Home » » KLABU MPYA YA MOJA MOROGORO PRESS CLUB YAPEWA ONYO KALI NA UTPC

KLABU MPYA YA MOJA MOROGORO PRESS CLUB YAPEWA ONYO KALI NA UTPC

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Friday, August 23, 2013 | 3:11 AM

Mkurugenzi Mtendaji wa umoja wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC), Abubakar Karsan 
....................................................................................................................................................

HUKU kukiwa na taarifa ya  baadhi ya  wanahabari  mkoa  wa Morogoro ambao wanadai  kushindwa katika uchaguzi wa klabu yao kuanza mchakato wa kuanzisha klabu yao mpya  ,uongozi wa umoja  wa  vilabu vya  waandishi wa habari Tanzania (UTPC) umetoa onyo kali kwa  klabu ya moja morogoro Press klabu  kuwa kamwe klabu  hiyo hakitatambuliwa na UTPC itakuwa ni klabu ya  wanahabari wa  vijiweni.

Tamko  hilo limetolea  mjini Dodoma  leo na  Mkurugenzi Mtendaji wa umoja wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania (UTPC), Abubakar Karsan wakati wa mkutano mkuu maalum wa  kupitia rasmu ya katiba  mpya ya UTPC .

Bw  Karsan alisema  kuwa amepokea  taarifa  kutoka mkoa wa Morogoro kuwa kuna baadhi ya  viongozi wa  klabu  hiyo ambao  walishindwa kwenye uchaguzi uliowatoa madakani.

" UTPC inatoa onyo kali kwa  wanahabari  wanaoanzisha  klabu  hiyo ya moja morogoro Press Klabu kwani  hadi  sasa  kwa katiba ya UTPC kila mkoa  unapaswa  kuwa na klabu moja pekee na kwa mkoa wa Morogoro tunatambua klabu ya Moro Press klab pekee  si nyingine ....hatuwazuii kuendelea na mchakato  ila  sema  hiyo klab yao itakuwa ya  kijiweni haitatambulika kamwe na UTPC"

Bw Karsan  alisema  kuwa  wapo baadhi ya  wanahabari  wanaondolewa katika vyama vyao vya msingi kwa kwa utovu wa nidham na kukimbilia  kuanzisha klabu za uchochoroni ambazo kamwe hazitatambuliwa .  

Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA