Home » » MTOTO AKUTWA AMEKUFA MAJI BWAWA LA KIHESA KILOLO , WANANCHI WATAKA BWAWA LIFUKIWE

MTOTO AKUTWA AMEKUFA MAJI BWAWA LA KIHESA KILOLO , WANANCHI WATAKA BWAWA LIFUKIWE

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, August 13, 2013 | 12:47 AM


 Mjumbe  wa  serikali ya mtaa wa Kihesa  Kilolo Bw Luwago akitazama mwili wa mtoto Oben  Sanga aliyekufa  maji  bwawa la Kihesa  Kilolo
 Wananchi  wakishuhudia mwili  wa mtoto Oben Sanga ukielea majini
 Askari  polisi ,mgambo na  wanajeshi  wakifika  eneo la  tukio katika bwawa la Kihesa  Kilolo  kusaidia kuutoa mwili  wa mtoto Oben sanga  aliyekufa maji
 Mwanahabari Agnes Samson  kushoto  akiungana na  wananchji kushuhudia  tukio  hilo
 Kikosi  cha uogeleaji  kikiwajibika  kuutoa mwili  huo majini
 hapa  baada ya  kuutoa mwili  huo
 Wananchi  wakishuhudia  tukio  hilo
 Nguo  za mtoto  huo ambazo  zilisaidia  kuwafanya  watafutaji  kuanza msako katika maji
 Wananchi  wakilia kwa  uchungu  kufuatia  kifo cha mtoto  huyo
 Polisi  wakiondoka na mwili  wa mtoto  huyo kwenda  Hospital ya  Rufaa ya mkoa  wa Iringa
 
 Mwili  wa mtoto  huyo  ukielea ( TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HII)
Hili ndilo Bwawa  ambalo mtoto  huyo amekufa maji
.........................................................................................................................................

BAADA  ya  mtoto  Obeni  Sanga ( 5)  mkazi  wa Kihesa  Kilolo katika Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa  kukutwa akiwa amekufa maji katika bwawa la Kihesa  Kilolo juzi  ,wananchi  wa eneo  hilo wametaka Halmashauri ya Manispaa kusaidia  kufukia Bwawa  hilo ama kuweka uzio kuzunguka bwawa  hilo ambalo  wamedai kuwa ni hatari kwa  watoto  wao .

Wakizungumza na mwandioshi wa habari hizi  leo  eneo la  tukio  wananachi  wa  eneo hilo  walisema kuwa  bwawa  hilo limeendelea  kupoteza maisha ya  wananchi  wa   eneo hilo na  kuwa kila mwaka lazima  kutokee  tukio la mtu  kufa maji.

Hivyo  walisema  kuwa kutokana na bwawa  hilo  kutokuwa na msaada  mkubwa  kwao  kutokana na maji  yanayopatikana  hapo kuwa machafu  yasio na yasiyotumika  kwa matumizi ya kunywa wala  kupikia chakula  wanaomba  uongozi  wa Manispaa ya  Iringa  kuangalia  uwezekano  wa  kufukia bwawa  hilo ama kuliwekea  uzio kwa usalama  wao .

Akizungumza kwa  niaba ya  wananchi  wenzake  waliofika  kushuhudia  tukio  hilo Yona  kalinga  alisema kuwa bwawa  hilo kwa  sasa  linatumika  zaidi na wakandarasi  wanaojenga  barabara  mbali mbali  ikiwemo  ya  Iringa- Dodoma kwa  kuchota  maji ya  kumwagilia  barabara   wanazojenga .

" Tunashindwa  kujua  kwa  nini Manispaa ya  Iringa  inashindwa  kufukia bwawa  hili ama kuweka uzio kuzunguka bwawa  ili  kuepusha madhara  zaidi  kwa  watoto  na  wananchi  wanaozunguka bwawa  hilo"

Mjumbe  wa  serikali ya  mtaa wa  Kihesa  Kilolo  Mary kabogo  alisema  kuwa  tukio la mtoto  huyo kufa maji lilitokea  juzi ambapo mtoto   huyo alitoweka nyumbani katika mazingira ya kutatanisha mara baada ya  kushiriki  chakula  cha jioni .

Alisema  kuwa  mtoto  huyo ambae  alikuwa akiishi na bibi yake baada ya  kutoweka  uongozi  wa serikali ya  mtaa na  wananchi  walifanya  jitihada za kumtafuta katika maeneo mbali mbali na  kukiri  kuwa  tukio la pili kwa watu  kufa maji katika  eneo  hilo.

Hata  hivyo  alisema uongozi  wa serikali ya mtaa   huo unaungana  na mawazo ya  wananchi kutaka  eneo hilo  kuwekewa  uzio  uli kuepusha ajali  zaidi ya maji kwa  watoto na  watu  wazima.
Kuhusu  mtoto  huyo inasadikika  alikufa maji baada ya  kufika  eneo hilo kwa  lengo la kuogelea  katika bwawa  hilo.

Kabogo  alisema  kupitia miradi ya TASAF  wanampango wa  kupendekeza eneo hilo kuwekwa  uzio kama njia ya  kuwaepushia ajali  zaidi na  kuwa  tayari  suala  la kupendekeza  eneo hilo kuwekewa uzio  lipo katika mipango ya  mtaa huo.Kamanda  wa  polisi  wa mkoa  wa Iringa Ramadhan Mungi amethibitisha  kutokea kwa  tukio  hilo .
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA