Home » » MWALIMO WA KUHUDHURIA TAMASHA LA JINSIA NA MAADHIMISHO YA MIAKA 20 YA TGNP

MWALIMO WA KUHUDHURIA TAMASHA LA JINSIA NA MAADHIMISHO YA MIAKA 20 YA TGNP

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Monday, August 26, 2013 | 10:10 AM
 

TGNP mtandao ni asasi isiyo ya kiserikali yenye lengo la kupigania haki za kijamii, usawa wa jinsia, kukuza uwezo wa wanawake, na kubadilisha mifumo kandamizi kiuchumi, kisiasa, kiutamaduni na kijamii.
 Tangu kuanzishwa kwa TGNP mwaka 1993, tumefanya kazi katika kuwezesha mjadala wa kijamii na uelewa kuhusu haki na usawa wa jinsia, ukombozi wa wanawake kimapinduzi, kuwajengea wanawake uwezo pamoja na kushawishi mabadiliko ya   mitazamo ya kijamii katika ngazi zote. 
Tamasha la mwaka huu litafanika  tarehe 3 hadi 6 Septemba 2013, Katika viwanja vya TGNP Mabibo. 
TGNP inatumia majukwaa ya wazi kama  Tamasha la Jinsia kuwapa wanawake fursa ya kushiriki mijadala ya wazi na kupaaza sauti zao, tamasha hili litashirikisha wanawake, wanaume, Vijana na watoto zaidi ya 5000 kutoka mikoa yote ya Tanzania na nchi mbalimbali za  Afrika, Ulaya na Amerika. 
 Kupitia Tamasha hili, wanawake na wanaume wanaoshiriki wanapata fursa ya  kujijengea uwezo wa kutumia mbinu za kiraghibishi katika, uchambuzi wa sera , bajeti ya kijinsia, kujadili kwa pamoja na watendaji wa serikali kuu na za mitaa walioalikwa namna bora ya utoaji huduma ambazo zitamfikia kila mwananchi.
Pamoja na mijadala hiyo ya wazi, kutakuwa na mahakama ya wananchi (Popular tribunal) itakayoendeshwa na Chama cha Majaji Wanawake (TAWJA), watunga sera, wanasheria,  wanaharakati waliobobea kwenye masuala ya Kisheria na wananchi walioathiriwa na mfumo kandamizi na kukosa msaada wa kisheria au kuathika na hukumu zilizotolewa.
 Aidha siku inayofuata kutakuwepo na Bunge la wananchi ambalo litaongozwa na wanazuoni na wataalamu wa sheria na wananchi wote watapata fursa ya kushiriki kikamilifu.
Mijadala mingine italenga katika masual ya haki ya uchumi kwenye upatikanaji wa huduma za msingi za jamii kama maji, afya, elimu, miundombinu na haki ya jamii katika umiliki wa rasilimali ardhi.
Aidha suala la Katiba mpya litapewa kipaumbele katyika mijadala itakayopfanyika ikiwepo kuendelea kudai ushiriki ulio sawia katika fursa na michakato iliyosalia kufikia kupata katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tunakukaribisha kushiriki kwa mawasiliano, ushiriki, au maonesho ya kazi mnazozifanya piga simu namba. 0712-335445 au email:  gf_coordinator@tgnp.org

Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA