Home » » TAARIFA TOKA KWA FRANCIS GODWIN BLOGU KWA WAMILIKI WA BLOGU WOTE AMBAO WANAKAWAIDA YA KUIBA KAZI ZANGU , SASA NASEMA INATOSHA NIPO TAYARI KUCHUKUA HATUA ….

TAARIFA TOKA KWA FRANCIS GODWIN BLOGU KWA WAMILIKI WA BLOGU WOTE AMBAO WANAKAWAIDA YA KUIBA KAZI ZANGU , SASA NASEMA INATOSHA NIPO TAYARI KUCHUKUA HATUA ….

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Thursday, July 4, 2013 | 3:05 AMFrancis Godwin ::Mzee wa matukio daima::


AWALI  ya  yote  tunapenda  kuwapongeza  wadau mbali mbali ambao  wameendelea  tukuunga mkono kwa kujitangaza kupitia kampuni yetu  ya Free community Media’s wamiliki wa blogu   ya  www.francisgodwin.blogspot.com ,www.matukiodaima.com na www.Iringa na maendeleo  yetu .blogspot.com ,nasema ahsanteni  kwa  kutuunga mkono .


Pamoja na  shukrani hizo kwa  wadau wetu   wakiwemo  wasomaji  pia ila tunapenda  kutoa onyo kali kwa  wamiliki wa mitandao ya  kijami zikiwemo Blogu ambao  wamekuwa  wakiiba kazi zetu  na  kuzitumia  bila kuingia makubaliano yeyote  nasi .


Ifahamike  kuwa kutumia habari  zetu  katika blogu  ama mtandao wako  au gazeti  lako  bila ya  makubaliano yetu ni sawa na wizi na huna tofauti na mwizi  hivyo basi kutokana na  vitendo vya wizi  wa kazi zetu   kuendelea kuongezeka Tumelazimika  kumpa  rungu mwanasheria  wetu ili  kuchukua hatua  kwa  wale wote watakaobainika kuiba kazi zetu  na kuzitumia bila makubaliano yetu.


Tumevumilia tumechoka  sasa  hatuaacha kuchukua hatua kali ili iwe fundisho kwa wenye tabia ya  kuiba kazi zetu na kuzitumia bila  ridhaa yetu .


Ushauri  wangu ni vema  kila mmoja  wetu  kutambua mchango  wa  mwingine kwa  kila anachokifanya  kwani  uendeshaji wa mitandao  hii ni kama  chombo kingine cha habari  lazima kutafuta  habari kwa gharama na  kulipa  wafanyakazi na mahitaji mengine yote  sasa kama wewe  huchangii chochote katika uendeshaji wetu  huna  sababu ya kutumia habari zetu  bure vinginevyo kwa  kila habari utakayoitumia hapa utailipia ama tutachukua hatua  dhidi  yako.

  Kwa  upande wa radio ambazo zinaweza  kutumia habari  zangu kwa Tanzania ni pamoja na Radio Clouds Fm, Radio Uhuru Fm, Radio Mlimani Fm ,Radio  Ebony Fm, Radio Furaha Fm, Radio Ovarcomers Fm, Radio Best Fm ( Ludewa) na Radio V.O.A


Kwa upande wa magazeti ni magazeti ya  Uwazi , Amani, IJumaa, Risasi  na  yote ambayo yanayohusika na kampuni  husika  ,Gazeti la Mwananchi  na gazeti la Daraja Letu .

Wakati upande wa mitandao ya jami inayoweza  kutumia kazi zetu kwa makubaliano ni , Issma Michuzi, Mjengwa, Fullshangwe, Watemi  SHAFFIH DAUDA na Milad Ayo wa Clouds ,  MATUKIO UKBBC SWAHILIVOA SwahiliMAFANIKIO NA MAISHADIAMOND PLATINUMZGLOBAL PUBLISHERSDAILY NKOROMO BLOGCCM BLOG ,Chadema Blog ,  BONGO LEAKS , MATERUNI ,sundayshomari, ASKOFU BOAZ SOLLO ,kamanda  wa matukio ,mohammeddewji,Mbeya yetu ,WAZALENDO25,jamiiforums.com  na  shwari.com zaidi  ya  hapo tutaonana  wabaya nimechoka kuibiwa kazi  zangu .

Pia napenda  kutoa onyo kwa badhi ya  waandishi ambao  wamekuwa  wakitapeli wadau kwa  kujitambulisha  kuwa wanafanya kazi na kampuni ya  Free Community Media’s  kupitia matukiodaima ama francisgodwinblog

Wafuatao ni  wawakilishi wetu  Estha Macha  ( Mbeya) , Elizabeth Ntambala ( Rukwa na Katavi),Juma Nyumayo ( Ruvuma), Tuma Sitta (Mwanza), Carlos Mtoye ( Dar es Salaam),Gustav Chahe , E. Materu , Kayanda MC , Mlalahoi Alwatan,Lukelo Mkami ,  (Iringa) japo wengine  kwa Iringa utawatambua  wiki ijayo Abdulaziz Video ( Lindi) Ally Suleiman ( Zanzibar) Anna John ( Arusha) Frank Ndelwa ( Dodoma) Bazil Makungu ( Njombe) mikoa  mingine  bado tunatafuta waandishi  wawakilishi
Imetolewa na Francis Godwin Blog -mzee  wa Matukio daima

 0754 026 299,0789 28 1030

Barua  pepe .francisgodwin2004@yahoo.com
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA