Home » » MBUNGE MSIGWA AWAONYA WASOMI AWATAKA KUTUMIA VEMA ELIMU YAO ......

MBUNGE MSIGWA AWAONYA WASOMI AWATAKA KUTUMIA VEMA ELIMU YAO ......

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Tuesday, July 23, 2013 | 2:49 AM

 
 Mbunge  wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa akifungua  mdahalo  wa wazi Asasi  isiyo ya  kiserikali ya Community Integrated Communication ana Culture (CICC) katika ukumbi wa Highalnds mjini Iringa
Add caption
Mkurugenzi  wa CICC Neema Mwamoto akitoa  maelezo ya utangulizi
Washiriki wa mdahalo huo ambao ni  wanavyuo  kutoka mjini Iringa wakifuatilia mdahalo  huo

.......................................................................................

MBUNGE  wa  jimbo la  Iringa mjini Mchungaji Peter  Msigwa amewataka  wasomi  wa  vyuo  vikuu nchini kuacha  kulalamika na uhaba wa ajira  badala yake  kutumia  elimu  yao kujiajiri  wenyewe katika  sekta  zisizo rasmi.

Mbunge  Msigwa ametoa rai  hiyo kwa  wasomi hao wakati wa mdahalo wa wazi ulioandaliwa na Asasi isiyo ya kiserikali ya  CICC inayoongozwa na mkurugenzi wake Neema Mwamoto ,mdahalo  uliofanyika katika ukumbi wa Highlands mjini hapa na mbunge  huyo  kuwa mgeni  rasmi.

Alisema  kuwa  elimu  ambayo  wasomi wameipata  iwe ni elimu ya   kuwawezesha  kupata ajira   badala ya kuendelea  kulia na ajira  za  serikali iliyopo madarakani ajara ambazo  hazipo.

Kwani  alisema  kuwa mbali ya  serikali kuwa na  wajibu wa kuwaunganisha  watanzania katika ajira  ila kutokana na  serikali kushindwa  kutengeneza mazingira mazuri ya ajira ni vema  sasa  wasomi  kuepuka  kulia ajira kama  ilivyo kwa  watu ambao  hawajabahatika  kwenda  vyuo  kusoma.

Hivyo  alisema  elimu  itakayowakomboa  wasomi hao wa vyuo  vikuu kiasi cha  kujivunia ni ile ambayo itawawezesha kujiajiri  wenyewe .

"Acheni  kukata tamaa katika maisha  kwa  tayari  ni  wasomi lazima  kupambana  kupata  kazi za kufanya badala ya  kusubiri kazi  moja ambayo  haipo kwa  sasa"
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA