Home » » MSTAHIKI MEYA WA MANISPAA YA IRINGA AWAONYA WANASIASA KUACHANA NA KAULI ZA KICHOCHEZI

MSTAHIKI MEYA WA MANISPAA YA IRINGA AWAONYA WANASIASA KUACHANA NA KAULI ZA KICHOCHEZI

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, July 23, 2013 | 2:50 AM
 maombi ya  kumkumbuka diwani Chonanga aliyefariki  dunia.
 madiwani  wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa  wakiwa katika  dua na sara ya kumkumbaka  diwani mwenzao Iddi Chonanga  aliyepoteza maisha  hivi karibuni
Watumishi  wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa  wakimkumbaka  diwani  wa kata ya Nduli marehemu  Iddi Chonanga

MSTAHIKI  meya  wa Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa Amani Mwamwindi amewataka  viongozi  wa  siasa  kuachana na  kauli  za kichochezi ambazo  zinaweza  kuhatarisha amani katika jamii.

Mwamwindi ametoa onyo  hilo  leo  wakati akifungua kikao  cha baraza la madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya  Iringa leo.

Amesema kuwa iwapo  viongozi wa vyama  vya  siasa  hawatakuwa makini na kauli  wanazotoa  kwa jamii  zinaweza kuleta machafuko makubwa kama  ambayo  yaliyojitokeza  hivi karibuni  mjini hapa kwa polisi kulazimika  kutumia mabomu  kutawanya  wananchi.

Mwamwindi  alisema  kuwa hali iliyojitokeza katika Manispaa ya Iringa kiasi cha polisi  kutumia nguvu zaidi ya  kuwatawanya  machinga  haijapata  kujitokeza katika  mji  wa Iringa  toka  nchi  ilipopata  uhuru  wake  mwaka  1961.

Hivyo  alisema  ili  kuendelea  kulinda amani ya Taifa  ni vema  wana  siasa  kuepuka  kutoa kauli za kichochezi  kama njia ya kudumisha amani na kuongeza kasi  ya  wananchi kufanya kazi  za kimaendeleo.

Katika hatua  nyingine Halmashauri  hiyo ya Manispaa ya  Iringa  imepongezwa kwa  kufanya  vema katika matumizi ya  fedha  za wahisani kiasi cha kupewa hati  safi na mkaguzi .

Mwamwindi alisema  kuwa jambo la  kijipongeza katika Halmashauri  hiyo ni kutokana na kupewa hati  safi na hivyo kuwataka  watumishi wa Halmashauri  hiyo kuendelea  kuboresha kasoro  ndogo ndogo  kama njia ya kuendelea  kupata hati safi  zaidi.
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA