Home » » ALIYEKUWA MKUU WA SHULE YA SEKONDARI IDODI RAYMOND MLASU AFARIKI DUNIA

ALIYEKUWA MKUU WA SHULE YA SEKONDARI IDODI RAYMOND MLASU AFARIKI DUNIA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Thursday, August 15, 2013 | 7:16 AM


 Marehemu Mlasu  enzi  za uhai  wake  alipozungumza na mtandao huu wa www.matukiodaima.com juu ya tukio la moto
Aliye kuwa  mkuu wa shule ya sekondari ya Idodi Bw Raymond Mlasu, akiangusha kilio mbele ya ya  aliyekuwa Naibu waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Mwantum Mahiza mara baada ya kumaliza kutoa taarifa kamili kwa waziri juu ya mkas wa  moto  uliosababisha  vifo  vya  wanafunzi  12 Augost 2009

TAARIFA  za  kusikitisha ambazo mtandao  huu  wa  www.francisgodwin.blogspot.com umezipata  hivi  punde  zinadai kuwa aliyekuwa mkuu  wa  shule ya  sekondari Idodi wilaya ya Iringa Raymond Mlasu amefariki  dunia  leo  katika Hospital ya  Taifa  ya  Muhimbili .

Mkuu  huyo  alikimbizwa  katika Hospital  ya Muhimbili  juzi  akitokea  katika  Hospital  ya  Rufaa ya  mkoa  wa  Iringa  kabla ya  leo kufariki  dunia.

Akitibitisha  kutokea  kwa  kifo  hicho  afisa  elimu  sekondari  mkoa  wa  Iringa Leonard Msigwa  alisema  kuwa   mkuu huyo amefariki  dunia  majira ya saa 8 mchana wakati  madaktari  wakiendelea na jitihada za kumtibu .

Alisema  kuwa  mkuu  huyo aligundulika na tatizo la TB japo  kwa  muda  wote  akiwa mkoani Iringa  alikuwa akitibiwa  tatizo la Kisukari .

Msigwa  alisema  kuwa  taratibu  za kuusafirisha  mwili  wa mkuu  huyo  wa  shule  kuelekea  mkoa  wa Iringa  zinafanyika .

Marehemu Mlasu  atakumbukwa  si  tu na familia  yake  bali Taifa zima la Tanzania hasa  ikizingatia  tukio  kubwa la  kihistoria  lililotokea  Augost  24 mwaka 2009  ambapo  bweni moja la  watoto  wa kike  shule  hapo  liliwaka  moto na mkuu  huyo kama mwangalizi mkuu  wa  wanafunzi hao alishindwa  kuendelea  kusoma taarifa  ya mkasa  huo ulivyotokea na  kuangua  kilio  mbele ya naibu  waziri wa  wa elimu na mafunzo ya ufundi Mwantum Mahiza wakati  huo.

Bwana  ametoa na  Bwana ametwaha  jina lake  lihimidiwe  milele  yote AminaHabari  hii  kwa  udhamini mkubwa  RJ COMPUTERS IRINGA NI ZAIDI YA WAOTE

 Mteja  kwetu ni mfalme  huchagua kile  akipendacho 
 Bei zetu ni poa kila  mmoja hufurahia  kununua bidhaa zetu  kwa  bei  poa hapa ni mwanzo na mwisho
 FIka  leo  upate  computers  za  kila aina pamoja na laptop pia
 Aina  mbali mbali  za Computers  zinapatikana  hapa  kwa Iringa  nzima
Kamera   za  kisasa kama Canon na nyingine  zipo


RJ  Computers Iringa ni  wauzaji  na watengenezaji  wa Computers na Laptop za  kisasa pamoja   na  vifaa mbali mbali  hapa ni   chaguo la wengi  piga  simu 0758 780948 au 0714 757197 ama 0685563353
Tupo  opposite na uwanja wa  Mwembetogwa barabara  ya kuelekea shule  ya  sekondari  Mwembetogwa 
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA