Home » » WANAFUNZI 80 WASIO NA UWEZO MUFINDI KUPATA UFADHILI WA ELIMU KUPITIA MPANGO WA MUFINDI SCHORLASHIP PROGRAMME -LIVE

WANAFUNZI 80 WASIO NA UWEZO MUFINDI KUPATA UFADHILI WA ELIMU KUPITIA MPANGO WA MUFINDI SCHORLASHIP PROGRAMME -LIVE

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Thursday, August 8, 2013 | 1:47 AM


Baadhi ya  wanafunzi  waliochanguliwa kuingia  katika mpango  wa  ufadhili  wa shirika la Shalom na MUYODESA baada ya  kufanya  vema  mitihani ya  kunying'anyiro  cha kuingizwa katika  mpango  wa  kusomeshwa  ni  vijana   80  ndio  wataanza  kunufaika na mpango  huo 
      

YOUTH EMPOWERMENT, WELBEING OF YOUNG PEOPLE, CARE AND SUPPORT TO CHILDREN & ENVIRONMENTAL CONSERVATION

Taarifa kuhusu Mufindi Scholarship Program (MSP) Tarehe 8/8/2013
Mufindi Scholarship Program (MSP), ni mradi ulioanzishwa na Mashirika yasiyoya kiserikali ambayo ni Mufindi Youth Development and Social Welfare Organization (MUYODESO) na Shalom center for street children.

Muyodeso
Ni shirika lisilo la kiserikali ambalo lilianzishwa na kusajiriwa chini ya sheria ya mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO ACT No. 24 ya Mwaka 2002, lengo likiwa ni kuona kuwa maendeleo na ustawi wa vijana katika Wilaya ya Mufindi, unaboreshwa na kuona kuwa vijana wa familia masikini wanapata elimu bora ili waweze kupata ajira na kupunguza umasikini.

Shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa elimu juu ya maambukizi ya VVU kwa vijana, kupima VVU kwa kutumia Mobile VCT, kutoa elimu kuhusu ujasiliamali, kufanya maandalizi ya ujenzi wa shule ya sekondari na chuo cha ufundi, kuhamasisha jamii ya vijana washiriki kupanda miti ili kuongeza vipato vyao na kuchangia kuhifadhi mazingira na kutoa misaada na huduma kwa vijana mashuleni waishio kwenye mazingira magumu.

Shalom center for street children
Ni shirika lisilo la Kiserikali lililoanzishwa na kusajiliwa mwaka 2005 na linafanya kazi nchi nzima isipokuwa Tanzania Visiwani. Makao makuu ya Shalom Centre yako Arusha. Shalom Centre linasimama katika kulinda na kutetea haki za watoto kwa kuwezesha jamii iliyopo.

Baadhi ya shughuli ambazo Shalom Centre inafanya ni :
Kuwaokoa na kuwazesha wasichana waishio katika mazingira magumu hasa wasichana wanaojiuza
Kuwezesha jamii katika utetezi na ulinzi wa haki za watoto
Kuwaondoa watoto walio katika mazingira hatarishi kwa kuwaweka katika rescue centre au referrals
Kuhamasisha Elimu jumuishi kwa watoto waishio na ulemavu
Kufanya kazi na serikali na wadau wengine wa maendeleo katika kutokomeza unyasasji wa watoto wa kike na kuwawezesha.

Mufindi Scholarship Program
Mradi huu unatekelezwa na Mashirika mawili ambayo ni Muyodeso na Shalom centre for street children ambapo Shalom atakuwa Shirika Kiongozi (lead Organization) na Muyodeso akiwa implementing Partner. Kazi za Mradi ambazo kwa mujibu wa taarifa tulizotoa serikalini tangu Mwezi May, 2013 ni kama ifuatavyo
Kuutambulisha Mradi Serikalini na idara zake za elimu na Maendeleo ya Jamii

Kufanya Mkutano na Maafisa elimu ili kuteua shule kumi na nane za Kata ambazo familia zinazozunguka shule ni maskini (Marginalized family)

Kufanya Mkutano wa Wakuu wa Shule husikaKutunga mithihani, kugawa, kufanya, kusahihisha na kutoa matokeo ya Mthihani huoKufanya Mkutano wa Wakuu wa shule na Wadau wengine wa elimu ili kuzindua Mradi na kuhamasisha jamii kuendelea kukubali kuchangia uboreshaji wa elimu

Kuanza kuwahudumia walioteuliwa na kuendelea kupanua huduma hizo hata katika shule nyingine na madarasa mengine kwa kadri tukavyoona inafaa
Kazi zilizokwishafanyika ni kama ifuatavyo:-

Utambulisho wa Mradi serikalini ulifanyika Mwezi May, 2013
Mikutano na Maafisa elimu na Baadhi ya Wataalamu wa elimu
Mkutano na Wakuu wa shule ulifanyika

Mithihani ya Masomo saba ilitungwa, kufanywa, kusahihisha na kupanga ufaulu
Kazi ambazo hazijafanyika ni Kufanya Mkutano wa Wakuu wa shule na Wadau wengine wa elimu ili kuzindua Mradi na kuhamasisha jamii kuendelea kukubali kuchangia uboreshaji wa elimu
Kuanza kuwahudumia walioteuliwa na kuendelea kupanua huduma hizo hata katika shule nyingine na madarasa mengine kwa kadri tukavyoona inafaa

Tunalenga kuwahudumia vijana 420 (Sawa na Tshs. 88,200,000/=) hadi kufikia mwaka 2015 katika kuwalipia ada na michango mbalimbali ya shule. Mradi unalenga pia kuwahamasisha wadau wengine kuona umuhimu wa kutoa misaada na huduma kwa vijana watokao katika familia masikini katika shule za Kata na ambao uwezo wao wa kufaulu ni wa kuanzia daraja la kwanza hadi la tatu.

Kwa Mwaka huu 2013, tunatarajia kuwahudumia vijana 81 ambao wamefaulu ambapo jumla ya shilingi 17,010,000 zinahitajika ili kuweza kuweza kugharamia ada, michango, vitabu na uniform. 
Uwezo wa Mashirika yetu ni kuwalipia ada na michango mbalimbali ya kawaida na mithihani. Hivyo tunatumia fulsa hii kuhamasisha jamii ili iweze kuona umuhimu wa kusaidia vijana hao.

Pamoja na barua hii ninaambatanisha nyaraka muhimu zinazohusu maelezo ya Mradi wenyewe na Matokeo ya Mithihani ya Kidato cha Tatu kwa shule kumi na nane za Kata ambazo ziko kwenye mazingira magumu (Marginalized family)

Asante

Ndimi

George Kavenuke
Mwenye Kiti wa Kamati ya Maandalizi
Share this article :

+ comments + 1 comments

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA