Home » » SAKATA LA NYUMBA INAYOJENGWA MAKABURI YA MTWIVILA IRINGA KUJULIKANA LEO

SAKATA LA NYUMBA INAYOJENGWA MAKABURI YA MTWIVILA IRINGA KUJULIKANA LEO

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, August 13, 2013 | 4:11 AMHii  ndio  nyumba  inayojengwa katika makaburi ya Mtwivila mjini  Iringa  bila kibali  cha mipango miji ,nyumba  hii  imezungukwa na makaburi na mmiliki kaamua  kuvamia  eneo la makaburi na kujenga
Wananchi  wakitoka  kuzika katika makaburi  ya Mtwivila ambako ujenzi  huu  wa  nyumba  ukiendelea


Nyumba  hiyo ikizungukwa na makaburi kama inavyoonekana hapa

SAKATA    la  nyumba  inayojengwa  katika  eneo la makaburi ya  Mtwivila  katika  Manispaa ya  Iringa  limechukua  sura mpya   baada ya  uongozi  wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa  kutoa magizo mazito  kwa  watendaji  wake.

Hatua  hiyo  imefikiwa  baada ya mtandao  huu  wa www.matukiodaima.com na www.francisgodwin.blogspot.com pamoja  kufichua  ujenzi huo holela  hivyo  kupelekea  uongozi  wa  Manispaa ya Iringa  kuingilia kati  mbali ya kuupongeza mtandao huu kwa  kuendelea  kuibua mambo mbali mbali yanayofanyika ndivyo sivyo na  wananchi  bado maagizo  mazito  yametolewa dhidi ya  wale  wote wanaojenga holela.

  Tayari  mkurugenzi  mtendaji  wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa  Terresia Mahongo ameagiza  mwanasheria  wa Manispaa ,ofisa mipango  miji na ofisa ardhi  kutembelea  eneo hilo na kuchukua hatua  kali kwa  mmiliki  wa nyumba  hiyo  ikiwa ni pamoja na kuivunja haraka.

Akizungumza na mwandishi  wa habari  hizi ofisini kwake  leo  mkurugenzi huyo Bi Mahongo  alisema  kuwa  kamwe hatakubali kuona  watu  wanaendelea  kuvamia maeneo na kujenga  bila  kuwa na kibali kutoka  ofisi ya mipango miji  wala  kupitisha  ramani  zao.

Kwani  alisema  kuwa  eneo hilo ambalo nyumba inajengwa  ni eneo maalum la  kuzika na sio eneo la makazi ya  watu  hivyo hatua ya  mwananchi huyo  kuanza ujenzi wa  nyumba ni kinyume na sheria  za mipango  miji hivyo lazima nyumba  hiyo ivunje haraka .

" Kwanza  napenda  kushukuru sana mwandishi  wa mtandao huu mkoani Iringa kupitia Bw Francis Godwin umetusaidia  kuibua suala  hili ambalo  bila  wewe  tusingejua  kinachoendelea  ila pia nimetazama picha  na  tukio  hili katika Blog yako  kweli  umefanya habari  nzuri  sana ya  kiuchunguzi kwa ajili ya Manispaa ya Iringa na mkoa wetu....nasema  ahsante na kamwe hatuta kaa kimya  lazima  tuchukue hatua"

Aidha  mkurugenzi  huyo alisema kuwa ujenzi  holela  umekuwa  ukiendelea katika  mitaa mbali mbali kutokana  na  baadhi ya maofisa watendaji  wa mitaa kutotambua  wajibu  wao na  kuendelea  kuwafumbia macho  wananchi  wanaojenga  holela.

Hata  hivyo  baadhi ya  wananchi  wanaozunguka  eneo  hilo mbali ya kudai  kuwa mhusika hajulikani ila inaonyesha mmiliki wa  nyumba  hiyo ametapeliwa  na  wajanja kwa  kuuziwakiwanja  hicho katika eneo la makaburi.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA