Home » » DIWANI WA KATA YA NDULI KUPITIA CCM IDD CHONANGA AFARIKI DUNIA MCHANA HUU

DIWANI WA KATA YA NDULI KUPITIA CCM IDD CHONANGA AFARIKI DUNIA MCHANA HUU

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Wednesday, July 3, 2013 | 5:58 AM

Katibu  mkuu  wa Chama cha mapinduzi (CCM) Taifa Bw Kinana akisalimiana na aliyekuwa  diwani wa kata ya Nduli katika Manispaa ya Iringa marehemu Idd Chonanga alipokuwa akipita  mkoa  wa Iringa  kuelekea katika ziara  ya CCM mkoa wa Njombe na hapa Chonanga  alimtania katibu mkuu kuwa yeye  ndie kijigoo wa CCM kata ya Nduli na kamwe kata  hiyo haitakuja ongozwa na upinzani hata kama atakufa ,kushoto ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu (picha na maktaba ya  Francis Godwin Blogu -mzee  wa matukio daima)



Na Francis Godwin, Iringa

CHAMA cha  mapinduzi  (CCM) mkoa  wa  Iringa  kimepata  pigo jingine  baada ya  diwani  wake mwingine  wa kata  ya Nduli  katika  Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa Iddy Chonanga  kufariki duni  mchana  wa  leo katika  Hospitali ya  rufaa ya mkoa  wa Iringa.

Huku  mbunge wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa (chadema) akiungana na  madiwani wa Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa katika  kuomboleza msiba huo na kutoa pore kwa familia yake kwa kumpoteza mzazi .

Mstahiki meya  wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa Aman Mwamwindi  amethibitisha  kutokea kwa  kifo cha  diwani  Chonanga  na kuwa alikuwa kifo  hicho  kimetokea  majira ya saa 8 mchana katika Hospital ya Rufaa ya mkoa  wa Iringa  ambako diwani  huyo alilazwa .

Alisema  kuwa  Chonanga  alifikishwa Hospital hapo leo majira ya saa 12  asubuhi kutokana na tatizo la ugonjwa wa BP ya kushuka ambao  ulikuwa ukimsumbua  na mbali ya madaktari  kuhangaika  kuokoa maisha  yake ili ilipofika majira ya saa  8 mchana  diwani  huyo alifiriki dunia.

Hata  hivyo  Mwamwindi  alisema kuwa  kifo cha  diwani  Chonanga  ni pingo  kubwa ndani ya  Halmashauri  ya  Manispaa ya Iringa  kutokana na utendaji kazi  wa  diwani  huyo katika Halmashauri hiyo kupitia kata  yake ya Nduli.
 
Kwa upande  wake naibu  Meya  wa Manispaa ya  Iringa Gervas Ndaki akielezea jinsi  alivyofanya kazi na  diwani  Chonanga  alisema  kuwa diwani  huyo alikuwa ni  mmoja kati ya  madiwani  wanaojituma  zaidi katika utendaji kazi  hasa kuwatumikia  wananchi  wa Manispaa ya Iringa .

Hivyo  alisema  kuwa kifo cha  diwani  chonanga mbali ya kuacha  pengo kubwa katika  familia  yake  ili kimeacha pengo  katika Halmashauri  ya Manispaa ya  Iringa .

Huku  kwa  upande  wake  mbunge wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA) akitoa  pore ndugu jamaa na marafiki   kufuatia  kifo cha  diwani  Chonanga .

“Ni  tukio la kusikitisha  sana  tunapoondokewa na mwenzetu  tuliyemfahamu  vizuri na hata  kushuhudia mchango  wake katika jamii….japo  wakati mwingine  tunakuwa katika masuala ya  kisiasa  ila pale  kati  yetu  anapofariki  dunia  masuala ya siasa tunaweka kando na kuungana katika maombolezo “

Alisema  mbunge Msigwa kuwa baada ya  kupata  taarifa ya kifo cha  diwani Chonanga  alipata  kuungana na  madiwani  wa Halmashauri ya  Manispaa ya Iringa kwenda katika Hospital ya mkoa wa Iringa kwa ajili ya kuuhifadhi mwili wa  diwani  huyo.

Kwa  upande  wake  mwenyekiti  wa Halmashauri ya  wilaya ya  Kilolo Joseph Muhumba mbali ya  kutoa pore kwa  mstahiki meya  wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa  kufuatia kifo cha  diwani  Chonanga  bado  alisema  kuwa  kwa  upande wa madiwani wa Kilolo  wamepokea kwa masikitiko makubwa  taarifa ya  kifo  cha  diwani  huyo kutokana na njinsi ambavyo walivyoutambua vema mchango  wake 
 
Kifo cha  diwani  Chonanga  kinafanya  idadi ya madiwani  wane wa  CCM katika mkoa  wa Iringa  kufariki  dunia  ndani ya  kipindi  kifupi cha miezi mitatu  baada ya  kifo cha kwanza ndani ya kipindi hicho kumhusisha  diwani wa kata ya Ukumbi Jesco Ngimba  aliyefariki dunia mwezi wa May  na  ni miezi mine toka  diwani wa kata ya Ngang’ange Bahath  Lwesa  kufariki wote  wakiwa wa  Halmashauri ya  wilaya ya  Kilolo .
 
Mbali ya  wilaya ya  Kilolo kupoteza  madiwani Diwani  wa kata ya Mbalamaziwa wilaya ya  Mufindi marehemu  chelesi  aliyefariki  dunia mapema  mwaka  huu .
 
Hata  hivyo  hadi sasa kutokana na vifo vya  madiwani  hao  wane tayari uchanguzi mdogo  umekwisha fanyika katika kata  ya Ng’ang’ange  jimbo la  Kilolo ambako  mgombea  wa CCM alipata  kushinda na katika kata ya Mbalamaziwa wilaya ya Mufindi ambako pia  mgombea wa CCM alipata  kushinda  huku kata  ambayo ilikuwa  wazi ni kata ya Ukumbi ambayo ilikuwa bado kufanya uchaguzi  na sasa  kifo cha Chonanga  kinafanya jumla ya kata  mbili kuwa  wazi bila uwakilishi wa  diwani.
 
Marehemu  Chonanga  enzi  za uhai  wake  alikuwa akikabiliwa na kesi mbili katika Mahakama ya hakimu mkazi  mkoa wa Iringa ikiwemo kesi ya  kutishia  kumuua kwa maneno mbunge  wa  jimbo la Iringa mjini mchungaji Msigwa  kinyume cha kifungu cha 89 cha Kanuni ya Adhabu kifungu kidogo cha 2 (a) sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002 na  kosa la  pili Chonanga alikuwa akishitakiwa kwa kutishia kumuua, Diwani mwenzake wa Kata ya Mivinjeni, Frank Nyalusi kesi  ambayo ilikuwa bado kutolewa hukumu .
MWISHO
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA