Home » » NGURUWE WAZAMIA ENEO LA WAVUVI BWAWA LA MTERA IRINGA

NGURUWE WAZAMIA ENEO LA WAVUVI BWAWA LA MTERA IRINGA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Thursday, August 15, 2013 | 6:22 AM


Nguruwe  wakitafuta  mabaki  ya  samaki katika mitumbwi  ya  wavuvi  wa  samaki bwawa la Mtera  Iringa


Nguruwe  wakiogelea katika  bwawa la Mtera  kusaka  mabaki ya  samaki eneo la  wavuvi

Wavuvi  wa bwawa la Mtera  Iringa  wakitayarisha  vitendea  kazi

Samaki  wa  bwawa la Mtera  wakiandaliwa  kwa umakini mkubwa
 Wavuvi  wakichota  maji kwa ajili ya  kuandalia  chakula
Mvuvi  akiwa kazini  bwawa la Mtera  Iringa
WANYAMA Mbali mbali  wakiwemo Nguruwe na  punda  wameendelea  kusumbua  kambi ya  wavuvi wa  Bwawa  la Mtera  wilaya ya  Iringa mkoani Iringa.
Uchunguzi  uliofanywa na mtandao  huu  wa  www.francisgodwin.blogspot.com na www.matukiodaima.com  umebaini kuwepo kwa  kundi  kubwa la wanyama mbali mbali wakiwemo Nguruwe na punda katika kambi  hiyo ya  wavuvi eneo la Mtera Iringa.
Baadhi ya  wavuvi  katika  eneo  hilo walisema  kuwa  mbali ya nguruwe  kuzagaa katika maeneo hayo  ila hakuna madhara  yoyote  ambayo  nguruwe hao  wamepata  kusababisha kwa  wavuvi ama  kugusa  samaki  wanaovuliwa .
Kwani  walisema  utayarishaji  wa  samaki  baada ya  kuvuliwa  hufanywa  kwa umakini mkubwa na uangalifu  wa hali ya  juu  hivyo nguruwe  hao hawagusi  wala  kusogea  katika matenga ya  kuhifadhia  samaki  hao.
Wavuvi  hao  waliwaondoa  hofu  walaji  wa  samaki  wa Mtera  kuwa mazingira ni  salama na  nguruwe  wanaozagaa maeneo ya kambi  wanafuata  mabaki ya uchafu  wa  samaki  na viumbe  wengine  mara  baada ya kutolewa katika  samaki.
Huku kwa  upande  wao  walaji wa Samaki  waliokutwa  wakinunua samaki katika  eneo hilo  wakiwataka  wavuvi  hao  kuweka mazingira mazuri  zaidi  katika maeneo yao  ili  nguruwe hao  wasipate  kugusa mitumbwi na  vifaa vya  uvuvi.
Mbali ya ushauri huo  bado  wameutaka  uongozi  wa afya  Halmashauri ya Iringa  kutuma  timu ya maofisa afya  kufika  eneo  hilo ili  kuangalia kama mazingira  ya  uvuvi  na utayarishaji wa  samaki  ni  mazuri na yapo  kiafya  zaidi.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA