwa  kumchoma moto kama  walivyomuua  mwezetu kinyama .....ila  hawa  polisi  wamefika mapema  sana na kuvuruga mpango  wetu"

Mtandao  huu  ulishuhudia askari  polisi  waliokuwa katika  gari la mkuu  wa usalama barabara  lenye  namba za usajili PT 14 67 wakifika  eneo hilo kwa kasi  zaidi  huku wakipiga  king'ora  kuashiria hatari   ,mbali ya askari  hao  pia  askari wengine  wanaolinda  stendi  kuu  walionekana wakikimbia kwa  miguu  huku wakiwa na silaha  kuelekea  eneo la  tukio kuokoa maisha ya  mtuhumiwa  huyo na kumpakia katika  gari na kuondoka nae kwenda  kituo  cha  polisi cha mjini hapa  huku madereva  boda boda wakilifuata  gari  hilo kwa  nyuma kutaka  kumteka mtuhumiwa  huyo .

Mauwaji ya  kijana Edga Lalika  yalitokea  usiku wa kuamkia Septemba  6 mwaka  huu. 

......................................................................................................................................................................................
TANGAZO ,TANGAZO ,
BASI HILI  LINAUZWA KWA  BEI  POA KABISA Basi la kampuni  ya  Sanya One linalofanya  safari  zake kati  ya  Iringa - Dar es Salaam  linauzwa  kwa bei nzuri kabisabasi hili  lipo  katika  hali  nzuri kabisa tupigie  simu namba 0766626373 au 0715004164  kwa  mawasiliano zaidi

 

KARIBU DR MSEKWA CLINIC IRINGA

BABAJI KUBWA ZA ABIRIA SASA ZINAPATIKANA KWA BEI POA ZAIDI KWA MDODE AUTO SPARES IRINGA

 ZS150ZK-LH (SIMBA LION) MAELEZO  ina  ukubwa  wa  kutosha  urefu na upana wa  kutosha sehemu ya  kukaa abiria ni kubwa  ya kutosha  abiria  zaidi watano,ina mataili makubwa .

siti zenye  uwezo mkubwa mbili zinazotizamana kwa ujumla  babaji  hii ni ya kisasa hakunaga  kama  Simba lion Bajaji
SIMBA LION NI BABAJI  ZA  KISASA  KWA AJILI YA  KUSAFIRISHA  ABIRIA  SASA  ZINAPATIKANA  MJINI  IRINGA  KWA MIKOA  YA  NYANDA  ZA  JUU  KUSINI ,WAKALA NI MDOPE AUTO SPARES WAPO  JIRANI NA UWANJA  WA  SAMORA MJINI IRINGA .KWA MAWASILIANO  PIGA  SIMU 0715872890,0754 87 28 90

SOUTHERN HIGHLANDS SCHOOL MAFINGA INATANGAZA NAFASI ZA MASOMO

SHULE YA  KIMATAIFA  YA SOUTHERN HIGHLANDS MAFINGA INATANGAZA NAFASI  ZA MASOMO KWA MWAKA 2014

KWA MZAZI MWENYE MTOTO ANAYETAKA SHULE BORA YA MSINGI NCHINI TANZANIA WAHI NAFASI SASA USAHILI UTAFANYIKA TAREHE 7/12/2013 KATIKA VITUO VIFUATAVYO  


#shuleni Southern Highlands Mafinga 
>Oyster bay -Dar es Salaam

>Msufini -Songea mjini  
>Ilembula mkoa  wa Njombe 
Kwa mawasiliano piga  simu 
0754 209251/0752 840884/0756721040/0754651966

  KWA  ELIMU BORA NCHINI TANZANIA SOUTHERN HIGHLANDS
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA