Home » » WADAU WA WATOTO WAGEUKA MBOGO IRINGA WATAKA WANAOTUMIKISHA WATOTO WABANWE

WADAU WA WATOTO WAGEUKA MBOGO IRINGA WATAKA WANAOTUMIKISHA WATOTO WABANWE

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Monday, August 5, 2013 | 10:55 AM


 Watoto  hawa  wakazi  wa  wilaya ya  Ludewa  wakitoka  kutafuta  kuni kwa matumizi ya nyumbani kama  walivyokutwa na karema ya mtandao  huu  wa  www.matukiodaima.com
 Mtoto  akiwa ameachia mdomo  wazi  kwa uchovu  baada ya  kubeba mzigo mkubwa wa  kuni ni mkazi  wa Mavanga  wilaya ya  Ludewa

WASHIRIKI  wa  warsha ya  malezi na  makuzi ya  watoto mkoani  Iringa  wamewataka  wazazi  na  walezi  wanaotumikisha  watoto kazi  za hatari  kuchukuliwa hatua  za  kisheria.

Mbali ya  wanaotumikisha  watoto  pia  wametaka  wale  wanaobaka  watoto  kupewa adhabu kali  zaidi na   vyombo  vya sheria  ikiwezekana kutumikia  jela  maisha.

Wadau hao  wametoa ushauri huo  leo katika  ukumbi  wa Maktaba ya  mkoa  wa Iringa  wakati  wa  warsha  ya  siku mbili  ya malezi na makuzi kwa  watoto inayoendeshwa na asasi  isiyo zisizo  za  kiserikali za TECDEN na asasi ya malezi na makuzi kwa  watoto nchini Tanzania .

Wakichangia  katika  mada ya  Haki na mahitaji  ya mtoto   wadau hao  wamesema  kuwa  watoto  wameendelea kunyanyasika katika jamii ikiwa ni pamoja na  baadhi ya  watu  kuwatumia  watoto hao kujipatia  fedha  za  kuendesha maisha  yao.

Kwani  walisema  hivi  sasa  vituo  vya kulea yatima  vimeendelea kuongezeka  zaidi katika maeneo mbali mbali ya mkoa  wa Iringa na nje ya mkoa wa Iringa huku  kila anayeanzisha kituo  cha yatima amekuwa akitanguliza maslahi yake  mbele badala ya  kuwasaidia  watoto hao .

"Hivi sasa wengi  wao wanaanzisha  vituo vya yatima kwa ajili ya kupata utajiri na kuishi maisha mazuri  wao na si  watoto na chimbuko la  kuanzisha  vituo  vya yatima  ni baada ya  kuona  waanzilishi waliotangulia wanamiliki magari ya  kifahari na  kujenga  majumba makubwa na ndio  sababu  wengi  wao  wamegeuza yatima  kama mradi  wao"

Kwa  upande wake mwanasheria  wa kituo cha msaada kwa  wanawake na  watoto  mkoa  wa Iringa Bw Jackson Gaso  alishauri  kuwepo kwa adhabu kali  ikiwezekana kuhukumiwa jela maisha kwa  wale  wote ambao watakutwa na hatia katika makosa ya ubakaji kama  njia ya  kukomesha  vitendo  vya ubakaji kwa  watoto.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA