Home » » UONGOZI WA TANESCO KIBAO MUFINDI VIPI?

UONGOZI WA TANESCO KIBAO MUFINDI VIPI?

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Friday, July 26, 2013 | 11:49 AM


Bro naomba  kuuliza swali  kuhusu hawa tanesco Mafinga wilaya ya  Mufindi ambao  sasa  wamefungua  ofisi Mufindi kwa Mugeluka  kijiji  cha  Kibao  katika  nyumba ya Mwarabu leo ni  leo ni  tarehe 27 walikuja na watu wakaenda lipa bili za umeme.cha kushangaza hawaandikitarehe ya leo na badala yake wanaandika tareh 29.je hii ni halali????? 

pia kuna mama mmoja mjane yupo kibao leo kaenda lipa bili cha ajabu yule mama  kabla haja fika officen akiwa njian tanesco wameenda kuchomoa cutout nyumban kwake kwa madai kuwa  mama  huyu ana nyumba mbili lakini hii nyingine wanakaa wapangaj inajitegemea iko mbali na yeye na ina mita yake.

Inasemekana huyo mpangaji hajalipa bili ya mwezi ulio pita anadaiwa  sasa basi  baada ya kwenda kukata umeme nyumbani  kwa huyo mpangaj wamekata nyumba anayoishi mwenye nyumba Je hii ni haki? au kwa sababu huyo mama huyu ni mjane na wanawe wapo mbali na tanesco wanajibu jeuri sana  Je afanyeje kumsaidia?
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA