Home » » BENK YA CRDB NCHINI YAZIDI KUPONGEZWA NA SACCOS RUKWA NA KATAVI

BENK YA CRDB NCHINI YAZIDI KUPONGEZWA NA SACCOS RUKWA NA KATAVI

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Saturday, July 13, 2013 | 10:22 AM

Meneja  wa  tawi la  CRDB Sumbawanga  akimkabidhi  cheti  Jonas Raphael  (kulia)  leo

Malietha  haule Uwami Saccos manispaa ya  Sumbawanga  akipokea cheti  chake  cha ushiri  leo


Mgeni  rasmi  meneja  wa CRDB tawi la  Sumbawanga   Tom  Aduwa akimkabidhi  cheti mmoja kati ya  washiriki
Mwakilishi  wa  washirki  wa  mafunzo hayo  Peter Kasomo kutoka Nkasi Teacher's Saccos  akitoa  pongezi kwa niaba ya  washiriki wengine
Meneja  wa uelimishaji na  uwezeshaji  wa  CRDB MFSCL - HQ Godwin L. Maimu  akizungumza na  wakufunzi  wa mafunzo hayo  usiku  huo


  Meneja  wa uelimishaji na  uwezeshaji  wa  CRDB MFSCL - HQ Godwin L. Maimu akitoa  ufafanuzi  juu ya mafunzo hayo ,kushoto ni meneja  wa CRDB Sumbawanga Bw Tom  Aduwa  na  kulia Bw Emma msimamizi  wa mafunzo hayo Sumbawanga 
.....................................................................................
 
   Meneja  wa uelimishaji na  uwezeshaji  wa  CRDB MFSCL - HQ Godwin L. Maimu  alisema kuwa  CRDB ndio benk pekee  nchini  Tanzania  katika kuwawezesha  wananchi kupitia  vyama vya ushiriki  vya kuweka na  kukopa (SACCOS)  hivyo  alisema  wataendelea  kuwawezesha zaidi.

Washiriki 93  ila  walioshiriki ni washiriki 82 ndio  wamepata  kujitokeza katikamafunzo hayo na kuwa  CRDB  wataendelea  kutoa mafunzo kwa  Saccos hizo

Alisema  kuwa kwa takribani wiki nzima  wameendelea  kuwapa  elimu  viongozi wa Saccos  mkoa  wa Rukwa  ili kujua mambo mbali mbali yakiwemo ya  maadili ya  viongozi na uandishi bora wa  ripoti pamoja na utunzaji wa  kumbukumbu ili kuwezesha kuendesha  Saccos zao kisasa zaidi.

Hata  hivyo alisema  kuwa  somo ya  sheria ya ushiriki wamefundishwa  viongozi hao na sasa  wanatambua vema  suala la  ushirika pamoja na kujua majukumu yao katika uendeshaji wa Saccos  hizo.

Maimu  alisema kuwa elimu  dhidi ya utoaji mikopo kwa  wanachama  viongozi hao wamefundishwa na kutambua  vema namana ya  kukopesha  wanachama na  kuwawezesha  wanachama kunufaika na mikopo  hiyo .

Huku  suala la majanga  limefundishwa kwa  viongozi hao  pamoja an kujiunga na bima  mbali mbali kama  njia ya  kuwakwamua  wanachama  pale  wanatakapo kumbwa na majanga mbali mbali  na kuwa  ni lazima  Saccos  kujiunga na bima ili pale  wanapopatwa na majanga  kuweza  kunufaika na bima .
 
Akielezea  kuhusu suala la ujarisiamali alisema kuwa mafunzo hayo yametolewa na hivyo CRDB itapendezwa  zaidi kuona viongozi hao  wanakwenda  kuendesha  Saccos  zao  kisasa   zaidi.
 
 Wakati huo huo wajumbe  wa bodi za  vyama vya  ushiriki  wa  vya kuweka na kukopa  (SACCOS)  mkoa  wa  Rukwa na katavi wamedai kuwa  jitihada zinazofanywa na benk ya  CRDB nchini Tanzani katika kutoa elimu na mikopo wa  SACCOS nchini  zinaendena na sera ya  serikali katika kukuza ushirika nchini.
Akitoa  pongezi hizo katika ukumbi wa Riboli mjini Sumbawanga kwa niaba ya  washiriki  wengine katika hafla ya  kukabidhi  vyeti kwa  washiriki wa  mafunzo hayo ya  siku saba Peter  Kasomo kutoka Nkasi Teacher's Saccos  
Kasomo alisema  kuwa  pamoja na Tanzania kuwa  na benk nyingi  ila  jitihada  zinazofanywa na CRDB katika kuziwezesha  Saccos nchini ni  jitiahda za  kuigwa na asasi  nyingine za  kifedha hapa nchini.
 
Alisema  kuwa  kuwa muda  wa  wote ambao  wamepata  kushiriki maunzo hayo wamepata  kushiriki mada mbali mbali ikiwemo ya  maana ya  Saccos  bora na maadili ya viongozi, sheria ya ushirika, utunzaji  wa mahesabu  na uandaaji  wa  ripoti  (MIHAMALA) , udhitibi wa majanga  na  bima pamoja na Ujasiliamali na masoko.
Alitaja masomo mengine ambayo  wamejifunza  kuwa ni  sera na taratibu  za  bidhaa na huduma , kazi za  wafanyakazi   wa Saccos na taratibu za mikoppo na upangaji  wa bei.
Hivyo  alisema kuwa masomo hayo ni  mwanzo za Saccos  zao  kufanya  vema na hata  kujikomboa  zaidi kiuchumi. 
Kasomo  alisema kuwa mafunzo  hayo yatawawezesha  kwenda kujikomboa zaidi na kuboresha  Saccos  zao  huku akiomba  CRDB kuendelea kuwa karibu na Asasi hizo za  kifedha vijijini  .
Kwani alisema kuwa mbali y akuwa na benki nyingi ila CRDB imeendelea  kuwa mkombozi wa kweli kwa  asasi hizo za kifedha  vijijini na kuwa wataendelea kujenga ushirikiano na benk hiyo ya CRDB hapa nchini.
Kwa  upande  wake  meneja  wa CRDB tawi la  Sumbawanga   Tom  Aduwa  alisema  kuwa  benk yake  itaendelea  kuwa karibu na  Saccos  hizo huku akitaka  mafunzo hayo  waliyopata  viongozi kutumiwa vizuri ili  kujenga  uwezo zaidi kwa asasi zao.
Alisema kuwa iwapo  viongozi hao  watatumia vema mafunzo hayo  upo uwezekano  wa  Saccos  zao kupiga hatu kabwa katika  maendeleo  . 
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA