Home » » NYUMBA INAYOJENGWA KATIKATI YA MAKABURI YA MTWIVILA IRINGA YAWA NGUNZO IRINGA

NYUMBA INAYOJENGWA KATIKATI YA MAKABURI YA MTWIVILA IRINGA YAWA NGUNZO IRINGA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Monday, August 12, 2013 | 9:49 AMHii  ndio  nyumba  inayojengwa katika makaburi ya Mtwivila mjini  Iringa  bila kibali  cha mipango miji ,nyumba  hii  imezungukwa na makaburi na mmiliki kaamua  kuvamia  eneo la makaburi na kujenga
Wananchi  wakitoka  kuzika katika makaburi  ya Mtwivila ambako ujenzi  huu  wa  nyumba  ukiendelea


Nyumba  hiyo ikizungukwa na makaburi kama inavyoonekana hapa
WANANCHI  mbali mbali  wa  mji  wa  Iringa  wameendelea  kujitokeza katika  eneo la makaburi ya Mtwivila  katika Manispa ya  Iringa  kushuhudia ujenzi  wa  nyumba  inayojengwa katikati ya makaburi  hayo na kulichukulia kama ni  tukio la ajabu  kwao.

Baadhi ya   wakazi  wanaozunguka  eneo  hilo la makaburi wameueleza  mtandao  huu  wa  www.matukiodaima.com  kuwa   hadi  sasa hawajapata  kumshuhudia fundi anayejenga  nyumba  hiyo  zaidi ya kuona nyumba  ikiendelea kujengwa .

Hata  hivyo  walisema  iwapo  uongozi  wa mipango miji katika  Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa utafumbia macho  suala hilo la ujenzi  holela kasi  ya  wananchi  kuendelea  kuvamia maeneo maalum kama  hayo ya makaburi itaendelea kuota  mizizi .

Kwani  walisema  wanashangazwa  mwananchi  huyo  kuvamia eneo la makaburi  na kujenga  nyumba huku  viongozi  wa  serikali ya mtaa na  viongozi  mbali mbali wa  serikali  wanaofika  kushiriki  shughuli za mazishi  eneo hilo wakiendelea  kutazama ujenzi huo .

Walisema  kuwa  nyumba  hiyo  inajengwa  huku  ikiwa  imezungukwa na makaburi na  kuwa iwapoitakamilika basi  wakazi  wa  nyumba  hiyo  watalazimika  kucheza na  kujipumzisha  kupunga  upepo  wakiwa juu ya makaburi  ya  watu  waliozikwa  eneo hilo.

Mtandao  huu  unaendelea na jitihada za  kumtafuta mmiliki wa  nyumba  hiyo  ili  kuona kibali  cha ujenzi na ramani yake  kama  imepitishwa na mamlaka  zinazohusika ama lah.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA