Home » » VIONGOZI WA DINI TUJIEPUSHE NA KAULI ZA KICHOCHEZI-MWALIMU SADICK

VIONGOZI WA DINI TUJIEPUSHE NA KAULI ZA KICHOCHEZI-MWALIMU SADICK

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Thursday, August 15, 2013 | 2:37 AM


                                                         Sadick Shaweji
 ......................................................................................................................................
WAKATI  matukio mbali mbali ya  uvunjifu  wa amani  yakiendelea  kutawala  nchini  wito  umetolewa  kwa  viongozi  wa taasisi  za  dini nchini  kulinusuru  Taifa  na machafuko  hayo kwa wao  kujikita  kuhubiri amani zaidi  badala ya  kuwa sehemu ya  kuvuruga amani kwa  kutoa kauli  za  kichochezi .

Pia  awataka  viongozi  wa dini na  serikali  na kila mtanzani  kuungana   kumuenzi hayati  mwalimu Julius Nyerere kwa   vitendo ikiwa ni pamoja na  kuhubiri amani zaidi  na  kuwa  suala la udini na ukabila  halipaswi kuwa ajenda katika Taifa  hili bali linapaswa  kuepukwa kwa nguvu  zote.

Wito  huo  umetolewa  leo  na   mwalimu  wa msikiti  wa Ilala  mjini Iringa Sadick Shaweji wakati  akizungumza na mtandao  huu  wa www.matukiodaima.com  kuhusiana na hali ya mambo  inavyoendelea  hapa nchini.

Alisema  kuwa  hali ya mambo katika  nchi  yetu kwa  sasa  si nzuri  kutokana na  mfululizo  wa matukio mbali mbali ya  kiuvunjifu  wa amani ambayo  yameendelea  kujitokeza na  kuwa matukio  hayo si tu yanalichafua  Taifa bali yanaweza  kuliweka katika katika hali mbaya  zaidi  kiuchumi   iwapo amani itatoweka  nchini.

" Ndugu  zangu  watanzania  tukitaka   kumuenzi  mwalimu Nyerere  lazima  kuchukia  suala la udini  na ukabila ....iwapo   udini na ukabili ukiachiwa na kupewa nafasi  amani  yetu  itaweza  kuvuruguka.....mfano  mwalimu Nyerere  alisema  kuwa  tusichague  viongozi kwa  kufuata  udini  waka kabila ama rangi yake  kwani  kinachotakiwa kwa  kiongozi  bora ni kuongoza  sio kwenda  kuhubiri "

Alisema  kuwa  viongozi  wa  dini  wanapaswa  kuwa makini  zaidi na kauli ambazo  wanazitoa ili  kuisaidia  serikali  yetu  kuendelea  kutumia  nguvu ya  kulinda amani badala ya  kutumia  nguvu  kulitumikia  Taifa  katika  kuwatumikia  wananchi  wake.

Mwalimu Shaweji  alisema  kuwa  kwa upande  wake  hana  shaka  hata  kidogo  na  serikali iliyopo madarakani kwani  ni  serikali  sikivu  inayotekeleza mambo yake  vema  kwa  kusikiliza wananchi  wake.

Kuhusu  vita  dhidi ya madawa  ya  kulevya  kuhusishwa  kwa  viongozi  wa  dini linapaswa  kuchunguzwa kwa  kina kwani  zipo  tetesi  kuwa  viongozi wa  dini wakitajwa  kutoka dini ya  kiislam na kikristo  ila  lazima  kufanya  uchunguzi  ili kujua  wanaotajwa wanaongoza kanisa gani ama msikiti  upi .

MWISHO
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA