Home » » UTPC YAPINGA MAOMBI YA CHADEMA KUTAKA KUIHUSISHA IPC KTK UJENZI WA MNALA WA DAUDI MWANGOSI

UTPC YAPINGA MAOMBI YA CHADEMA KUTAKA KUIHUSISHA IPC KTK UJENZI WA MNALA WA DAUDI MWANGOSI

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Friday, August 23, 2013 | 2:42 AM
 Makamu mwenyekiti wa UTPC Bi  Jane Mihanji akitoa  tamko  la UTPC dhidi ya  Chadema  kutaka  kutumia  kifo cha Mwangosi kisiasa

 Rais  wa  UTPC Bw  Keneth  Simbaya kushoto akimpongeza makamu wake Bi Jane Mihanjo kwa tamko zuri alilolitoa


Wajumbe  wa bodi  ya  UTPC wakiwa katika  picha ya pamoja na viongozi wa juu wa UTPC baada ya kutolewa tamko la kupinga uamuzi wa Chadema kutaka  kushirikiana na IPC katika ujenzi wa mnala wa marehemu Daudi Mwangosi ,kutoka kushoto ni makamu mwenyekiti Jane Mihanjo ,Rais wa UTPC Keneth Simbaya  na mkurugenzi wa UTPC Bw.Abubakar Karsan
.......................................................................................................... 
BAADA ya chama  cha  Demokrasia na maendeleo ( Chadema) jimbo la Mufindi  kusini kuandika barua ya maombi ya  fedha na kutaka  ushirikiano na klabu  ya  waandishi wa habari mkoa  wa Iringa (IPC) katika ujenzi wa mnala wa kumbukumbu ya kifo cha Daudi Mwangosi ,Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Nchini (UTPC) imetoa tamko la kupinga  hatua  ya  Chadema kutaka  kujitafua  umaarufu kupitia kifo  hicho.

Akitoa  tamko kwa niaba ya  bodi ya UTPC jana , Makamu wa Rais Jane Mihanji wakati  mkutano mkuu maalumu wa kupitisha marekebisho ya Katiba ya UTPC uliyofanyika Mjini Dodoma kwa muda wa siku mbili.

Alisema kuwa Chama hicho kisitumie kifo cha mwandishi wa habari huyo kujinufaisha katika maslahi binafsi ya kisiasa  kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na ukiukwaji wa haki za binadamu katika  kutumia vifo kama mtaji  wa kisiasa.

“..Sisi kama UTPC tunatoa tamko hilo kwa uchungu na pia chama hicho kisitumie kifo cha Daudi Mwangosi katika maslahi ya kisiasa kwani hatuko tayari na swala hilo au zoezi hilo la kujenga mnara kwenye sehemu hiyo kwani tunapinga vikali ujenzi huo unaotarajiwa kufanywa na chama hicho’Alisema Mihanji.

Alisema ujenzi wa mnara huo ambao inatarijiwa kufanywa na chama sio kazi yao kwa ili wanatafuta umaharufu wa kwenye  majukwaa na kuwataka waache wakawaachia wahusika wenyewe  jumuhia za waandishi wa habari ambao ndiyo wenye mamlaka na si vinginevyo.

 Mihanji alisema kuwa, Mwangosi hakuwa mwanasiasa bali alikuwa ni mwana taalumu katika tasnia ya habari “Kwani yeye kufuatia mauaji yake hakuwa  katika harakati za kisiasa bali alikuwa kikazi ambayo ni ya kitaaluma kwahiyo wenye mamlaka ya ujenzi au kufanyiwa jambo fulani la kihistoria ni wahusika ambao ni wanataaluma wenyewe na siyo chama cha kisiasa.

“UTPC ndiyo wenye mamlaka ya kufanya suala au zoezi hilo na siyo chama hicho kwahiyo ni vema swala hilo waakaliacha kama lilivyo kwani sisi ndiyo wahusika kwahiyo tunajua nini tunataka kufanya juu ya Mwangosi kwahiyo tamko letu ndiyo hilo kwa chama hicho swala hilo liachwe na tuachiwe wenyewe”Alisema makamu wa rais huyo.

Mwangosi alikuwa mwandishi  wa kituo cha  Televisheni cha  Chanel ten Mkoani Iringa ambaye pia alikuwa ni mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoani humo (Iringa Press Club) ambapo ameuawa mikononi mwa jeshi la polisi mnamo 2012.
 
Hata  hivyo hadi  sasa  bado suala la kifo cha Mwangosi  limeendelea  kupigwa dana dana  kutokana na kesi yake  kutosikilizwa na  hakuna mwandishi  aliyeitwa  kutoa ushahidi  wake  juu ya mauwaji hayo .
 
 Mwangosi hakuuwawa kama mwanachama wa Chadema bali aliuwawa akiwa kazini kutimiza  wajibu wake wa kitaalum ya uandishi  hivyo kwa  kitendo cha Chadema kutaka kushirikiana na IPC katika ujenzi  huo itakuwa ni kuvuruga mwenendo wa kesi na kupingana na msimamo wa awali ya IPC ,UTPC na vyombo vingine kuhusu taarifa  za awali ambazo jeshi la polisi lilianza  kutaka kupotosha kuwa eti  alikuwa ni mwanachama wa Chadema jambo ambalo si kweli.
Sikiliza  VIDEO  yake  katika  You tube ( andika Tamko la UTPC )

Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA