Home » » BENK YA WANANCHI MUFINDI YAUNGA MKONO JITIHADA ZA SHULE YA SOUTHERN HIGHLANDS MAFINGA , YAJITOLEA TSH MILIONI 2.5 KUSOMESHA WATAKAOFANYA VEMA

BENK YA WANANCHI MUFINDI YAUNGA MKONO JITIHADA ZA SHULE YA SOUTHERN HIGHLANDS MAFINGA , YAJITOLEA TSH MILIONI 2.5 KUSOMESHA WATAKAOFANYA VEMA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Sunday, September 22, 2013 | 11:17 PM


Baadhi  ya  wahitimu darasa la saba Southern Highlands Mafinga
.................................................................................
 
BENK ya  wananchi  wilaya ya  Mufindi ( MUCOBA) imwevutiwa  na  kiwango cha  elimu  kinachoendelea  kutolewa katika shule ya kimataifa ya Southern Highlands Mafinga na  kuahidi  kutoa  kiasi  cha  Tsh milioni 2.5  kwa  ajili ya  kuwafuingulia  akaunti  katika benk hiyo  wanafunzi  watakaofanya  vema  katika matokeo ya  mtihani  huo  mwaka  huu.

Akitoa  ahadi  hiyo  kwa niaba ya  meneja  wa  MUCOBA  mwakilishi wa  benk  hiyo  Ben Mahenge  jana  alisema  kuwa  moja kati ya  sababu  iliyopelekea  benk  yake kujitokeza  kuunga  mkono  jitihada za  shule  hiyo  ni  kutokana na ufaulu  mzuri  wa  mitihani  ya Taifa  ya  darasa  la  saba  ambayo shule  hiyo  imeendelea  kuongoza na  hivyo  kutoa  heshima kwa  wilaya  ya  Mufindi na mkoa  wa Iringa kwa  ujumla .

Kwani  alisema  kuwa  mbali ya  benk hiyo  kuendelea  kutoa  mikopo mbali mbali  ila imekuwa  karibu  zaidi na  shule  hiyo ya  Southern Highlands Mafinga  ambapo  mkurugenzi  wake Bi Mary A. Mungai  ni mmoja kati ya  wateja  wakubwa  wa  benk  hiyo  kutokana na wazazi  wote  wanaosomesha  watoto  katika  shule hiyo  kulipia ada kupitia  benk  hiyo hivyo  kiasi  hicho cha fedha  kilichotolewa na  MUCOBA ni  kutambua mchango  wa  shule  hiyo katika  uendelezaji  wa  benk hiyo. 

" Kati ya  wateja  wakubwa  wa  benk  ya  MUCOBA ni  pamoja na  shule ya  Southern Highlands Mafinga  ambapo  wazazi wa watoto  wanaosomesha  hapo  hulipa ada  kupitia  benk  yetu .....hivyo  kwa  ajili ya  kumpongeza  mkurugenzi  wa  shule hiyo kwa kuzidi  kuiunga mkono  benk  yetu  bado tunazidi  kuwahamasisha  wananchi  wa  wilaya ya  Mufindi na nje ya  mkoa  wa  Iringa kujiunga nasi"
Mahenge  alisema  kuwa  benk hiyo  imeendelea  kutoa  mikopo  mbali mbali  kwa  wateja  wake  ikiwemo mikopo ya  ujenzi  wa  nyumba  bora , ujasiliamali na mikopo  ya kuendeshea  biashara .

Hata  hivyo  Mahenge  alisema  kuwa  wanafunzi  watakaonufaika na msaada  huo  ni  yule  atakayefanya  vizuri katika matokeo  ya mtihami  wa  Taifa  wa darasa la  saba pamoja na mwanafunzi Aida  Mhagama  ambae  aliibuka  mshindi  wa  jumla katika masomo  mbali mbali  na  kupongezwa  wakati  wa  mahafali  ya  darasa  la  saba ya  shule  hiyo .

Alisema  fedha  hizo  zitaingizwa katika akaunti   zao baada ya  kufunguliwa na  benk hiyo  kwa  lengo la kusaidia  kuwasomesha  elimu  ya  sekondari pindi watakaojiunga na  elimu  hiyo ya  sekondari mapema  mwakani .

Mkurugenzi  mtendaji  wa  Southern Highlands Mafinga  Bi Mary Mungai akishukuru kwa  msaada alisema  kuwa  msaada  huo  wa  MUCOBA ni  heshima  kubwa kwa  shule  yake na  kuwa ni chachu  ya shule  hiyo  kuendelea  kufanya  vema zaidi ili  kuwavuta  wahisani  wa ndani  na nje kuendelea  kuiunga mkono  shule  hiyo.

Bi  Mungai  alisema  MUCOBA  hawajakosea  kuunga mkono  jitihada za  elimu  katika  shule  hiyo kwani  kweli ni shule  inayotoa  elimu  bora na toka  ilipoanzishwa  zaidi ya  miaka  13  iliyopita  shule  hiyo haijapata  kufelisha  mwanafunzi hata mmoja.
MWISHO
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA