Home » » HAKUNA MADHARA KWA WATU KUISHI JIRANI NA MAKABURI -MGANGA

HAKUNA MADHARA KWA WATU KUISHI JIRANI NA MAKABURI -MGANGA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Friday, August 16, 2013 | 12:11 AM

Mganga  mkuu  wa Manispaa ya  Iringa Dr May Alexzander
ZIKIWA  zimepita  siku  mbili  toka  mtandao  huu  wa www.francisgodwin.blogspot.com kuibuka sakata  la ujenzi  holela  katika makaburi ya Mtwivila mjini Iringa  na  baadhi ya  wananchi kuwa na imani tofauti  kuwa kuishi makaburini kuwa ni hatari  kiafya ,Mganga  mkuu  wa Manispaa ya  Iringa Dr May Alexzander amesema  kuwa hakuna  madhara yoyote  kifya kwa  watu  kuishi  jirani na makaburi  iwapo taratibu za mazishi yakizingatiwa.

Dr Alexzander amesema  kuwa  kwa  kawaida maeneo ya  ujenzi  katika Manispaa ya  Iringa  yametengwa  na  kwa  asilimia 100 mazishi  katika  makaburi yote  yanazingatia taratibu za  uchimbaji  wa makaburi  hayo kwa  kuchimba futi zaidi ya 5 ambazo  ndizo  zinatakiwa.

Kwani  alisema  kuwa  madhara  kwa  binadamu  yanaweza  kutokea  makubwa zaidi  iwapo  taratibu  za mazishi  hazitazingatiwa .

Hata  hivyo alisema  kuwa  madhara  kwa  binadamu  kupita ama kuishi jirani na makaburi  yanaweza  kujitokeza katika maeneo ambayo taratibu  za mazishi  zinafanyika  chini ya  kiwango kwa  kuchimba makaburi mafupi  zaidi ambapo wanyama kama mbwa wanaweza  kufukua na kupelekea kutokea kwa magonjwa ya mlipuko kwa  wanaopita  ama  kuishi maeneo ya makaburi.

" Hakuna madhara  ya  mtu  kuishi karibu na maeneo ya   makaburi ama  kupita katika maeneo  hayo ....hasa  ukizingatia  kwa  sehemu za mazishi ni  sehemu maalum ambazo  zimetengwa  kwa shughuli hiyo japo kwa kawaida inapaswa maeneo ya makaburi  kuzungushiwa  uzio"

Hata  hivyo  aliwataka  wananchi  wa Manispaa ya  Iringa kuendelea  kuheshimu makaburi na kuepuka  kuvamia maeneo ya makaburi .
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA