Home » » BARAZA LA MADIWANI KILOLO LAAGIZA WAUGUZI WANAO KUDISHA AMBULENCE NA KUPOKEA POSHO KWA MGONJWA HOSPITAL TEULE YA ILULA KUCHUNGUZWA ........

BARAZA LA MADIWANI KILOLO LAAGIZA WAUGUZI WANAO KUDISHA AMBULENCE NA KUPOKEA POSHO KWA MGONJWA HOSPITAL TEULE YA ILULA KUCHUNGUZWA ........

Written By mzee wa matukiodaima habari bila uoga on Thursday, July 11, 2013 | 4:14 AMMfano wa gari  la wagonjwa

 Madiwani  wakimkumbuka  aliyekuwa mkurugenzi  wa Kilolo na diwani wa kata ya Ukumbi

 Diwani mteule wa kata ya  Ng'ang'ange  wilaya ya  Kilolo Msuva (kushoto) akila  kiapo mbele ya  mwenyekiti wa Halmashauri ya  Kilolo Joseph Muhumba leo anayeshudia wa  pili kulia ni kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya  Kilolo Benison Kilangi
 Mbunge  wa  jimbo la Kilolo Prof Peter Msolla kulia akishuhudia zoezi la kuapishwa  diwani mteule wa kata ya Ng'ang'ange  leo
 Kiapo  cha utii  kwa  diwani mteule

 Mwenyekiti wa Halmashauri ya  Kilolo JOseph Muhumba  akifungua kikao cha baraza la madiwani leo


BARAZA la madiwani katika  Halmashauri ya  Wilaya ya Kilolo mkoani  Iringa limeagiza kufuatilia  tuhuma  zilizotolewa na mmoja kati ya madiwani  wa baraza  hilo kuhusiana na Hospital  teule  ya Ilula  Ilula kuwakodisha  gari  la  wagonjwa (Ambulence) wagonjwa  wanaopewa  rufaa kwenda  Hospital ya mkoa pamoja na kuomba posho ya Tsh 10000 kwa mgonjwa .

Hatua  hiyo  imekuja kufuatia madai  yaliyotolewa na diwani viti maalum tarafa ya Mazombe Anna Kulanga kuhusiana na mwenendo  usiofaa unaofanywa na  uongozi  wa Hospital  hiyo teule ya  Ilula kwa kuwakodisha Ambulence wagonjwa.

Diwani  Kulanga alisema kuwa hatua  iliyofikiwa katika  Hospital  hiyo si nzuri kwani  siku za hivi karibuni walipata  kukodisha  Ambulence  hiyo kwa majeruhi wa ajali ambae alitakiwa kukimbizwa katika  Hospital ya Rufaa ya  mkoa wa  Iringa ila mbali ya majeruhi  huyo kupoteza maisha njiani ila bado  wauguzi  wawili waliomsindikiza majeruhi  huyo  walitaka  ndugu  kulipa gharama ya Ambulence  kiasi cha  Tsh 40000 pamoja na kuwalipa posho ya Tsh 20000 wauguzi  wawili  walioongozana na majeruhi  huyo.

Kwa   diwani  wa  viti maalum tarafa ya  Mahenge Shera Ngailo  alitaka  kuundwa kwa kamati  ya kuchunguza  lugha chafu  ambayo imekuwa  ikitolewa na wauguzi  wa  Hospital hiyo  teule ya  Ilula kwa  wanawake  wajawazito.

Alisema  kuwa kumekuwepo na malalamiko ya muda  murefu  kutokana na lugha za matusi zinazotolewa  kwa  wajawazito  kutoka kwa wauguzi hao  hivyo  kutaka  wauguzi  wenye tabia  hiyo  kuchukulia  hatua ya  kinidham .

Hata  hivyo kaimu  mganga mkuu  wa wilaya ya  Kilolo  Michael Simwanzi akijibu madai  hayo ya  baraza la madiwani  dhidi ya  gari la wagonjwa  kukodishwa kwa wagonjwa na wauguzi kuomba  posho kwa wagonjwa alisema  kuwa ni kinyume na taratibu  za wizara ya afya .

Alisema  kuwa  kimsingi gari hilo la  wagonjwa mafuta  yanajazwa na Halmashauri na  kuwa  wauguzi  wanaolsindikiza wagonjwa  hawapaswi  kulipwa  posho  yeyote  toka kwa mgonjwa .

Hivyo  alisema  uongozi  wa afya  wilaya ya  Kilolo  utafuatilia  suala hilo  ili kuondoa kero kwa wagonjwa  wanaofika  katika Hospital  hiyo.

Huku kaimu mkurugenzi  wa  Halmashauri ya  Kilolo Benson Kilangi  aliomba baraza  hilo la madiwani  kuweza  kutoa muda  wa  kulifanyia kazi  suala hilo ikiwa ni pamoja na hatua  zitakazochukuliwa  toka kwa  wahusika  wa suala  hilo.

Mwenyekiti wa Halmashauri  ya  wilaya ya Kilolo Joseph Muhumba alitaka  ofisi ya  mkurugenzi wa Halmashauri  hiyo  kulifanyia kazi suala  hilo la kikao kichacho  cha baraza la madiwani  kuhakikisha  wanakuja na jibu  la hatua  zilizochukuliwa kwa  wahusika.

" Lengo la  serikali ni  kuendelea  kuboresha huduma za afya  kwa wananchi wake  hivyo hatua ya kufumbia macho  kero kama hizo za wagonjwa  kukodi gari la wagonjwa na kuwalipa posho  wauguzi  si utaratibu hivyo lazima  wahusika  wachukuliwe hatua kali ili iwe  fundisho kwa  wengine"
Share this article :

Post a Comment

 
blog designer Hoseaplatnum
Copyright © 2013. MATUKIO DAIMA - All Rights Reserved
Template Created by Hoseaplatnum Published by Francis Godwin
Proudly powered by FREE COMMUNITY MEDIA