Home » » MBUNGE RITTA KABATI ATIMIZA AHADI YAKE KWA VIKUNDI VYA VICOBA ATAKA WANAWAKE WASIKUBALI KUWEZESHWA .......

MBUNGE RITTA KABATI ATIMIZA AHADI YAKE KWA VIKUNDI VYA VICOBA ATAKA WANAWAKE WASIKUBALI KUWEZESHWA .......

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Sunday, August 11, 2013 | 11:12 AM


 Mbunge  wa  viti maalum mkoa  wa Iringa  Ritta Kabati akizungumza na wanachama  wa  VICOBA ambao walifika  kupokea fedha alizokuwa amewaahidi

 Baadhi ya  wanavikundi  vya VICOBA Manispaa ya  Iringa  walionufaika na fedha  za  mbunge Kabati
 Katibu  msaidizi  wa  mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati , Bw  Geofrey Lukuvi akitoa  utambulisho  wa  wageni mbali mbali katika  ukumbi  wa Manispaa ya  Iringa


 Mbunge  wa  viti maalum mkoa  wa Iringa  Ritta Kabati akizungumza na wanachama  wa  VICOBA ambao walifika  kupokea fedha alizokuwa amewaahidi
 Katibu  wa kikundi  cha  vijana walioacha  kutumia  dawa  za  kulevya Manispaa ya  Iringa Bw Geofrey Lukuvi akipokea msaada wa  fedha  kutoka kwa  mbunge Ritta Kabati fedha kwa ajili ya   kuwawezesha kuongeza mtaji katika shughuli yao ya utengenezaji Sabuni, wengine  pichani ni mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Abed Kiponza ,naibu  meya  wa Manispaa ya Iringa Gervas Ndaki

 katibu  wa  timu ya  wanawake mkoa wa Iringa Mwanahery Kalolo  akipokea msaada wa mipira  kutoka kwa mbunge  wa  viti maalum mkoa  wa Iringa  Ritta Kabati (CCM)
Naibu  meya  wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa Bw Gervas Ndaki aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla  hiyo ya  mbunge Kabati  kutimiza ahadi  zake kwa wanachama wa VICOBA jimbo la Iringa mjini
.......................................................................................................................................................

MBUNGE  wa  viti maalum kupitia  chama  cha Mapinduzi (CCM) mkoa  wa Iringa Ritta Kabati amewataka  wanawake katika  jimbo la Iringa mjini kutokubali kuwezeshwa na badala  yake  kuendelea  kujiwezesha  kwa  kujiunga katika  vikundi  vya kukopeshana maarufu kama VIKOBA.

Mbunge Kabati  alitoa kauli  hiyo jana  wakati akiwakabidhi msaada  wa  fedha  zaidi ya Tsh milioni 1.8 ambazo ni sehemu ya ahadi  zake  alizopata  kuwaahidi  wanachama wa VIKOBA katika  jimbo la Iringa mjini.

Alisema  kuwa  ili  kuondokana na kilio  cha kuwezeshwa ambacho  kimekuwa  kikitolewa na  wanawake ni  vema  kuendelea  kujiunga katika  vikundi  vya VIKOBA ambavyo  ni ukombozi mkubwa kwao na vinaweza  kuwakwamua kiuchumi  .

"Lazima  wanawake  sasa tukatae  kuwezeshwa na badala yake  tujiwezeshe wenyewe  kupitia  vikundi kama  hivi  vya VIKOBA ....mimi kama mbunge  wenu nitaendelea kuwa karibu nanyi kwa  kuwaunganisha  katika vikundi na hata katika  taasi  za  kifedha"

Hata  hivyo  alisema  kuwa moja kati ya  jitihada ambazo anaendelea  kuzifanya  ni pamoja na  kuwatafutia uwezeshwaji zaidi wanawake  hao ikiwa ni pamoja na  kuwaunganisha na benk ya  wanawake nchini ili kuja  kutoa  elimu kabla ya  kunufaika na benk hiyo ya  wanawake ambayo ni  benk kwa ajili ya  wanawake  wote nchini

Alivitaja  vikundi  ambavyo amevipatia  msaada  huo wa  fedha  kwa kila  kikundi kati ya Tsh 200,000 na 250,000  kuwa ni  pamoja na kikundi  cha  vijana  walioachana na matumizi ya dawa  za kulevya cha Uvimwema,Vicoba Mashine  Tatu,Vicoba Azimio ,Vikoba Mtwivila,Kanisa la E.A.G.T Frelimo, Kanisa la Presbyterian,Kanisa la T.A.G Kihesa,Pamoja  na  wamsanii wa nyimbo  za injili watatu 

Alisema  kuwa  vikundi hivyo alipata  kuviahidi  kwa nyakati tofauti  wakati wa  ziara yake katika maeneo mbali  mbali ya  jimbo la Iringa mjini.

Mbali ya  kutoa msaada  kwa  vikundi  hivyo  pia mbunge  huyo na viongozi mbali mbali wa  vikundi vya Vicoba na pamoja na mgeni  rasmi naibu meya  wa Manispaa ya Iringa Gervas Ndaki walimchangia zaidi ya Tsh 200,000 kati ya Tsh 400,000 ambazo mwanafunzi Sillo Ally ambaye  anatakiwa  kwenda  kujiunga na kidato  cha tano katika shule ya sekondari ya Songea Boys zinahitajika huku mbunge Kabati akiahidi  kumsaidia kumlipia ada  baada ya mwanafunzi huyo kudai kunyimwa msaada wa fedha  kutoka kwa mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA