Home » » SITAKI KUONA ,MVUTANO HUU KILOLO BILA UFUMBUZI NI WANANCHI NDIO WATAKAO TESEKA

SITAKI KUONA ,MVUTANO HUU KILOLO BILA UFUMBUZI NI WANANCHI NDIO WATAKAO TESEKA

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, July 16, 2013 | 1:17 PM

 Mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo Bw Gerald Guninita 
............................................................................................
 Awali  ya  yote  napenda  kuchukua nafasi hii  kumpongeza   mkuu wa mkoa  wa  Iringa Dr Christine Ishengoma kwa  kuamua  kuingilia kati sakata  hili la mvutano  kati ya mkuu wa  wilaya ya  Kilolo Bw Gerald Guninita  ,watumishi  wa Halmashauri ya  Kilolo kupitia  chama chao  cha  wafanyakazi na baraza la madiwani Kilolo .

Ikumbukwe  kuwa  chanzo  cha mvutano  huu ni  hatua ya  mkuu  wa wilaya  hiyo Bw  Guninita kuwaweka mahabusu ya  polisi watumishi  wawili  wa  wilaya  hiyo akiwemo afisa usafirishaji wilaya (T.O) na mtendaji  wa kata kwa madai  ya  uwajibikaji mbovu .

Kwa  upande wa  afisa mtendaji inadaiwa  kuwa alikamatwa na kuwekwa mahabusu mbele ya wananchi katika mkutano wa DC katika kata  yake  eti kwa  kushindwa kuandaa vema mkutano wa mkuu  huyo wa  wilaya mbali ya katika  eneo la mkutano kudaiwa  kuwepo msiba 

Huku kwa upande wa T.O anadaiwa  kushindwa  kutoa usafiri  wa  kupeleka  askari  polisi kulinda  nyumba ya mkuu  wa  wilaya .

Sina  shaka  na hatua  ambazo mkuu wa wilaya  alizichukua ila  nina shaka na mahusiano kati ya  mkuu huyo  wa  wilaya na  watumishi wenzake ambao  ndio tegemeo lake katika  kuisimamia  wilaya  hiyo ili  wananchi waweze  kupata  maendeleo ya haraka.

Binafsi kwa mtazamo   wangu  suala la mtendaji kushindwa  kuandaa mkutano  kutokana na eneo hili  kuwa na msiba  ilikuwa ni vema mkuu huyo wa wilaya pia angeshiriki msiba  huo badala ya  kumkamata mtendaji tena  mbele ya  wananchi  wachache  waliofika  kumsikiliza mbali ya  kuwa na tatizo la msiba  kijijini.

Kwani kiongozi  wa  watu  lazima pia ashiriki katika masuala ya  kijamii kama msiba  na mengine kama  anavyofanya  Rais  Jakaya  Kikwete ,waziri  mkuu Mizengo  Pinda  kwa mfano mdogo Pinda alipofika mjini Iringa na  kutua uwanja wa Ndege  Nduli na kusikia diwani wa eneo hilo Iddi Chonanga amefariki kabla ya  kwenda Ikulu alilazimika  kwenda  kuhani msiba huo kwa  dakika 20 tu na kesho yake  kuungana  na wananchi  wa Iringa katika mazishi huo ni mfano ambao  viongozi  wengine  wanapaswa  kuiga isiwe  wananchi  wanaonekana bora  pale  wewe  unapohitaji kutekelezewa mambo yako.

Lakini katika  suala la T.O Kilolo  kushindwa  kutoa usafiri  kwa askari  polisi wa  kulinda  nyumba ya DC mbali ya  kuwa  ulinzi nyumba za viongozi  unahitajika  ila bado polisi wenyewe  walipaswa  kutafuta njia nyingine  ya kwenda  kutimiza  wajibu  wao  kwa mkuu  huyo wa wilaya  hata kama kwa usafiri  wa  piki piki .

Mbali  na  hilo mkuu wa wilaya kama  mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama  wilaya kabla ya  kumkamata T.O alipaswa kumchukulia hatua mkuu  wa polisi  wa wilaya (OCD) kwa  kushindwa  kupeleka ulinzi kwani suala  hili ndilo  linamhusu  zaidi .

Ila  kwa kuwa  haya  yametokea  tuchukulie  yamepita na yawezekana  kila mmoja atajifunza  ila kwa  sasa  ni suala la kukaa chini na kuanglia mbele  zaidi  badala ya  kuanza  kujengeana chuki ambazo mwisho  wa siku anayeteseka ni mwananchi wa  chini .

Pia kwa  upande  wa mkoa kuna haja ya mkuu  wa mkoa ama katibu  tawala  wa mkoa  kulifanyia kazi haraka suala  hili kwani iwapo  litafanyika kwa  kusua  sua upo uwezekano wa baadhi ya mambo  kusimama hasa  ukizingatia  kuwa mkoa  wa Iringa ndio utakuwa mwenyeji wa kilele  cha mbio za mwenge mwaka  huu na bila shaka maandalizi yake  ni  sasa na kila wilaya msimamizi mkuu wa mbio  za mwenge ni mkuu  wa wilaya  sasa  iwapo hili  lisipofanyiwa kazi haitakuwa njema.

Suala  hapa ni mkuu  wa wilaya  kufuta kauli kwa  kuwaomba radhi watumishi Kilolo kwa  yaliyotokea na kufanya kazi ya  kuwatumikia  wananchi kwa ushirikiano ,itaendelea  Alhamis ila  leo  nasema mvutano  huu  unawatesa  wananchi wa  kilolo  hivyo sasa nasema  hivyo SITAKI KUONA mvutano  huu ukiendelea 
 
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA