Home » » AIRTEL YAMWAGA ZAWADI KWA WASHINDI WAKE WA WIKI

AIRTEL YAMWAGA ZAWADI KWA WASHINDI WAKE WA WIKI

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, August 13, 2013 | 3:42 AM

 Kulia ni Meneja uhusiano wa Airtel Tanzania Bw, jackson Mmbando akiwa
na mshindi wa zawadi ya shilingi milioni moja kwa wiki  hii  Bw,
Rakesh Mawji huku akitoa pesa zake mara baada ya kutumiwa  kupitia
huduma ya Airtel Money. Hafla ya makabidhiano na mshindi huyo
ilifanyika katika ofisi za Airtel jiji ni Dar es salaam leo
 Kulia  ni Meneja wa Duka la Airtel Mako makuu Bi, Happy John  akiwa na
mshindi wa zawadi ya shilingi milioni moja kwa wiki  hii  Bw, Rakesh
Mawji  akihesabu pesa zake mara baada ya kuzitoa kupitia huduma ya
Airtel Money. Hafla ya makabidhiano na mshindi huyo ilifanyika katika
ofisi za Airtel jiji ni Dar es salaam  leo
 Kushoto ni Meneja uhusiano wa Airtel Tanzania Bw, jackson Mmbando
akiwa na mshindi wa zawadi ya shilingi milioni moja kwa wiki  hii  Bw,
Steven Maguru huku akihesabu pesa zake mara baada ya kuzitoa kupitia
huduma ya Airtel Money. Hafla ya makabidhiano na mshindi huyo
ilifanyika katika ofisi za Airtel jiji ni Dar es salaam leo
 Kulia  ni Meneja uhusiano wa Airtel Bw jackson Mmbando akiwa
akimpongeza mume wa mshindi wa wiki hii Bw, Hassan Abdalah mara baada
ya mke wake (kati) Bi Mwajuma kukabidhiwa zawadi yake shilingi milioni
moja na kuitoa kupitia huduma ya Airtel Money Hafla ya makabidhiano na
mshindi huyo ilifanyika katika ofisi za Airtel jijini Dar es salaam
leo
Kati ni Mwalim steven Maguru akionyesha pesa yake kwa furaha kiasi cha
shilingi laki moja aliyotoa kupitia Airtel money mara baaada ya
kushinda milioni moja na kupokea yote kupitia Airtel Money. Kulia ni
mshindi mwingine wa wiki hii Bw, Rakesh Mawji na kushoto ni meneja
Uhusiano wa Airtel bw, jackson Mmbando mara baada ya kukutana na
washindi hao makao makuu ya Airtel jijini dar es salaam leo
................................................................................
 Airtel yakabidhi zawadi kwa washindi saba wa AIRTEL YATOSHA wiki hii
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imewazawadia washindi saba wa
wiki  kiasi cha shilingi milioni saba na kufanya kila mshindi kuondoka
na pesa taslimu shilingi milioni moja.

Meneja masoko wa Airtel, Aneth Muga, aliwataja washindi hao kuwa ni
pamoja na Peter Ignasho kutoka Muheza Tanga, Edita Rweyabura  kutoka
Bukoba, Steven Maguro , Rakesh Ali Mauji, Mwajuma Hassani  kutoka Dar
es Saalam, Siasa Yahaya Songo kutoka  Manyoni Singida na Vero Mispela
Kiwango kutoka Biharamulo.

Akizungumza wakati wa dhima fupi ya kuwakabidhi wateja hao pesa zao,
Meneja Uhusiano wa Airtel, Bw Jackson Mmbando alisema kuwa huo ni
muendelezo wa huduma bora zinazotolewa na kampuni hiyo ya simu kwa
wateja wake nchi nzima.

"Huduma kama hizi zinapunguza kabisa makali ya maisha kwa watanzania
na hiyo inaonesha ni jinsi gani Airtel inawajali wateja wake kwa kutoa
huduma bora ambazo zinaweza kuwaendeleza kimaendeleo na kuwafanya
wapige hatua kiuchumi na kujikwamua kwenye limbwi la umasikini,"
Alisema Mmbando.

Wakielezea furaha zao baadhi ya washindi walisema wanashukuru sana kwa
Airtel kuwazawadia pesa hizo na kusema kwamba watazitumia katika
shughuli mbalimbali za maendeleo.

Airtel imekua ikitoa zawadi mbali mbali kwa wateja wake ambapo mpaka
sasa kupitia promosheni ya Airtlel yatosha imeweza kutoa milioni 30
kwa wateja 30 ambao walishinda milioni moja kila mmoja. 
Sambamba na hilo Airtel pia imetoa nyumba yenye thamani ya milioni 65 kwa mshindi
wa kwanza wa nyumba Bwana Silvanus Juma mkazi wa Iringa.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA