Home » » WANHABARI IRINGA WATANGAZA KUMALIZA MGOGORO NA JESHI LA POLISI IRINGA

WANHABARI IRINGA WATANGAZA KUMALIZA MGOGORO NA JESHI LA POLISI IRINGA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Friday, August 23, 2013 | 3:27 AM

BW. FRANK LEONARD

RPC MICHAEL KAMUHANDA (ALIYEHAMISHWA)
KLABU ya   waandishi  wa habari mkoa  wa Iringa (IPC) imetangaza rasmi kumaliza mgogoro na jeshi la polisi baada ya aliyekuwa kamanda wa  polisi mkoa  wa Iringa Michael Kamuhanda  kuondolewa mkoani hapo na nafasi yake  kuchukuliowa na kamanda mpya Ramadhan Mungi.
Mwenyekiti wa IPC  Frank Leonard  ametoa tamko  hilo la kumaliza mgogoro na jeshi la polisi mkoa wa Iringa ,leo katika mkutano mkuu maalum wa UTPC uliomalizika leo katika ukumbi wa Hotel ya Gorden Hotel mjini Dodoma.
RPC MPYA IRINGA BW.RAMADHAN MUNGI

Bw  Leonard  alisema kuwa hatua ya  IPC  kutoa tamko hilo ilikuja  baada ya Kamuhanda  kuhusishwa na kifo  cha Daudi Mwangosi aliyekuwa  mwenyekiti wa IPC .

" Ndungu  wajumbe wa UTPC napenda  kuwatangazia  sasa kuwa mgogoro  wetu na jeshi la polisi Iringa  umemalizika baada ya RPC Kamuhanda  kuhamishwa mkoani Iringa na  sasa  tunaendelea  kufanya kazi na jeshi  la polisi Iringa" 
 
 Siku  ambayo  aliyekuwa  mwenyekiti wa IPC marehemu Daudi Mwangosi  alipouwawa katika kijiji  cha Nyororo wilaya ya  Mjufindi ilikuwa ni  septemba 2 /2012 siku ya jumapili majira ya saa 10 jioni.
Habari  hii kwa udhamini  wa Hope service  station na Dr Msekwa Clinic
KARIBU  UJAZE MAFUTA KWENYE GARI YAKO HAPA HOPE SERVICE STATION TUPO JIRANI NA BENKI YA CRDB MIYOMBONI BARABARA YA IRINGA DODOMA 
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA