Home » » VETA IRINGA YAVIFUNGIA VYUO VYA MFUKONI .......

VETA IRINGA YAVIFUNGIA VYUO VYA MFUKONI .......

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Thursday, July 4, 2013 | 4:16 AM

Mhitimu  wa ukweli  wa VETA Iringa Perida Erasto akionyesha  cheti kinachotambulika


 ...............................................................................................................................................
Na Eliasa Ally, Iringa
Mkurugenzi wa VETA wa Kanda ya Nyanda za Juu, Bi, Monica Mbelle amevifungia
Vyuo wa Utalii zaidi ya vitatu mkoani Iringa ili visiendelee kuendesha mafunzo ya Utalii na kuwaibia wazazi ada na gharama zingine kutokana vyuo hivyo kushindwa kukidhi vigezo vilivyowekwa na VETA na kuendesha mafunzo hayo bila kuwa na usajiri na kuchukua wanafunzi ambao wamekuwa wakilipishwa wanafunzi wa vyuo vya Utalii ada kubwa bila kuwa na matumaini ya kupata ajira katika maisha yao.
 Akizungumza jana na ofisini kwake,Mkurugenzi wa VETA wa Nyanda za Juu Kusini, Bi. Monica Mbelle alisema kuwa maamuzi ya kuvifunga vyuo hivyo vya Utalii, umefanyika baada ya yeye mwenyewe kuvitembelea na kuthibitisha kuwepo kwa mapungufu makubwa na mengi ambapo vyuo hivyo wanafanya makosa kuanza kuwapokea wanafunzi kabla VETA haijawaruhusu baada ya vyuo husika kukidhi vigezo sitahiki vinavyotakiwa na VETA.

Bi. Monica Mbelle alivitaja Vyuo vya Utalii ambavyo amevifungia na kuvitaka viache kuwapokea wanafunzi na kuendesha mafunzo yao kuwa ni pamoja na chuo cha Utalii ya Ruaha Utalii College, Capricon College na Delima Hotel and Tourism School vyote vipo mjini Iringa ambavyo amesema kuwa kutokana na kukosa vigezo havitaruhusiwa kuendesha mafunzo na kuwa ametoa taarifa polisi, ofisi za Mkurugenzi Manispaa ya Iringa pamoja na ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Iringa ili kuwakamata mara moja endapo wataendelea kuendesha mafunzo na kuwalaghai wanafunzi wao.

Aidha alisema kuwa ameshangazwa na wamiliki wa vyuo hivyo vya Ruaha Utalii College, Delima Hotel and Tourism School na Capricon College kwa kutoa vyeti vya Diploma na Satefiketi vilivyo feki wakati masomo ambayo wamekuwa wakiyaendesha hayafuati mitaala yoyote ambayo imewekwa na VETA na ameonya kuwa endapo wapo wengine wenye mipango kama hiyo anawaasa wafuate sheria na taratibu zilizowekwa na serikali.


Aliongeza kuwa ujenzi wa vyuo vya ufundi na utalii ambavyo vinatakiwa kutoa elimu hiyo awali ya yote hutakiwa kupata ushauri kutoka kwa wataalamu wa vyuo ambao ni VETA ambako kunakitengo maalumu na baadaye vyuo hivyo endapo vitakuwa vimekithi vigezo hutakiwa kupatiwa mitaala ya kufundishia na VETA na siyo kujifanyia wanavyotaka.

Alisema kuwa hata hivyo ofisi yake itavitambulisha vyuo ambavyo vimekithi vigezo vyote na vinatoa elimu ya ufundi na utalii ambavyo tayari VETA imeviruhusu kuendesha masomo yake kuondoa utata unaowakumba wanafunzi na wazazi kwa sasa kwa kuingia gharama zisizo na msingi ambapo pia amewataka wazazi kufika ofisi za mkoa za VETA kujirithisha kama vyuo vinavyojitangaza tayari vimesajiliwa.

Mwisho;

MAANDALIZI YA LIGI KUU, MECHI ZA KIRAFIKI NA KOMBE LA ROLINGSTONE 

Klabu ya Simba Sports Club imepata mualiko wa Waziri Mkuu kwenda Katavi kucheza mechi ya kirafiki ambapo itaondoka tarehe 13/7/2013 na baada ya hapo itaelekea kucheza mechi za kirafiki Tabora, Mwanza na Musoma kabla ya kuweka kambi fupi Kenya na baadae kushiriki mashindano ya Kilimo yatakayofanyika Kisumu Kenya kuanzia tarehe 31/7/2013 hadi tarehe 4/8/2013.
Tarehe za mechi husika na timu zitakazocheza dhidi ya Simba SC zitatangazwa hapo baadae.
Timu ya vijana Simba B inatarajiwa kuondoka tarehe 5/7/2013 kwenda Arusha kwa ajili ya kombe la Rolingstone linalotarajiwa kuanza tarehe 6/7/2013.
SIMBA KUENDELEZA WIKI YA KIJAMII
Simba Sports Club inatarajia kuwa na wiki ya kijamii kuanzia tarehe 5/8/2013 hadi tarehe 11/8/2013 na programu itakuwa kama ifuatavyo:-
5/8-KUTEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA NA KUTOA MSAADA
6/8-KUTEMBELEA WAGONJWA WASIOJIWEZA HOSPITALI NA KUTOA MSAADA
7/8-KUHUDHURIA KOZI/SEMINA ILIYOANDALIWA NA WADHAMINI TBL PAMOJA NA KUTEMBELEA KIWANDA CHA TBL
8/8-SIMBA DAY
9/8-KUTEMBELEA SHULE YA MSINGI NA KUHAMASISHA MICHEZO MASHULENI
10/8-KUTEMBELEA MEDIA HOUSE ILI KUENDELEZA MAHUSIANO MEMA NA VYOMBO VYA HABARI
11/8-KUFANYA DUA NA IBADA KLABU KATIKA IMANI ZOTE (KUWAOMBEA REHEMA WALIOTANGULIA, KUOMBA MEMA KATIKA MSIMU UJAO)
MAENDELEO YA MPANGO MKAKATI WA KLABU (STRATEGIC PLAN)
Open university wameishatuma draft ya kwanza ya Strategic Plan ambapo Kamati ya Utendaji mnamo tarehe 13/7/2013 itakutana na kamati ya marejeo kuipitia strategic plan hiyo ili kuijadili kwa mapana kurudisha mrejesho kwa ajili ya kuandaa draft ya mwisho tayari kuingizwa Mkutano Mkuu wa wanachama.
SUALA LA MATIBABU YA KIGI MAKASI
Timu ya kitabibu ya Simba Sports Club ipo katika mchakato wa kupata “appointment” nchini India kwa ajili ya kumsafirisha KIGI MAKASI kupata matibabu zaidi nchini humo baada ya kupata rejesho la daktari wa timu. Mchezaji husika anatarajiwa kuwa nchini India mwanzoni mwa mwezi ujao.
IMETOLEWA NA
EZEKIEL KAMWAGA
AFISA HABARI
SIMBA SPORTS CLUB
4/7/2013

WAZIRI PROF MAGHEMBE ALIA NA UFISASDI UNAOFANYA NA MAMKALA ZA MABONDE YA MAJI SAFI .......

 
 Waziri Prof Maghembe
..............................................................................................................................
Na Esther Macha, Mbeya
WAZIRI wa Maji Prof.Jumanne Maghembe (Mb)amewataka maafisa wa  Mamlaka  za Mabonde za  maji safi na usafi wa Mazingira Nchini kuacha urasimu wa utoaji wa vibali vya utumiaji wa maji na utupaji  maji taka kwa wananchi  na watu binafsi kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizopo.
Amesema kuwa watu wamekuwa wakiomba vibali hivyo kwa  muda mrefu lakini wamekuwa hawapewi kwa wakati ambao unatakiwa na muda mwingine hawapewi kabisa.
Prof.Maghembe  aliyasema hayo jana wakati wa ufunguzi wa mkutano  wa tano wa mwaka wa bodi za maji za mabonde ambao unafanyika katika hoteli ya  mtenda sun set uliopo Mkoani Mbeya.
“Mpaka kufikia septemba mwaka huu  nataka watu wote  yakiwemo mashirika yalioomba vibali hivyo vya maji  wawe wamepewa  na kama hawatakuwa wamepewa nimepewe ripoti kamili kujua tatizo  gani ambalo linakwamisha”alisema Waziri Maghembe.
Hata hivyo Prof. Maghembe alisema kuwa katika mkutano wa mwaka jana walibaini kuwepo kwa kasi ndogo ya utoaji wa vibali vya kutumia maji na kwamba zoezi hilo haliendani samba samba na mahitaji ya uwekezaji  nchini na kulingana na maombi yanayopokelewa katika ofisi za maji za mabonde.
Aidha  Waziri Maghembe alizitaka bodi za maji za mabonde kuendeleza juhudi za utoaji wa  vibali kwa wakati kwa kuzingatia utaratibu uliopo.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu  wizara ya maji  Mhandisi ,Bashir Mrindoko alisema kuwa  ofisi za mabonde  zimeendelea  na uandikishwaji  wa  watumia maji, pamoja na utoaji wa vibali  vya kutumia maji  na ukusanyaji wa maduhuli  kwa mujibu wa sheria ya rasilimali za maji.
Aidha Mhandisi Mrindoko aliwataka  maafisa wa mabonde  kuacha tabia ya kufanya kazi kwa mazoea  katika maeneo yao ya kazi ambayo wanafanyia.
‘Kitendo cha kufanya kazi kwa mazoea kinafanya hata utendaji kuwa mbovu miongoni mwetu kutokana na tabia tuliyojijengea hivyo ndugu zangu tubadilike ili tuweze kusonga mbele”alisema.
Mwisho.

MAMLAKA YA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA JIJI LA MBEYA YATAKA WANANCHI KUTUNZA MAZINGIRA

Na Esther Macha, Mbeya
MAMLAKA ya Maji safi  na  usafi  wa mazingira Jijini Mbeya imesema  kuwa baadhi ya wananchi wamekuwa hawana mwitikio mkubwa wa utunzaji wa vyanzo vya maji katika maeneo ambayo yanazunguka vyanzo  vya maji na hivyo kusababisha  kuendelea kuharibiwa . 
Hatua hiyo ya wananchi ya kutotunza vyanzo vya maji inatokana na wananchi hao kuendelea kukata miti  nyasi za kulishia mifugo wanyama katika maeneo ya vyanzo hivyo kusababisha vyanzo kuewndelea kuharibiwa.
Kauli hiyo imetolewa  jana  na Ofisa Uhusiano wa Mamlaka  hiyo Jijini hapa Neema Stanton wakati akizungumza na gazeti hili ofisini kwake kuhususiana na mwitikio mdogo wa wananchi katika utunzaji wa vyanzo vya maji .
Santon alisema kuwa  kwa ujumla bado  kuna tatizo kwa wananchi  kuwa  mwitikio wa utunzaji wa vyanzo kutokana na wananchi wenyewe kutozingatia umuhimu wa nyanzo  na hata kutofahamu atharei zake  kwa hapo baadaye.
“Lakini pia wananchi wenginbe huamua  kulisha mifugo ndani ya nyanzo kwa makusudi huku wakifahamu kuwa ni makosa kufanya hivyo,wanafanya tu  ili waone mamlaka itafanya nini  juu yao “alisema Ofisa Uhusiano huyo.
Akizungumzia kuhusu hatua wanazochukua kwa wananchi wanaofanya uharibifu  ndani ya vyanzo ,Ofisa Uhusiano huyo alisema kuwa ,wanachofanya kama mamlaka ni kuwakamata  wananchi wenyewe  pamoja na mifugo  na kutoa elimu na wahusika kuhaidi  kutorudia  kufanya uharibifu.
Aidha Santon alitaja vyanzo vya maji ambavyo vimekuwa vikiharibiwa  na wananchi kuwa  ni iziwa  pamoja na Iduda ambavyo vimekuwa vikisumbua kwa muda mrefu .
Hata hivyo alitoa wito kwa wananchi  kutii sheria kwani maji yapo kwa ajili watu wote kwani  wananchi wakiendelea kulima kwenye vyanzo  maji yatakauka na  hakuna atakayeishi bila maji .
Mwisho.

'DUNIA IMEKWISHA 'MCHUNGAJI WA EAGT AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 30 NA KUCHAPWA BAKORA KWA UBAKAJI

 MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi akiwa mahakamani kungojea kesi yake.
Wananchi Mbalimbali wakisubiri Kusikiliza Kesi ya MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi

   MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi aliye vaa koti Jeupe   akiwa anatolewa mahakamani Baada ya kusomewa kifungo cha Miaka 30 Jela

  Watoto wa MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi wakiwa wanatoka Mahakamani Baada ya Baba yao kusomewa kifungo
  Mtoto wa MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi akiwa anaongeaa na waandishi wa Habari baada ya kesi kumalizika
 Waumini Mbalimbali wakiwa nje Baada ya kesi kumalizika
Watoto wa MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania(EAGT) la Iwambi Jijini Mbeya Daniel Mwasumbi wakiwa nje hawaamini  baada ya kusikia Baba yao anafungwa Miaka 30
 Binti  anaye daiwa kufanyiwa kitendo hicho akilia kwa Uchungu baada ya kesi kwisha(picha  na Mbeya  Yetu Blog)
 ...............................................................................................................................................
Na Esther Macha, Mbeya
MAHAKAMA ya wilaya ya Mbeya imemhukumu kifungo cha miaka (30 )jela na kuchapwa viboko kumi na mbili Mchungaji wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God of Tanzania (EAGT),lililopo Iwambi jijini Mbeya, Daniel Mwasumbi,
Hukumu hiyo imefuatia baada ya mahakama hiyo, kumtia hatiani mchungaji Masumbi baada ya kukutwa na makosa mawili ya Kubaka na kumpa mimba Mwanafunzi wa miaka 19.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu wa mahakama ya Wilaya ya Mbeya Gilbert Ndeuruo, alisema mahakama imemta hatiani kutokana na ushahidi uliotolewa na shahidi namba moja katika kesi hiyo ambaye ni mhanga wa tukio hilo Neema Beni (19).
Hakimu Ndeuruo alisema mahakama imemkuta mtuhumiwa na makosa mawili ya ubakaji na kumpa ujauzito kwa ushahidi uliotolewa na Mhanga mwenyewe pamoja na mwalimu wa Shule aliyokuwa akisoma ambapo alidai shtaka limedhihirishwa pasipo shaka chini ya kifungu cha 235/1985.

Kwa upande wake mchungaji Mwasumbi alipopewa nafasi ya kujitetea, aliomba kupunguziwa adhabu kwa madai ameachiwa watoto na ndugu zake aliozaliwa nao wakiwemo wazazi wake hivyo akifungwa hawatakuwa na msaada.
Kutokana na utetezi huo, Hakimu Ndeuruo alimhukumu kifungo cha Miaka 30 na viboko 12 kutokana na kosa la kwanza, wakati kwa kosa la pili alimhukumu kifungo cha Miaka 5 na kuongeza kuwa adhabu hizo zitaenda kwa pamoja na kulipa fidia ya Shilingi Milion 20 kwa fedha za Tanzania kwa familia ya Mhanga.

Awali akisoma maelezo ya kesi Mwendesha mashtaka wa Serikali Archiles Mulisa, mbele ya mahakama hiyo ilidaiwa kutenda makosa hayo kati ya Mwezi Januari 2008 hadi Mwaka 2011 katika eneo la Iwambi kinyume na Sheria kifungu cha 130(2)e na 131 (1) sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 kwa kosa la ubakaji.
Mulisa aliiomba Mahakama hiyo kutoa adhabu kali kutokana na Mwasumbi kutenda kosa la kinyama tofauti na umri wake na wa binti ambapo Binti ana umri wa Miaka 19 ili hali Mtuhumiwa akiwa na Miaka 57.
 Aliongeza kuwa  mtuhumiwa huyo alimwalibia masomo na maisha yake binti huyo na vitendo hivyo alikuwa akivifanyia sehemu mbali mbali ikiwemo kanisani hivyo aliiomba mahakama hiyo kuvitaifisha na kutoa amri ya Matunzo ya Watoto kwa kutumia amri ya kutaifisha malishtakiwa.

Mwisho.

MSTAHIKI MEYA JERRY SILAA AKUTANA NA MKURUGENZI WA MASOKO NA MAUZO WA MAKAMPUNI YA MeTL GROUP HUSSEIN DEWJI KATIKA MAONESHO YA SABASABA.

IMG_8869
Muonekano wa Banda la MeTL Group lililopo kwenye maonyesho ya 37 kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
IMG_8862
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiwa na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Makampuni ya MeTL Group Hussein Dewji wakati alipotembelea Banda la Kampuni hiyo kwenye maonyesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
IMG_8860
Mstahiki Meya Jerry Silaa akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Makampuni ya MeTL Group Bw. Hussein Dewji ambapo pia alimpongeza kwa bidhaa nzuri wanazozalisha katika kampuni yao.
IMG_8866
Mstahiki Meya Jerry Silaa akiendelea kuzungukia bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na Kampuni ya MeTL Group kwenye banda hilo.
IMG_8857
Mstahiki Meya Jerry Silaa akisalimiana na warembo wanaotoa huduma katika banda hilo ambao wamevalia Khanga zinazotengenezwa kiwanda cha 21 Century Textile cha MeTL .
IMG_3829
Pichani juu na Chini ni Wananchi wakimiminika kwenye Banda la kampuni ya MeTL Group kujipatia mahitaji mbalimbali ya nyumbani zikiwemo Sabuni za kufulia, Unga, Mafuta ya kupikia, Vitenge, Khanga na vingine vingi.
IMG_3840 IMG_3848 IMG_3867
Baadhi ya Kinamama wakisaidiwa kuchagua Khanga na Vitenge na mmoja wa warembo nadhifu wa MeTL wanaotoa huduma kwa wateja katika banda hilo.Picha na Zainul A. Mzige,
IMG_3880
Bidhaa mpya ya Kampuni ya MeTL Group "Sheeba Shake" yenye ladha tatu za kuvutia ikiwemo Vanilla, Chocolate na Banana. Kinywaji hicho kitaingia mtaani baada ya maonesho haya kumalizika. Kinatia nguvu na kukuburudisha.
IMG_3897  

JAJI WARIOBA KUKUTANA NA WANAHABARI KESHO, IJUMAA, JULAI 5 - SAA 4:00 ASUBUHI

 
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, atakutana na Wanahabari kesho, Ijumaa, Julai 5, 2013, kuanzia saa 4:00 asubuhi, katika Ukumbi wa Mikutano wa Tume uliopo katika Ofisi za Tume, Mtaa wa Ohio, jijini Dar es Salaam.
 
Katika mkutano huo, pamoja na mambo mengine, Jaji Warioba atazungumzia mikutano ya Mabaraza ya Katiba ya kujadili Rasimu ya Katiba itakayofanyika katika kila halmashauri ya wilaya. Mikutano hiyo itaanza hivi karibuni. 
Nyote mnakaribishwa.
 
Rgds
--
Omega S. Ngole,
Principal Information Officer,
Constitutional Review Commission (Tanzania),
PO Box 1681,
Dar es Salaam,
Tel: +255 (0) 22 2133425,
Fax: +255 (0) 22 2133442,
Mobile: +255 (0) 757 500800,
Website: www.katiba.go.tz
Facebook:www.facebook.com/people/Omega-Ngole
Twitter: https://twitter.com/OmegaNgole

HILI NDILO KUNDI JIPYA LA MUZIKI WA INJILI LINALOITWA NDEGE WATATU,SASA KUFANYA MAMBO JIJINI


Kutoka kushoto ni Paulyne Zongo, Khadija Mnoga (Kimobitel) na Joan Matovolwa. 
Wanamuziki hao watatu na wakongwe nchini ndio wanaounda kundi hilo litakalojulikana kwa jina la NDEGE 3
Kundi la Ndege 3 linaloundwa na wanamuziki wakongwe katika Tasnia ya muziki wa dansi na kizazi kipya Joan matovolwa, Khadija Mnoga (Kimobitel) na Paulyne Zongo, hivi karibuni limeshatoa kibao chake kinachokwenda kwa jina la 'MISUKOSUKO YA MAPENZI' ambacho redio kadhaa nchini zimeanza kukirusha.
 
MISUKOSUKO YA MAPENZI ni nyimbo ambayo imetungwa kwa umahiri wa hali ya juu, na kuonyesha viwango vya juu katika uimbaji na utunzi.
 
Kwa sasa Joan Matovolwa na Paulyne Zongo ni wanamuziki huru wakati Khadija Mnoga (Kimobitel) ni mwanamuziki anayeimba katika bendi ya Extra Bongo inayoongozwa na Camarade Ally Choki.

MHANDISI WA MAJI LUDEWA MIKONONI MWA TAKUKURU KWA TUHUMA ZA RUSHWA

 
 MKURUGENZI wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah
.........................................................................................................................................
Mwandishi maalumwa matukiodaima.com Njombe 
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoa wa Iringa imemfikisha mahakama mhandisi  wa Idara ya Maji ya wilaya ya Ludewa katika mkoa wa Njombe Bw, Athanasius Munge kwa kumdanganya Mwajiri wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ludewa kwa kumpelekea risiti za malipo hewa kwa madai kuwa kuna wajumbe wa Idara ya maji walikula na kunywa chai wakati wanatembelea miradi ya maji katika wilaya ya Ludewa kwenye mgahawa wa mfanyabiashara Bi. Videa Kayombo jambo ambalo si kweli.

Akisoma mashitaka ya watuhumiwa hao jana, Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU wa mkoa wa Iringa PP Imani Mitume Mizizi kwa watuhumiwa hao wawili mbele ya Hakimu Hassan Juma  wa mahakama ya wilaya ya Iringa alisema kuwa watuhumiwa hao walifanya makosa ya kufoji risiti zao ili wajipatie malipo hayo ambapo katika makosa hayo Injinia Athanasius Kayombo alipatikana na makosa matano ambapo makosa manne yanamhusu Athanasius Munge na kosa la tano wameunganishwa na Bi, Videa Kayombo kwa kufoji risiti feki kwa nyakati tofauti kutoka kwa Bi, Videa Kayombo.

Akisoma mashtaka ya mtuhumiwa Injinia Athanasius Kayombo, Mwendesha Mashitaka wa Takukuru Imani Mizizi alisema kuwa kosa la kwanza katima mwezi October 9 hadi 18, 2008 Injinia Munge alimpelekea risiti mwajiri wake kumtaka alipe kiasi cha shilingi milioni 4,200,000 kwa madai kuwa wajumbe wa idara ya maji walifanya mkutano na kula chakula pamoja na chai katika mgahawa wa Bi, Videa Kayombo na kukiuka sheria ya manunuzi namba 11 ya mwaka 2007.

Mwendesha mashtaka Imani Mizizi alisema kuwa kosa la pili Bw, Athanasius Munge akiwa katika Halmashauri ya wilaya ya Ludewa October 7, 2008 alimpelekea mwajiri wake risiti Na. 0004994 iliyotolewa katika Mgahawa wa Merelendi Mgahawa unaomilikiwa na Bi, Videa Kayombo akidai kulipwa shilingi milioni 4,200,000 kwa madai kuwa wajumbe wa Idara ya maji wa National Rural Water Supply and Sanitation Programe (NRWSSP) walikula chakula pamoja na chai wakadi siyo kweli. 

Mwendesha mashtaka, Imani Mzizi alisema kuwa kosa la tatu October 7, 2008 Injinia Athanasisus Munge alimpelekea pia vocha ya malipo Na. 21 kutoka katika Mgahawa wa Merelindi unaomilikiwa na Bi, Videa Kayombo kwa madai kuwa kamati ya wajumbe wa maji kutoka vijiji vya wilaya ya Ludewa walikusanyika na kulaa chakula pamoja na kunywa chai wakati siyo kweli na kumtaka Mkurugenzi kulipwa malipo ya milioni 4,200,000 mwenye mgahawa huyo.

Mwendesha mashitaka Imani Mizizi alisema kuwa katika kosa Nne Injinia Munge alilifanya October 7, 2008 baada ya kumpelekea (payment voucher) Vocha feki ya malipo mwajiri wake Vocha Na. 5/10 ambayo iliandikwa October 8, 2008 akidai kulipwa milioni 4,200,000 ambapo alidai kuwa wajumbe wa mradi wa maji wa NRWSSP walikula na kunywa chai katika Mgahawa wa Merelindi uliopo Ludewa ambao unamilikiwa na Bi, Videa Kayombo.

Mwendesha mashtaka Imani Mizizi alisema kuwa katika kosa la tano linawaunganisha washtakiwa wote wawili Injinia Athanasius Munge na Bi. Videa Kayombo kwa kula njama za kuandaa hati feki za malipo ya milioni 4,200,000 kwa nyakati tofauti kuanzia October 9 hadi 18, 2008 kwa kulaka kulipwa malipo ya fedha na Halmashauri ya Ludewa kuihujumu serikali kwa malipo hayo hewa.

Katika kesi hiyo watuhumiwa wote wawili walikana mashitaka kutohusika na hujuma hizo ambapo Mwendesha mashitaka Imani Mizizi alisema kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika ambapo alimwomba Hakimu tarehe ya kuanza kuisikiliza kesi hiyo pamoja na kuwaleta mashahidi.

Hakimu Hassan Juma ambaye alikuwa anasikiliza kesi hiyo aliahirisha kesi hiyo hadi July 15, 2013 ambapo watuhumiwa wameshindwa kutoka rumande baada ya kutakiwa kudhaminiwa kwa shilingi milioni 3,000,000 na wadhamini wawili kila mmoja ambapo watuhumiwa hao walishindwa vigezo hivyo na kurudishwa rumande hadi siku ya kesi.

Mwisho

HUYU NDIE MSANII ALIYETUHUMIWA KUMLOGA MSANII MAGUMASHI AJITOKEZA HADHARANI ...........

 Msanii maarufu mkoani Iringa Lackson Luwema  (aliyevaa suti) aliyepata  kutuhumiwa  kumloga msanii mwenzake Magumashi leo amejitokeza na kukanusha taarifa  hizo na kumaliza ugomvi wake na msanii Magumashi
 Huu ndio  usafiri  wa msanii Lackson aliokuja nao  leo
 Huyu ndie  msanii Lackson aliyetuhumiwa kumloga mwenzake  leo afichua siri ya  kutuhumiwa
 Huyu ndie msanii Magumash akiwa katika gari ya mhasimu  wake aliyedai awali kuwa analoga kazi zake zisipate soko
 Msanii maarufu wa Filam mkoa wa Iringa Erasto Kilowoko a.k.a Magumashi kulia akiwa na msanii Lackson ambae  alimtuhumu kuwa ni mcahwi
hapa  wasanii hao  wakionyesha  umoja baada ya kumaliza  tofauti  zao na kuwa kitu  kimoja 

LILE sakata  la msanii   maarufu wa Filam mkoa wa Iringa Erasto Kilowoko a.k.a Magumashi kudai  kulongwa na msanii  mwenzake Lackson Luwema limemalizika baada ya mtandao  huu wa www.matukiodaima.com kuwakutanisha  mahasimu hao na  kumaliza  tofauti yake  huku Lackson akitoa siri ya  kuzushiwa mambo kuwa ni kutokana na jitihada  zake.

Msanii Luwema ambae ni mmoja kati ya manguli wa  kuigiza Filam mkoani Iringa amesema kuwa kwa upande wake  katika mkoa  wa Iringa amekuwa akifanya  vema katika tasnia ya filam na kuwa hakuna msanii wa mkoa wa Iringa ambae hajui jitihada zake.

Luwema alisema kuwa  mbali ya kuonyesha uwezo katika tasnia hiyo ya uigizaji ila bado yeye ni mmoja kati ya  wasanii ambao wanafanya kazi kwa  kumtegemea mwenyezi Mungu  zaidi kwani yeye amekulia katika mazingira ya ulokole  hivyo kamwe hatajiingiza katika mambo ya shetani ya  kutumia ndumba katika kazi  hiyo ambayo anaamini ni kipaji toka kwa mwenyezi Mungu.

Hata  hivyo amesema  kuwa tatizo la wasanii  wengi wa mkoa  wa Iringa hawataki  kujibidiisha kwa kuboresha kazi zao na badala yake  wamekuwa  wakikurupuka katika kuingia katika tasnia hiyo  bila  kujiandaa vya kutosha na mara  baada ya mambo kwenda  kombo ndipo  huanza  kutafuta mchawi  wa kukamwa kwao  huku wakitambua kuwa  wameingia kichwakichwa katika fani.

Msanii Luwema ameendelea  kujizolea umaarufu mkubwa kupitia filam zake mbali mbali ambazo amepata kutoa ikiwemo la  Polisi Jamii,Yoshua na Stress  na sasa  ni mmiliki wa kundi la sanaa la Mundu sanaa Group ambalo limeendelea  kutikisa  vichwa vya wasanii mkoani Iringa .

Akieleza malengo yake ya mbele amesema kuwa kwa  sasa yupo mbioni kutoka filam nyingine inayokwenda kwa  jina la Hostages ambayo itakuwa ni funika mbaya na kuwataka  watanzania  kujiandaa kuona filam hiyo.

Kwa upande  wake msanii Magumashi baada ya kukutanishwa pamoja  na kuelezwa ukweli na msanii huyo aliyekuwa akihisi  kuwa kikwazo  cha maendeleo yake ameupokea ushauri  uliotolewa kwake na kuafikiana  kumaliza  tofauti  zao na kuchapa kazi zaidi.

 HII  NDIO STORI YA  AWALI  ILIYOCHAPISHWA HAPA JUNE 25 ,2013 

MSANII FILAM IRINGA ADAI KULONGWA NA MSANII MWENZAKE

 
Msanii maarufu  wa Filam mkoa  wa Iringa Erasto Kilowoko a.k.a Magumashi akionyesha kazi  zake
 
MBALI ya kupiga hatua katika tasnia ya uigizaji na kufanikiwa  kutoa DVD inayokwenda kwa  jina la Bi MUWASHO ambayo  imetokea  kupendwa  zaidi na  watanzania ambao wamefanikiwa  kuinunua ,msanii maarufu katika uigizaji mkoa  wa Iringa Erasto Kilowoko a.k.a Magumashi ametinga ofisi  za mtandao  huu wa  www.matukiodaima.com na  kuibua tuhuma dhito dhidi ya msanii mwenzake kuwa amekuwa akiloga kazi  zake.
 
Msanii huyo alisema  kuwa msanii   ambae amekuwa akimloga  ni kiongozi  wa  wa  kundi la sanaa mjini Iringa ( jina lake limehifadhiwa  ) na  sababu  za  kufanya hivyo ni kutokana na kuona mafanikio makubwa ambayo ameanza kuyapata na  kufanikiwa kulitupa mbali  kundi linaloongozwa na msanii  huyo mwenye roho ya  kwanini.
 
Magumashi  amesema  kuwa kazi  ambayo ameitoa  inayokwenda  kwa jina la  Bi Muwasho  ameisambaza katika  mkoa  wa  Ruvuma, Dodoma na Iringa na  kuwa  kazi hiyo  imepokelewa vizuri na  wadau  wa sanaa ya maigizo na  hivyo  kupelekea kiongozi  huyo  wa  kundi la Sanaa linalofanya mazoezi yake katikati ya  mji  wa Iringa kuingiwa na  hofu na  hivyo kuanza  kutumia ndumba kuzoofisha jitihada  hizo.
 
Hata  hivyo  mbali  ya  kumuonya kiongozi huyo Mlogi bado  amesema yeye anamtegemea  zaidi Mwenyezi Mungu na  kuwa kamwe jitihada zake  za  kukwamisha kazi  zake hazitafanikiwa kwa  sasa.
 
Pia  alisema  kwa  sasa yupo mbioni  kutoa kazi  nyingine inayokwenda kwa  jila la Kiboko yao ambayo itakuwa funika mbaya .
 
Akielezea  kwa masikitiko makubwa juu ya ubaya anaofanyiwa na kiongozi huyo wa kundi la  sanaa mjini Iringa amesema  kuwa hivi  sasa mbali ya  kutoa kazi ya kwanza na kuendelea  kuiandaa ya  pili ila bado hakuna maendeleo yoyote na pesa anayoipata hafanyii kituo chochote  cha maendeleo  na hadi  sasa hana  pesa hata ya  kununua kiatu  wala kandambili

DIWANI CHONANGA ALIONYESHA UWEZO WAKE WA KISISASA MBELE YA KINANA ..............

Katibu  wa CCM Taifa Bw  A.Kinana akielezwa jambo na  marehemu  Idd Chonanga  aliyekuwa  diwani wa kata ya Nduli enzi ya uhai wake ,kushoto ni mwenhyekiti  wa CCM mkoa  wa Iringa Jesca Msambatavangu.

Akizungumza na katibu mkuu  Bw Kinana  siku alipofika kumpokea katika uwanja  wa ndege wa Nduli Iringa  wakati wa Kinana alipokuwa akipita kuelekea  ziara  mkoa wa Njombe ,Chongana  alisema  yeye ndio  kijogoo wa  kata  hiyo na CCM hivyo hata kama atakufa  bado CCM itaendelea  kuongoza katika kata  hiyo ya Nduli.
 
Chonanga  ambae alikuwa ni mmoja kati ya madiwani wanaojiamini na madiwani  wenye nguvu kubwa kwa maana ya ubabe katika kata  ya  Nduli alikuwa ni kiongozi mwenye msimamo na ni mtu  anayejiamini  zaidi katika kusimamia  kauli yake na hata  siku moja hakuwa tayari  kushindwa kwa jambo lolote  lile.

..................Itaendelea .........

TAARIFA TOKA KWA FRANCIS GODWIN BLOGU KWA WAMILIKI WA BLOGU WOTE AMBAO WANAKAWAIDA YA KUIBA KAZI ZANGU , SASA NASEMA INATOSHA NIPO TAYARI KUCHUKUA HATUA ….Francis Godwin ::Mzee wa matukio daima::


AWALI  ya  yote  tunapenda  kuwapongeza  wadau mbali mbali ambao  wameendelea  tukuunga mkono kwa kujitangaza kupitia kampuni yetu  ya Free community Media’s wamiliki wa blogu   ya  www.francisgodwin.blogspot.com ,www.matukiodaima.com na www.Iringa na maendeleo  yetu .blogspot.com ,nasema ahsanteni  kwa  kutuunga mkono .


Pamoja na  shukrani hizo kwa  wadau wetu   wakiwemo  wasomaji  pia ila tunapenda  kutoa onyo kali kwa  wamiliki wa mitandao ya  kijami zikiwemo Blogu ambao  wamekuwa  wakiiba kazi zetu  na  kuzitumia  bila kuingia makubaliano yeyote  nasi .


Ifahamike  kuwa kutumia habari  zetu  katika blogu  ama mtandao wako  au gazeti  lako  bila ya  makubaliano yetu ni sawa na wizi na huna tofauti na mwizi  hivyo basi kutokana na  vitendo vya wizi  wa kazi zetu   kuendelea kuongezeka Tumelazimika  kumpa  rungu mwanasheria  wetu ili  kuchukua hatua  kwa  wale wote watakaobainika kuiba kazi zetu  na kuzitumia bila makubaliano yetu.


Tumevumilia tumechoka  sasa  hatuaacha kuchukua hatua kali ili iwe fundisho kwa wenye tabia ya  kuiba kazi zetu na kuzitumia bila  ridhaa yetu .


Ushauri  wangu ni vema  kila mmoja  wetu  kutambua mchango  wa  mwingine kwa  kila anachokifanya  kwani  uendeshaji wa mitandao  hii ni kama  chombo kingine cha habari  lazima kutafuta  habari kwa gharama na  kulipa  wafanyakazi na mahitaji mengine yote  sasa kama wewe  huchangii chochote katika uendeshaji wetu  huna  sababu ya kutumia habari zetu  bure vinginevyo kwa  kila habari utakayoitumia hapa utailipia ama tutachukua hatua  dhidi  yako.

  Kwa  upande wa radio ambazo zinaweza  kutumia habari  zangu kwa Tanzania ni pamoja na Radio Clouds Fm, Radio Uhuru Fm, Radio Mlimani Fm ,Radio  Ebony Fm, Radio Furaha Fm, Radio Ovarcomers Fm, Radio Best Fm ( Ludewa) na Radio V.O.A


Kwa upande wa magazeti ni magazeti ya  Uwazi , Amani, IJumaa, Risasi  na  yote ambayo yanayohusika na kampuni  husika  ,Gazeti la Mwananchi  na gazeti la Daraja Letu .

Wakati upande wa mitandao ya jami inayoweza  kutumia kazi zetu kwa makubaliano ni , Issma Michuzi, Mjengwa, Fullshangwe, Watemi  SHAFFIH DAUDA na Milad Ayo wa Clouds ,  MATUKIO UKBBC SWAHILIVOA SwahiliMAFANIKIO NA MAISHADIAMOND PLATINUMZGLOBAL PUBLISHERSDAILY NKOROMO BLOGCCM BLOG ,Chadema Blog ,  BONGO LEAKS , MATERUNI ,sundayshomari, ASKOFU BOAZ SOLLO ,kamanda  wa matukio ,mohammeddewji,Mbeya yetu ,mzalendo25 blog jamiiforums.com  na  shwari.com zaidi  ya  hapo tutaonana  wabaya nimechoka kuibiwa kazi  zangu .

Pia napenda  kutoa onyo kwa badhi ya  waandishi ambao  wamekuwa  wakitapeli wadau kwa  kujitambulisha  kuwa wanafanya kazi na kampuni ya  Free Community Media’s  kupitia matukiodaima ama francisgodwinblog

Wafuatao ni  wawakilishi wetu  Estha Macha  ( Mbeya) , Elizabeth Ntambala ( Rukwa na Katavi),Juma Nyumayo ( Ruvuma), Tuma Sitta (Mwanza), Carlos Mtoye ( Dar es Salaam),Gustav Chahe , E. Materu , Kayanda MC , Mlalahoi Alwatan,Lukelo Mkami ,  (Iringa) japo wengine  kwa Iringa utawatambua  wiki ijayo Abdulaziz Video ( Lindi) Ally Suleiman ( Zanzibar) Anna John na Gadiola Emmanuel ( Arusha) Frank Ndelwa ( Dodoma) Bazil Makungu ( Njombe) mikoa  mingine  bado tunatafuta waandishi  wawakilishi
Imetolewa na Francis Godwin Blog -mzee  wa Matukio daima

 0754 026 299,0789 28 1030

Barua  pepe .francisgodwin2004@yahoo.com

MLEZI WA CCM MKOA WA IRINGA WAZIRI PINDA KUTUA IRINGA KWA SHUGHULI ZA CHAMAWaziri  mkuu Mizengo Pinda 
..............................................................................................
 Wakati  chama   cha mapinduzi  (CCM) mkoa  wa  Iringa kikiwa katika majonzi kufuatia  pigo  kubwa la  kumpoteza  diwani wa kata ya Nduli Idd Chonanga aliyefariki jana kwa ugonjwa ,mlezi wa CCM mkoa  wa Iringa  waziri mkuu  Mizengo Pinda kutua Iringa leo jioni kwa  shughuli za chama  kesho.

Taarifa  zaidi utaipata  hapa  endeleo  kutembelea mtandao huu kila wakati kwa habari moto moto 

GARI LA EMERGENCY LA TANESCO LAPIGWA 'STOP' KUINGIA OFISI ZA MANISPAA YA IRINGA NA WALINZI

Fundi  wa Tanesco  mjini Iringa akifanya marekebisho ya umeme nje ya ofisi ya Manispaa ya Iringa baada ya kuwepo kwa tatizo la umeme toka jana
Fundi akiwa amemaliza kazi akishuka juu ya nguzo
Hili ndilo gari la Tanesco  lililozuiwa na  walinzi wa Manispaa ya Iringa  kuingia ndani ya uzio wa Manispaaa ya Iringa leo asubuhi
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA