Home » » WATOTO MARUKUFU KUSIMAMIA HARUSI-WADAU

WATOTO MARUKUFU KUSIMAMIA HARUSI-WADAU

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Monday, August 5, 2013 | 10:54 AM


 Siku  wanahabari  Frank Kibiki na  Tumain Msowoya  walivyofunga  pingu ya maisha 
.............................................................................................................................................................

WANAHARAKATI wa  maendeleo ya  watoto mkoani Iringa wametaka  kuwepo kwa sheria kali kwa  watu  wanaowatumia  watoto  wadogo katika  kusimamia  harusi .

Kwani  wamedai  kuwa katika  siku za hivi karibuni umezuka  mtindo  wa baadhi ya  watu  wa kada  ya kawaida na  viongozi wa umma ,ambao  harusi zao zimekuwa  zikisimamiwa na  watoto ama kupambwa na  watoto jambo ambalo ni kinyume na mkataba  wa kimataifa  wa haki za  mtoto ,sheria  ya mtoto inayohusiana na maendeleo yake.

Hivyo  kutokana na sheria hiyo  wanaharakati hao  wamesema  ni vema  kusimamia vema  sheria  hiyo  ili  kuwabana  wale wote  wanaotumia  watoto katika  kupamba harusi  zao kuwajibishwa .

Usauti ya  wanaharakati hao  imepazwa  leo katika  warsha ya  siku mbili ya  malezi  na makuzi  ya  watoto  inayoendeshwa na asasi  zisizo  za kiserikali za TECDEN na CIC katika ukumbi wa maktaba ya mkoa  wa  Iringa.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA